2017-12-29 15:07:00

Ni watu 19,000 wa kujitolea katika maandalizi ya Ziara ya Papa nchini Cile!


Kuwa mtu wa kujitolea kipapa ni kama kutumwa katika kujenga Kanisa ambalo ni nzuri zaidi na  ulimwengu ulio baora. Haya ni maelezo ya Francica Jose’ Miranda mmoja kati ya  maelfu na maelfu ya watu wa kijitolewa waliojikwamua kusaidia katika maandalizi ya ujio wa Baba Mtakatifu Francisko, anayetarajia kwa mara nyingine tena  katika Bara la Amerika ya Kusini kwa namna ya pekee katika nchi ya Cile na Peru  mwezi Januari, 2018.

Francesca alikuwa katika mkutano wa Tume ya Kitaifa kwa ajili ya maandalizi ya ziara ya Baba Mtakatifu iliyoitishwa na Rais wa nchi ya Cile,  bi Verónica Michelle Bachelet Jeria, uliofanyika tarehe 27 Desemba 2017 katika jumba la Moneda. Francesca amesema kuwa,  amemsikiliza kwa makini Rais wa nchi akisisitiza juu ya ziara ya Baba Mtakatifu na kwamba,itakuwa ni nafasi ya makutano na kutafakari katika ulimwengu wa wakatoliki, hata kwa nchi nzima. 

Halikadhalika amesema,kushiriki katika maandalizi ya ujio wa Papa nchini Cile ni uzoefu usio sahaulika, kwa maana ni siku chache zimebaki, kabla ya kufika kwamke, lakini ambazo tayari zimejaa maandalizi kiroho,shauku, furaha na maombi mengi. Aidha amesisitiza juu ya tendo na sababu ya kujituma kuhudumia kwa furaha, mahali popote ambapo atapangiwa  na kwamba, marajio yake baada ya ziara ya Baba Mtakatifu nchini Cile ni kwamba, nchi inaweza kubadilika kuwa mpya.Na pia  watu wa Cile wanaweza kupokea kila ujumbe  wa amani utakaotolewa na Baba Mtakatifu kwa jina la Yesu. Na kwanjia hiyo upo ulazima wa   kusikiliza  kwa makini na kutafakari maneno yake, zaidi kujikita kwa dhati katika  matendo.

Tume ya taifa kwa ajili ya maandalizi ya Papa Francisko nchini Cile imeundwa na watu19,000 waliojiandikisha kujitolea na kushiriki katika kuandaa ziara yake ambayo atatembelea miji ya Santiago, Iquique na Temuco nchini Cile,  kati ya tarehe 15 na 18 Janauri 2018.

Angela Rwezaula
Vatican News

 








All the contents on this site are copyrighted ©.