2017-12-21 16:26:00

Papa anawaalika wakuu wa Mabaraza ya Kipapa Vatican kuwa kama Eria!


Ni kwa mara nyingi tena inapatikana fursa ya kuweza kubadilisha matashi mema ya sikukuu za Kuzaliwa kwa Bwana kwa wote wahudumu na wawakilishi kutoka Mabaraza yote ya Kipapa ambao wanafanya kazi katika sekratarieti kuu Vatican. Ni maneno aliyo anza nayo Baba Mtakatifu Francisko  kwa Sekretarieti kuu ya Vatican kwa ajili ya matashi mema ya sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana, 21 Desemba 2017. Baba Mtakatifu anmesema kwamba, Noeli hiyo iweze kufungua macho na kuacha mambo yasiyo na maana ya udanyifu, ubaya na unafiki ili kutambua yale yaliyo muhimu, ya kweli, mema na ya dhati. Noeli ni sikukuu ya imani ya Mwana wa Mungu aliyejifanya binadamu kwa ajili ya kutupatia hadhi yetu ya kuwa wana, kutokana  na kupotee katika dhambi na ukosefu wa itii. Noeli ni sikukuu ya imani katika mioyo iliyobadilishwa katika holi, ili kumpokea yeye katika mioyo ambayo katika Mungu inaweza kuchanua katoka kisiki cha umaskini na kutoa chupukizi cha matumaini , upendo na imani. 

Baada ya tafakari juu ya Noeli ameendelea na hotuba yake ikiwa ni kwa mara ya tano ya Sekretarieti ya Vatican  tangu alipochaguliwa kwa ajili ya matashi mema ya sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana, ambato ameweza kusisitiza  juu ya hatari ya kusaliti imani au  kujinufaisha katika umama wa Kanisa.
Kwa kufafanua hilo  amesema, ni kutokana na watu ambao wanachanguliwa kwa uangalifu na makini ili kuweza kutoa nguvu zaidi katika mwili mmoja wa Kanisa na katika mageuzi, lakini kumbe watambui ukubwa huo na uwajibika wao, mahali ambapo wanajichia na  kupotoshwa na tamaa au ubatili. Lakini inapotokea hao watu kuwawekwa mbali ,wanajidanganya wenyewe kwamba hawana hatia (mashahidi) na kwa njia hiyo wanafikiri kwamba ni  mfumo wa mageuzi ya Papa badala ya kujisemea kuwa ni  makosa binafsi (mea culpa)!

Karibu na watu kama hao, Baba Mtakatifu katika hotuba yake kwa  Sekretarieti kuu amesema, bado kuna wengine ambao wanafanya kazi katika Sekretarieti kwa njia sahihi kwa matumaini na kwamba wanakuwa na uvumilivu wa Kanisa katika nafasi iliyopo ya kuongoka, si kwa ajili ya kutafuta faida yake. Pamoja hayo Baba Mtakatifu kwa hakika hakusahahu sehemu kubwa ya watu waaminifu ambao wanafanya kazi kwa sifa na jitihada kubwa, kwa imani, ujuzi, kujikita zaidi na kwa utakatifu mkubwa.

Na kwa njia hiyo Baba Mtakatifu Francisko  anawataka wawe na moyo huo katika mabaraza yote ya Kipapa ambapo amesema wanapaswa kufanya kazi kulingana na asili yao na madhumunii yao kwa jina na kwa mamlaka ya Mkuu wao na daima kwa ajili ya mema ya huduma ya Makanisa yote. Wao wanaalikwa kuwa ndani ya Kanisa kama eria aminifu na nyeti ambazo zinasaidia kama watangazaji na wapokeaji.

Akifafanua juu ya eris ambazo ni nyeti zenye uwezo wa kupeleka matangazo na kupokea matangazo pia kwa uaminifu amesema; Neno uaminifu hasa kwa upande wao wakiwa wanafanya kazi Vatican, linachuka tabia maalumu, hasa wanapokuwa wanatoa huduma kwa Kharifa wa Mtume Petro, ambapo ndiyo sehemu kubwa na maisha yao katika huduma ya kila siku. Kwa maana hiyo anaongeza kusema kuwa, hiyo ni semehemu muhimu ya uwajibikaji, wakati huo huo ni zawadi ambayo kadiri ziku zinavyozidi kwenda mbele inajenga uhusiano wa kina na Papa .

Na kwa upande wa neno la eria, ameifananisha pia na mwendo wa mawimbi ya mtangazaji na msikilizaji  na kwa njia hiyo anasemam inajihusisha na kupokea habari kutoka mbali kama vile  maombi,maswali,vilio,furaha,machozi ya Makanisa, hasa makanisa duniani, kwa njia yao ili kuweza kumfikia Askofu wa Roma,ambaye ni Papa,hatimaye, kumwezesha yeye kuendelea vizuri na shughuli zake za kitume na utekelezaji wake  ambao ni msingi daima na unaonekana wazi  wa umoja, imani na muungano.

Kutokana na kupashana habari hizo, kwa upande wa Baba Mtakatifu amethibitisha kuwa ni muhimu kwa mantiki ya kuwasilishwa kutoka kwa Mabaraza ya Kipapa yote na kwa ukarimu katika mchakato wa kusikiliza na kushirikishana. 

Mara baada ya Hotuba yake, amesema maneno bila kusema kuwa kama zawadi ya Kuzaliwa kwa Bwana anamependelea kuwachia kitabu kimoja cha Mwenye heri Padre Maria Eugenio wa Mtoto Yesu: “Ninataka kumwona Mungu”. Ni kazi ya kitaalimungu ambayo itawasadia wote.  Hata hivyo amesema labda hawatasoma kitabu chote, lakini kwa namna moja au nyingine wajaribu kutafuta maana yake. Hata hivyo amewasifu Kardinali Mauro Piacenza na Mosinyo Nykiel waliotunga kitabu hicho “Sikukuu ya huruma kama matokeo ya Jubilei ya Huruma”.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News

 








All the contents on this site are copyrighted ©.