2017-12-20 16:26:00

Tarehe 22 Desemba Kard. Parolin ataadhimisha misa ya Noeli kituo cha CeIS


Tarehe 22 Desemba 2017 saa kumi na mbili Jioni Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican, ataadhimisha Misa ya Kuzaliwa kwa Bwana katika Kituo cha Kiitalia cha Mshikamano kiitwacho Padre Mario Picchi wa Roma. Katika maadhimisho yatakayofanyikwa katika kituo hicho Mjini Roma, wataudhuria  pia  watoto na vijana  wa Jumuiya zote za kutoa tiba , aidha wanawake na watoto, wakimbizi wa kisiasa  wa kituo cha pamoja na familia zao, wahudumu katika sehemu mbalimbali za kutoa huduma ya upendo.

Naye Mwenyekiti wa Chama hicho CeIS, Bwana Roberto Mineo katika kuelezea maandalizi haya amesema , ni furaha kubwa kwa vijana hao na wengine wengi,  kwa mara nyingine tena ,mhudumu wa Papa Francisko kupendelea  kusheherekea mwaka wa tatu mfululizo sikukuu ya kuzaliwa kwa Bwana pamoja na watu wengi wanaopambana kila siku ili kuondokana na matatizo ya janga la madawa ya kulevya. Hasa katika kipindi hiki kigumu Roma, mahali ambapo ripoti zinatoa vitisho vingi vya matumizi ya madawa ya kulevya na ambapo ni muhimu kuongeza nguvu ili kuweza kuzuia kila aina ya dawa kwa upande wa sera za kisiasa na  kuzuia majanga haya yasiendelee kwa vijana ha ona pia kwa hali nyingine ya kucheza kamali. 

Kwa miaka hamsini ya Kanisa,  Kituo hicho kimeeweza kutembelewa na Mababa watakatifu tofauti, kuanzia na Mwenye heri Paulo VI, Mtakatifu Yohane Paulo II na Baba Mtakatifu Francisko. Kituo hiki kilianzishwa na Padre Mario Picchi mwishoni mwa mwaka wa 60 na hivyo kituo hicho kimeendelea na ufanisi mkubwa kadiri ya miaka inavyokwenda, kwa kufungua vituo mbalimbali katika Wilaya ya Roma na wilaya nyingine. Vituo hivyo ni majengo ya tiba kwa ajili waathirika wa  madawa ya kulevya hasa  vijana, pia magonjwa ya akili kutokana na madawa hayo. Aidha vituo vingine ni vya  kuwasaidia wagonjwa wa ukimwi,vituo vya wazee,  na vituo vingine kwa ajili ya wale wasio kuwa na mahali pa kiushi, wahamiaji, wakimbizi na wale wanaoomba makazi kisiasa, ikiwa pamoja na wanawake na waathirika wa kijinsia.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News

 








All the contents on this site are copyrighted ©.