2017-12-27 14:08:00

Noeli ni sikukuu iwapo kuna mshikamano wa kuondoa majanga ya historia


Kutakiana heri za Noeli ni kutakiana matumaini na kuwa na shauku kubwa ya kwamba historia ya uchungu na ugumu wa maisha ambayo mara nyingi binadamu anakabiliana  nayo iweze kuisha. Ni maneno ya Kardinali Francesco Montenegro ambaye ni Askofu mkuu wa Jimbo Kuu la Agrigento lililoko kisiwani, Kusini mwa Italia wakati wa kutoa matashi mema ya sikukuu ya Noeli kwa waaamuni wote kwa njia ya video.

Katika ujumbe huo wa video anasisitiza kuwa, iwapo yule mtoto alikuja huko Betlehemu, ni kwasababu dunia kwa haraka uweze kuwa na  utofauti na iweze kutambua namna ya kuchagua vitu vyenye thmani kubwa. Lakini kwa bahati mbaya, bado hatujatambua hilo, kwa maana hatujali na hatujuhi kwamba kutojali huko kunaondoa taratibu na kwenda mbali na ukweli kutoka katika ukweli,aidha kuwa mbali na mwingine.

Hata hivyo Kardinali Montenegro pia ameonesha masikitiko na  kukumbusha huzuni mwingi kwa watu wanao uishi, hasa wale ambao kwa namna moja au nyingine hawawezi kufanya sikukuu ya Noeli ili wapate kuona siku mojawapo ya pekee, na badala yake wanazidi kuona ongezeko la hali mbaya ya maisha, kuona wengine wanasheherekea, na wengine wamewekwa kandoni na kusahauliwa.

Na kwa njia hiyo mawazo yake yote yamewaendea kwa wale wote wanaoteseka kimwili au kiroho. Akikumbuka wazee wengi, familia zenye kiu, wasio kuwa na ajira au nyumba za kuishi, wahamiaji, wakimbizi, vijana wengi ambao wanatazama siku zikipita bila kujua wanafanya nini, bila kufikiria wakati endelevu.

Na mwisho anafikiria kwamba heri ya sikuu za Noeli zinaweza kuwa za kweli iwapo wote wanaweze kuhisi kweli  historia yao ya maisha inaweza kubadilika kwa maana, Noeli haikamilishwi na mtoto kuzaliwa  pangoni tu iwapo bado kuna wengine wanazaliwa katika mitumbwi, njiani, katika watu walio achwa peke yao , kwa wazazi wengi wanaotafuta ajira bila kupata. Ni noeli katika historia ya majanga, na hivyo iwapo wanataka mabadiliko, basi Noeli inategemea na sisi wenyewe , kwa maana yak ile ambacho tutajikita katika historia ili ipate kubadilika kwa kila binadamu. Amemaliza Kardinali Montenegro!

Sr Angela Rwezaula
Vatican News

 








All the contents on this site are copyrighted ©.