2017-12-19 15:00:00

Papa Francisko na Mfalme Abdullah wajadili kuhusu hatma ya Wakristo!


Baba Mtakatifu Francisko, Jumanne, tarehe 19 Desemba 2017 amekutana na kuzungumza na Mfalme Abdullah II wa Yordan, ambaye pia alibahatika kukutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameambatana na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican.

Katika mazungumzo kati ya Baba Mtakatifu Francisko na Mfalme Abdullah II, wamejikita zaidi katika mchakato wa maendeleo endelevu ya binadamu, amani na utulivu huko Mashariki ya Kati mintarafu umuhimu wa Yerusalemu pamoja na utunzaji bora wa Maeneo Matakatifu ya Hashemita. Katika mazingira kama haya, viongozi hawa wamekazia umuhimu wa pande zinazohusika kuendeleza mchakato wa majadiliano sanjari na kudumisha majadiliano ya kidini katika ukanda huu! Mwishoni, wamejadili umuhimu wa Wakristo kuendelea kubaki huko Mashariki ya Kati na kwamba, hata wao ni sehemu ya wananchi wa eneo hili!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S

Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.