2017-12-21 16:50:00

Papa:Kazi ni njia ya utakatifu,bila kazi hakuna hadhi ya maisha!


Baba Mtakatifu mara baada ya kukutana na Sekretarieti Kuu ya Vatican Kwa matashi ya Noeli, katika Ukumbi wa Mkutano wa Clementina, amekutana pia na wafanyakazi wote wa Vatican na familia zao katika ukumbi wa Mwenye heri Paulo VI . Katika hotuba yake bila kuandika amewashukuru kila mmoja wao, kwa kazi ambayo inaunda kukundi kimoja na kila mmoja kwa ajili ya mema ya Vatican, kwa ajili ya kuwasadia watu wengi, ambao ni kama mnyororo unao peleka mbele Kanisa. Hata hivyo katika hotuba yake hiyo , amesema anataka kuwaeleza  juu ya kazi, hasa kuwashukuru kwa kazi zote wanzozitenda japokuwa ameonesha wasiwasi mkubwa kwamba , hata Vatican kuna matatizo ya kazi Na amebainisha jinsi alivyokuwa amesha sema hawali juu ya tatizo la kazi na kwamba nataka kurudia kusema kuwa , hataki kusikia  neno la kazi za suluba ndani ya Vatican! 

Aidha amesema hakuna haja ya kuacha mtu bila kazi, labda kama kuna mikataba tofauti. Na kwa upande wake ni matatizo ya adhimu, kwani tunaweza kusema kwamba yoe hayo yapo hata katika mafundisho Jamii ya Kanisa na kuwa na nyumba ya matatizo hayo. Lakini katika kutatua matatizo hayo inatakiwa juhudi na msaada wa wote. ”Kazi ni njia yenu ya utakatifu anasema, ni furaha na kuendelea mbele katika maisha yanayotakiwa na kwamba kazi inatoa  hadhi na usalama wa kazi unatupatia hadhi.

Baba Mtakatifu pia akiendelea na suala hili la kazi , bila kutaja jina, amesema hata nchini Italia kuna makampuni muhimu ambayo yako hatarini na ambayo yanataka kuthibitii,kwa maana ya kuachisha watu kazi, lakini kuwaachisha kazi watu elfu tatu au nne ni jambo baya sana! kwasababu ni kutolea hadhi na hivyo amethibitisha  kuwa suala hilo linatazama Vatican, Italia na dunia nzima kwa ujumla.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News

 








All the contents on this site are copyrighted ©.