2017-12-28 14:37:00

PERU:Sehemu ya moja ya msitu wa Amazoni umepewa jina Papa Franciscko!


Sehemu moja ya msitu wa Amazon nchini Peru umepewa jina jipya kwa ajili ya heshima ya Baba Mtakatifu Francisko. Ni uamuzi wa kabila moja asili nchini Peru ambao wameamua kutoa eneo hilo lenye ukubwa wa ekari 1,800 na kuliita jina “Nihii Eupa Francisco” ikiwa na maana “kichaka cha Francisko” katika lugha ya kabila la amabuaca.

Naye waziri wa Mazingira wa nchi ya Peru, akielezea zaidi amesema kuwa, uamuzi wa kuita jina eneo hilo, umechukuliwa kwa sababu ya utambuzi  na wasiwasi wa Baba Mtakatifu Francisko katika utetezi katika kuhifadhi mazingira dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa. Eneo hilo linapatikana katika jumuiya ya watu wa asili wa Boca Pariamapu, katika mkoa wa (Madre de Dios) maana yake  Mama wa Mungu. Mji Mkuu wa Mkoa ni Porto Maldonado, mahali ambapo Baba Mtakatifu atatembelea tarehe 19 Januari 2018, akiwa katika ziara yake ya kitume. Na msitu wa Ammazon ulikuwa tayari umesha zungumziwa wakati wa ziara ya kitume ya Baba Mtakatifu Francisko  akiwa nchini Colombia  katika  siku ambayo ilikuwa inahusu kuombea  mazingira huko Villavincencio 2017.

Akielezea zaidi kuhusu Sinodi kuhusu kanda ya Amazon, mbele ya Taasisi ya Populorum Progressio kwa ajili ya Amerika ya Kusini, hivi karibuni mjini Roma, Kardinali Lorenzo Baldisesseri, katibu wa Sinodi ya Maaskofu,  amesisitiza umuhimu wa mada ya ekolojia katika sinodi ijayo, pia amewatangazia  juu ya uwepo wake katika ziara ya Baba Mtakatifu kutokana na mwaliko na REPAM, ambayo ni Mtakandao wa Kanisa la Kanda ya Amazon unaojikita katika jitihada ya kuunda jumuiya za pamoja ili kukabiliana na matatizo ya ukataji miti hovyo wa misitu.

Pamoja na hayo, mada ya ekolojia inaendana na ile ya utetezi na ulinzi wa jumuiya ndogo ya watu asili. Baba Mtakatifu  daima amakuwa akionesha nguvu na fursa ambazo katika tamaduni tofauti zilizopo Amerika ya Kusini, imekuwana tabia ya kutelekeza ukoloni wa kiitikadi ambao kwa katika bara la Amerika ya Kusini imefanya uzoefu huo tayari kutokana na kwamba utamaduni asili ulikuwa umetaka kuondolewa kabisa.

Kazi kubwa na yenye  thamani ya utamaduni mahalia ilikuwa imefanywa na shirika la Yesu (JESUIT). Na ndiyo maana ya umakini ambao umesababisha kutoa uamuzi wa kuita jina la Baba Mtakatifu eneo hilo. Jumuiya ya watu wa Boca Pariampu imeundwa na wakazi 180, waliokusanyika katika makundi ya familia 20 hivi. Ni moja ya jumuiya pekee ya Mama wa Mungu  wa kabila la amabuaca, maana yake wana wa Kapibara, yaani mnyama ambaye katika historia anataka kuimba kwa lugha ya asili ya watu hao.

Msitu ambao wanaishi watu hawa ni mzuri sana, mahali ambapo wanaishi tai, chui, hata mimea mizuri na mikubwa inayojumuisha, miti ya matunda (chestnut) na mierezi. Baba Mtakatifu anawatazama watu hawa wa kiasili kwa moyo wa huruma. Halikadhalika Baba Mtakatifu, ameonesha hata thamani hiyo katika misa ya Mama yetu wa Guadalupe tarehe 12 Desemba 2017 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. Na siku iliyokuwa ikifuatia tarehe 13 Desemba 2017 alikutana na Taasisi ya Populorum Progressio ya Amerika ya Kusini, ambapo wakati wa mazungumzo yao ya faragha ambayo hakutangzwa, alisema kuwa watu wa asili waliikomboa Bara la Amerika…

Sr Angela Rwezaula
Vatican News.

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.