2017-12-21 16:18:00

Papa anatoa mwaliko wa kuwa na furaha kwakuwa tumekombolewa!


Baba Mtakatifu ametoa mwaliko wa nguvu wa kuwa na furaha na kwamba tabia ya kukata tamaa ya maisha, siyo ya kikristo. Amesema hayo katika mahubiri yake, kwenye misa yake ya asubuhi ya tarehe 21 Desemba 2017 katika Kikanisa cha Mtakatifu Marta mjini Vatican. Baba Mtakatifu anasema ni muhimu kuwa na uso watu waliokombolewa, waliosamehema na siyo kuwa na sura ya waliyofiwa. Baba Mtakatifu anzunguka juu ya furaha itokanayo na msamaha wa dhambi na ukaribu wa Bwana, akiangazwa Somo la Injili ya Makatifu Luka 1,39-45 ambayo inaelezea juu ya furaha ya kina tokayo ndani ya moyo na si itokanayo na sikuuu. Katika liturujia ya leo,ujumbe ni ule wa furaha  ambao unaalikwa kufurahi katika Bwana. 

Baba Mtakatifu ameelezea mantiki tatu za furaha : kwanza ni furaha itokanayo na kusamehewa dhambi; Bwana amekusamehe dhambi zako, kwa njia hiyo anawaalika kufurahi na si kufanya maisha ya vuguvugu, kwa maana ya kuwa na utambuzi wa kusamehewa: Ndiyo mzizi hasa wa furaha ya kikristo,Nana Mtakatifu ametoa mfano kwamba, inatosha kufikiria furaha ya mfungwa anayetoka gerezani mara anapomaliza hukumu ya makosa yake au wagojwa, au viwete ambao waliponywa katika Injili. Ni lazima kuwa na utambuzi huo wa ukombozi ambao uliletwa na Yesu. Baba Mtakatifu anathibitisha.

Mfalsafa mmoja alikuwa akichambua wakristo , kwa maana alikuwa akikiri kuwa yeye aamini Mungu. Alikuwa akisema: wakristo wanasema kuwa wanaye mwokozi , mimi siwezi kuamini, ila nitaamini mwokozi iwapo sura zao zitaonesha kama zilizokombolewa, yaani furaha ya kukombolewa. Baba Mtakatifu anaongeza; Je wewe kama una sura ya aliayefiwa , ni jinsi gani unaweza kuaminika kwamba wewe umekombolewa, na kwamba dhambi zako zimesamehewa? Huo ndiyo ujumbe wa kwanza katika liturujia ya leo kwamba wewe umesamehewa , na kila mmoja wetu amesamehewa dhambi. Ni Mungu wa msamaha anasema Baba Mtakatifu, kupokea msamaha huo na kuendelea mbele kwa furaha kwasababu Bwana atasamehe hata mambo ambayo tunafanya kwa udhaifu.

Mwaliko wa pili ni ule wa kuwa na furaha kwasababu, Bwana anatembea nasi tangu wakati ule wa Ibrahimu, yeye yuko kati yetu, katika matatizo, furaha na kila kitu. Na hivyo kila siku ni vema kumwelekea neno Bwana maana yupo nasi katika maisha yetu.  Na mantiki ya tatu ambayo Baba Mtakatifu amesisitiza ni ile ya kutojiachia kuwangukia katika matukio: kwa maana yakukata tamaa ya maisha si tabia  ya kikristo. Hiyo inatoka kwenye mzizi ambao hutambui kama umesamehewa , inatoka kwenye mizizi ambao hujawahi kubembelezwa na Bwana. Katika Injili, tunaweza kuona furaha hiyo: Maria kwa furaha kubwa aliamka na kwenda kwa haraka. Kwa njia hiyo  hata furaha inafanya uwe na haraka daima, kwasababu ni neema ya Roho Mtakatifu ambaye hajuhi kwenda poleple, Roho Mtakatifu mara nyingi anakwenda haraka, daima inatusukuma kwenda mbele: mbele kama upepo uvumao na kupeleka mashua  na mitumbwi.

Kusimama haraka  na kufurahi, kwa ufupi ni furaha ambayo ilifanya kitoto kichanga tumboni mwa Elizabeth kusikika tumbozi mwake alipokutana na Maria: ndiyo maana ya furaha ambayo Kanisa linasema, ni lazima kuwa wakristo wa furaha na kufanya kila juhudi zote ili kufanya wengine waamini kwamba tumekombolewa. Ni watu ambao Bwana wamewasamehe kila kitu hata kama tunaweza kuteleza, lakini Mungu anatusamehe daima, kwa maana Bwana yupo kati yetu na hatatuacha kamwe tuanguke. Na mwisho ndiyo ujumbe ambao Yesu anasema simama kwa wagonjwa, simama  na imba kwa furaha; furahi na kutangaza kwa moyo wako wote.

Sr Angela Rwezaula

Vatican News

 








All the contents on this site are copyrighted ©.