2017-12-23 09:09:00

Tafakari ya Pili Majilio 2017 Vatican:Nafasi ya Yesu katika maisha ya binadamu!


“Mara baada ya kutafakari juu ya nafasi ya Yesu inavyojikita katika dunia, kwa kutazama kwamba, yote yalifanyika kwa njia yake na Kristo ni muumba ; sehemu ya pili ni kutafakari ni nafasi gani ya Kristo inakuwa kama kiini  cha maisha ya Binadamu hasa uwepo katika nafasi na nyakati“. Ni maneno aliyo anza nayo Padre Raniero Cantalamessa, Mhubiri mkuu wa nyumba ya Kipapa, akiwepo hata Baba Mtakatifu Francisko Ijumaa tarehe 20 Desemba 2017.Ilikuwa ni tafakari  ya pili na ya mwisho kabla ya sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana ni tafakari iliyotolewa katika Kikanisa cha “Mama wa mkombozi” “Redemptoris Mater” mjini Vatican.

Mada ya ya tarehe 22 Desemba imetokana na somo ni Yesu Kristo, jana , leo na daima kutoka katika kitabu cha Waebrania 13,8: uwepo wa Yesu katika nyakati. Padre Cantalamessa amesema, Misa ya Mkesha wa Noeli katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, ilianzishwa tena  mara baaada ya Mkutano wa Mtaguso Mkuu wa II wa Vatican ikiwa na  wimbo wa zamani wa Kalenda ya Mashahidi wa Roma.  Wimbo unaoelezea kuzaliwa kwa Yesu Kristo umebadilika kulingana na nyakati.  Pamoja na hayo Padre Cantamalessa ameorodhesha baadhi ya sentensi zilizomo katika maandishi ya mabadiliko hayo.

Mabadiliko hayo ni kama vile:“Baada ya kupita karne nyingi ya  uumbaji wa dunia (…); karne 13 ya wana wa Israeli kutoka Misri chini ya uongozi wa Musa; karibia miaka elfu tatu baada ya Daudi kutabarukiwa  kuwa Mfalme wa Israeli (…); Kipindi cha siku 193 za Olimpiki; katika mwaka wa 752 tangu kuundwa kwa Roma; katika mwaka wa 40 wa ufalme wa Kaisari Ottaviano Augusto: wakati dunia yote ilikuwa inatawaliwa na amani, Yesu Kristo, Mungu milele na Mwana wa Baba milele, akitaka kukomboa nchi yake, akatungwa mimba kwa njia ya roho Mtakatifu, ilipita miezi 9, akazaliwa Betlehemu ya Yuda na Bikira Maria, akawa mwanadamu”

Padre Cantalamessa ameendelea kuwa, ufafanuzi wa kuhesabu katika nyakati , kuanzia mwanzo kwa kuelezea matukio mbalimbali ndiyo ilikuwa inatarajiwa mabadiliko ya kina ya kuja kwa Kristo hata kama hayakutokea kwa hara na mara moja. Aidha amesema kuwa,mwandishi Oscar Cullmann, katika tafiti zake mara moja, alitambua na kuandikia kitabu  “Kristo na wakati” akilezea namna wazi ya nini maana ya mabadiliko hayo kwa namna ya kibinadamu katika kuhesabu nyakati.

Hiyo ni kwasababu amesema kuwa, sisi mara nyingi tunasumbuka kutka kujua zaidi  tangu kipindi cha mwanzo, yaani wa kuumbwa kwa dunia, kipindi cha uamisho wa kwa Wamisri, kuundwa kwa Roma, kutokana na maendeleo makubwa kuelekea  wakati endelevu kwa maana ya usio kuwa na mwisho. Tunaanza na kipindi cha kati ambacho ni Kuzaliwa kwa Bwana, tunahesabu kipindi kinachoendelea kwa namna ya kuona ukuu kuelekea kwake, karne ya nne baaada ya Kristo, kwa namna ya kukua katika kipindi kinachofuata yaani, karne moja, mbili au milenia mbili baada ya Kristo kuzaliwa na kwa njia hiyo siku chache tunaadhimisha miaka 2017 ya tukio hilo.

Padre Cantalamessa anaendelea kufafanua,Kristo ni matukio na sakramenti, kwasababu ni uthibitisho wa upeo wa Kristo katika historia na katika nyakati. Katika yeye, ni uwepo halisi wa historia ya uokovu, kama tusonavyosoma katika kitabu cha waebrania, Ni Kristo, jana, leo na daima (Ebr 13,8), japokuwa si kwa namna moja . Kristo yupo hata katika  maandiko Matakatifu ya Agano la kale, yeye  kama sura na matukio ambayo yanatimilizika katika  nyakati za  Kanisa, kwa njia ya sakramenti.

Nafasi yake inatangazwa katika kuandaa matukio, wakati sakramenti inamwadhimisha na kufanya awepo leo hii kwa maana ya mwendelezo wa muda mrefu. Ndiyo maana Liturujia inatufanya tuadhimishe Noeli  kwa kusema,“leo Kristo amezaliwa, leo hii ametokea Mwokozi, (Hodie Christus natus est, hodie Salvator apparuit”:  Aidha ni uthibitisho huo unaendelea katika mafundisho ya Barua za Mtakatifu Paulo na Agano la Kale, matukio yote na wahusika wakuu wanathibitisha kuwa Kristo ni nabii au mfano wake. Na uthibitisho wake unajieleza kwa makini katika Injili, japokuwa maneno mengi yametokana na Agano la Kale.

Maana ya kusema  Kristo yupo katika Agano jipya na Kale  kama kwenye matukio maana yake ni kuthibitisha kwamba ni jambo la aina yake la kihistoria ambalo linamtazama Yesu, kwa karibu, kwa namna ya pekee katika fumbo la Pasaka, kifo na ufufuko wake. Kama inavyothibitisha katika Kitabu cha Waebrania kwamba tendo hilo si mara moja tu bali, sasa, nyakati hizi zinapokaribia mwisho wake, yeye ametokea mara moja tu kuondoa dhambi kwa kujitoa yeye mwenyewe dhabihu (Ebr  9, 26-28). Na kila mara mlapo mwili na kunywa damu yake mwatangaza kifo cha Bwana hadi atakapokuja (1 Cor 11, 26).

Lakini wanapoeleza juu ya uwepo wa Kristo katika historia ya uokovu,kama sura , kama tukio na kama sakaramenti,lazima kuhepuka makosa mengine yaliyotokea katika baadhi ya waandishi wa kutenga historia ya binadmu katika sehemu tatu, yaani nyakati za Baba kama kipindi cha Agano la Kale, kipindi cha kati kama vile cha mwana kwenye Agano jipya na  kipindi cha kuja Roho Mtakatifu ambacho ni kipindi cha Kanisa.

Padre Cantalamessa amesisitiza kuwa, tukio la Kristo halijawahi kugawanyika katika hatua tatu za kihistoria badala yake yeye ni kitovu, yeye yupo ndani ya wakati,kwa maana yupo kabla ya kuja kwake na yupo hadi sasa kwa maana ya kwamba wakati wote yeye ni kiunganishi na ndiyo maana katika orodha ya matukio ya historia katika uenezi wa hesabu wanaandika  kabla ya /Baada ya Kristo.(KK/BK) Uenezi wa

Makutano yanayobadilisha maisha: kama kawada ya kutaka kuondoka katika dunia yetu ndogo kuelekea hadi iliyo kubwa,katoka historia ya ulimwengu kufikia historia binafsi, kwa maana ya kutoka katika taalimungu kufikia kuwa maisha. Padre Cantalamessa amesema, mtazamo huo wa matukio ya ulimwengu, Kristo ametambuliwa kuwa kiini katika nyakati, katika historia; hiyo isiwe ni sababu ya wakrsto kujidai na kuona ushindi, bali iwe ni fursa kwa ajili ya kufanya tathimini ya dhamiri binafsi. Swali rahisi la kuanizani kwamba Kristo ni kitovu cha maisha, katika udogo wa historia yangu binafsi. Katika muda wangu na je anachukuia nafasi yangu vipi kinadharia au kimatendo? Ni ukweli wa kufikiriwa au wa kuuishi? .

Padre Canatalamessa amethibitisha kuwa, sehemu kubwa ya watu yapo matukio amnayo yanagawanyika katika sehemu mbili, yaani mwanzo na baadaye, kwa mfano walio olewa au wenye ndoa,wamegawanyika katika maisha sehemu mbili: kabla ya kuoa na kuolewa, mapadre nao kabla ya kuwekwa daraja la kikuhani na baada, watawa, kabla ya kufunga nadhiri na baada.

Lakini hiyo ni tofauti na maisha ya Mtakatifu Paulo, ambapo maisha yake yamegawanyika katika shemu mbili kaiji mganyiko huo si wa ndoa au daraja; yeye mwenyewe anathibitisha kuwa,mimi sikuwa hivyo  na kuonesha vyeo vyake alivyokuw navyo(....) lakini kwa neema nikawa jinsi nilivyo kwa maana  niliyofikiria ni faida, yakawa yote ni hasara kwa ajili ya Kristo (Fil 3,5….) Kwa maana hiyyo, Padre Canatalamessa anabainisha kuwa tendo la kukutana na moto na Yesu uliweza kuunda upya maisha ya mtume  kwenda mbele binafsi hata baada ya Kristo.

Kwa upande wetu amebainisha kuwa tendo la utungu wa mimba daima ni mgumu kuutambua;kila kitu ni kama maji yanayoyeyuka  wakati kupitia kile kiitwacho liturujia za mpito yaani : Ubatizo, Kipaimara, ndoa daraja la wakfu au wito maalumu wa kitawa. Je tufanyeje uzoefu kama huo kama alioufanya Mtakatifu Paulo na wangine baada ya kukutana na Kristo? Sakramenti zinaweza kuwapo lakini zisizae matunda, na kwa namna hiyo, jambo muhimu ni kukutana ya Kristo binafsi,ndiyo tukio muhimu na nafasi kubwa katika maisha yetu.

Katika mahubiri ya mmoja asiyejulikana jina  kipinchi karne ya V mwaka 387 , ni Askofu alithibitisha kuwa, kwa kila binadamu msingi wake wa maisha ni ule wa kuanzia na Kristo ambaye alitolewa sadaka kwa ajili yake. Lakini kwa yule Kristo aliyechinjwa sadaka wakati ule, pia anapotambua neema na maisha yatokanayo na huyo aliyotoa maisha kwa ajili yake.Kwa njia hiyo Padre Cantalamessa amesema, tunapokaribia siku ya Kuzaliwa kwa Bwana ni vema kukukaribia na maneno hayo ya Kristo katika saa kifo; na  kwamba kila binadamu, mwanzo wa maisha yakea ni ule wa kuanzia na Kristo aliyezaliwa kwa ajili yake. Hata hivyo ni mawazo ambayo twaweza kusema ni ya historia ya tasaufi nzima ya Kikristo kuanzia Origene, kupitia Mtakatifu Agostino, Mtakatifu Bernardo, Luteri na wengine wengi. Je ina maana gani kwangu kusema Kristo alizaliwa mara moja na Maria huko Betlehemu, iwapo hazaliwa kwanza katika roho yangu? Hivyo kila sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana na hata ya mwaka huu inaweza kuwa Noeli ya kweli katika maisha yetu.

Ina maana gani  kufanikiwa hasa unapounganika na imani na Yesu mfufuka na hai? Jambo la kwanza unafunguka mbele ya maskini na majanga ya watu; unafunguliwa wazi mbele ya dunia ya Mungu, kwasababu Kristo ni mlango, ni njia ambayo inakuunganisha katika Utatu usiogawanyika na ambao hauna mwisho.

Tafakari ya “Kristo na wakati” ambayo imejikita ndani yake, inaweza kufanya kazi muhimu ya kuponyesha ndani kwa ajili yetu: kupoyesha kilio tasa cha vijana wenye wengi kuhusu  mawazo yaliyotanda mizizi ambayo yanapelekea kuona uzee ni kushindwa na magonjwa siyo baraka.  Mbele ya Mungu kufanikiwa katika maisha si laaima yawe yamejaa tele au maisha yenye  uwezo wa kufanya kazi na ubunifu, lakini hata ule uliojazwa  na Kristo kwasababu ndani yake upo tayari ujazo wa milele.

Mwaka unao anza 2018 utakuwa na maana kubwa na hasa Kanisa kuwafikiria kwa karibu Vijana kwa njia ya Sinodi ya Maaskofu, yenye kauli mbiuVijana imani na Mang’amuzi, aidha katika maandalizi ya Siku ya Vijana duniani. Ka njia hiyo Padre Cantalamessa amehimiza kuwasaidia vijana waweze kupenda Yesu Kristo na kwa kufanya hivyo tutakuwa tumefanya zawao kwao iliyo kubwa na nzuri zaidi.

Kwa kumalizia tafakari lake amependelea kuwakumbusha maneno yanazingiaia juu ya kuingia wakati ulio timia wa umilele ambao unsikika katika maneno ya  Usiku wa Neoli, kwa namna rahisi na yeye shangwe kuu, kwamba katika mwaka wa 42 wa utawala wa Kaisari Ottaviano Augusto, wakati dunia nzima ilikuwa ikitawala amani, Yesu Kristo,Mungu Milele na Mwana wa Baba milele alizaliwa huko Betlehemu ya Yuda naBikira Maria na  akawa mwanadmu.

Aidha amesema Padre Raniero,karibia sikukuu ya Noeli ya mwaka 1308 alikufa Mtakatifu Angela wa Foligno. Akiwa katika kitanda cha mauti, wana wake kiroho waliokuwa wamemzunguka wakasikia akitamka : Neno la Mungu akafanyika mwili! Na baada ya kimya kidogo kama vile roho yake inajirudi, akaongeza “kila kiumbe ni mdogo; akili za malaika hazitoshi! Kwa kitu gani, wakamuuliza, kila kiumbe ni mdogo kwa jinsi ganimna kuhusu akili ya malaika kutotosha? Akajibu “ “vigumu kueleza” Padre Cantalamessa anaongeza, ilikuwa kama fumbo,hivyo amethibitisha kuwa , alikuwa anasababu ya kusema hivyo kwasababu hili ni fumbo kubwa sana ambalo si rahisi kulitambua kama siyo kwa njia ya kuabudu.
Bikira Maria tunayemwomba katika antifona za siku hizi, aweze kutupatia neema ya kupokea kwa furaha, shukrani na mshangao  wa Neno wa Mungu anayekuja kuishi kati yetu. Amewatakia matashi mema ya Noeli kuanzia kwa Baba Mtakatifu Francisko, na washiriki wote wa mafungo ya Noeli katika Nyumba Kuu ya Papa.
Sr Angela Rwezaula
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.