2017-12-20 16:08:00

Televisheni:Makubaliano kati ya Sekretarieti ya Mawasiliano Vatican na RAI


“Kwa kutia sahini  upya  protokali hizo katika tukio muhimu  la ushirikiano kati ya  Rai na Sekretarieti ya Mawasiliano Vatican ni ishara ya kina katika kuimarisha ushirikiano na  urafiki”. Amethibitisha maneno hayo Bwana Mario Orfeo, Mkurugenzi Mkuu wa Rai ( Kituo cha Televisheni na  matangazo nchini Italia akifafanua  juu ya Protokali za Makubaliano yaliyotiwa sahini  katika Makao Makuu ya Sekretarieti ya Mawasiliano Vatican na Rai tarehe 19 Desemba 2017 na Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Mawasiliano Vatican Monsinyo Dario Vigano.

Bwana Orfeo amesema, makubaliano hayo yanaongeza ushirikiano chini ya mwongozo wa uhariri, wa sasisho la teknolojia na  ubora wa kuelezea katika utume  kamili wa kuhabarisha katika huduma ya umma. Aidha amesisitaza kuwa, mageuzi ya vyombo vya habari  na utekelezwaji wake kwa upande wa  Sekretarieti ya Mawasiliano  Vatican unawakilisha  nguzo muhimu katika kuunga mkono mchakato huo wa pamoja. 

Zaidi ya hayo Misa ya Mkesha wa  Usiku wa Kuzaliwa kwa Bwana, itakayoongozwa na Baba Mtakatifu Francisko katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, tarehe 24 Desemba 2017, itaoneshwa mbashala,  hata kwa njia ya Satelite katika muundo wa ubunifu uitwao ( Ultra HD 4K), kwenye kituo cha Rai 4K, kwa ushirikiano na Sekretarieti ya Mawasialino na RAI. Kwa maelezo mengine amesema kuwa, ina maana ya utoaji wa sauti kwa ngazi ya maalumu na ya juu.

Halikadhalika habari nyingiza zinasema kuwa  kwa kifupi watatangaza rasmi mipango mipya iliyoko katika michakato lakini pamoja hayo ni  ile ambayo itakarekebishwa kwa upya  na hasa ya kudhibiti na kulinda Documantary  juu ya Vikosi vya Ulinzi wa Vatican  iliyotayarishwa  kwa kushirikiano na ofisi ya Mawasiliano, ambapo tarehe 29 Desemba 2017 utaoneshwa na Kituo cha Televisheni cha RAI I .

Tendo hilo linawakilisha hatua mpya ya mchakato uliohitimishwa mwaka 2016 na “Usiku kwa Mtakatifu Petro, (Notte a San Pietro) na mwendesha kipindi Alberto Angela.Kipindi kilichopendwa sana na watazamaji wengi wa RAI:

Sr Angela Rwezaula
Vatican News.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.