“Pamoja daima, katika safari ya sakaramenti ya ndoa” ni kauli mbiu ambayo imechaguliwa
na itakayoongoza katika majimbo na katika maparokia ya ujerumani wakati wa kuadhimisha
sikukuu ya familia tarehe 31 Desemba 2017, na ambayo itasikindiza Kanisa la Ujerumani
kwa mwaka mzima wa 2018.
Na kwa maana hiyo kitabu kidogo cha ufafanuzi zaidi kimetolewa katika kutoa jibu
la maombi ya Baba Mtakatifu Francisko kuhusu kuutafakari na kuunyambulisha Waraka
wake wa Amoris Laetitia, (Furaha ya upendo) ili kuhusisha na kujumuisha kwa kiasi
kikubwa jumuiya ya kikristo katika kuwasindikiza familia katika ndoa.
Kitabu kidogo hicho kimegawanyika katika sehemu nne ambazo zinawakilisha baadhi ya tafakari muhimu ya uzoefu ambao tayari upo ndani ya familia na kusaidia kutoa neno muhimu la kuweza kutambua nini maana ya ndoa ya kikristo. Aidha katika kitabu kidogo hicho kimeandikwa hata sala na maandhimisho mbali yenye mada ya ndoa vilevile wameweka mkusanyiko wa viunganishi vya vitabu vikubwa mbalimbali vyenye marejea ya kupata ufahamu zaidi vilivyopo nchini Ujerumani.
Mwenyekiti wa Tume ya Baraza la Maaskofu wa Ujerumani, kwa ajili ya ndoa na familia, Askofu Mkuu Heiner Koch wa Jimbo Kuu la Berlin, katika utangulizi wa kitabu hicho kidogo ametoa ufafanuzi kuwa, majadala mkali uliotokea mwaka huu 2017, kuhusiana na ufunguzi wa ndoa ya kiraia wa jinsia moja, umeonesha kuwa dhana ya sakramenti ya ndoa bado haitambuliwi kwa walio wengi, kwa maana hiyo wameamua kuweka nyenzo kama hiyo, ili kuanzia katika maparokia, waamini wanaweza kujadiliana na kukabiliana na mada hiyo muhimu hambayo haiwezi tena kukosa mwelekeo na kuzingatia umuhimu wake kama ilivyokuwa mwanzo.
Askofu Mkuu Koch anafafanua tena kwamba; moja ya matatizo, ni kudumisha uimara wa uhusiano kati ya mafundisho ya Kanisa juu ya ndoa na michakato yake. Ni siku nyingi sasa wamependekeza kufanya maandalizi ya ndoa katika majimbo na majimbo makuu wakiwa na madhumuni ya kukabiliana na changamoto za jamii inayobadilika na zaidi, hasa kuwa na wasiwasi wa kukutana na watu katika hali zao za maisha.
Sr Angela Rwezaula
Vatican News
All the contents on this site are copyrighted ©. |