2017-12-16 08:53:00

Tafakari ya kwanza ya Majilio Vatican:Kristo awe kitovu cha historia ya maisha!


Tafakari ya Majilio ya mwaka huu inapendekeza kuweka Mungu mtu ambaye ni Kristo katika kitovu, katika mambo makuu ambayo yanaunda ukweli, yaani kuumbwa kwa ulimwengu,kipindi cha kihistoria, nyakati,uumbaji na binadamu. Lazima kujikita kwa kina zaidi kwasababu, sehemu kubwa ya kuongea na kufafanua juu ya  Kristo ki ukweli imeacha pembeni katika utamaduni wetu. Yesu hayupo kabisa katika maisha ya watu maana ni rahisi kutambua katokana na misingi mitatu ya mazungumzo yanayojikita katika ulimwengu wa sasa yaani wa sayansi, falsafa na dini.

“Yote yalifanyika kwa njia yake na Kristo ni muumba” ndiyo kauli mbiu inayoongoza tafakari za kipindi cha Majilio kwa Mwaka 2017.Tafakari inayotolewa na Padre Raniero Cantalamessa, Mhubiri mkuu wa nyumba ya Kipapa, kwa uwepo na ushiriki wa Baba Mtakatifu Francisko kila Ijumaa, yaani kuanzia tarehe 15 Desemba, na  20 Desemba, 2017 tu kwa maana amesema kwamba kwaka huu tafakari ni fupi kutokana na utaratibu wa kalenda. Tafakari hizi zinatolewa kwenye Kikanisa cha “Mama wa mkombozi” “Redemptoris Mater” kilichoko mjini Vatican.

Akiendelea na tafakari ya kwanza amesema, lengo la kuelezea siku ya mwisho  wa dunia si kuafuatia utaratibu  kinadharia, bali katika matendo. Na hiyo ni kutaka kwanza kumweka Yesu awe kitovu cha maisha yetu binafsi na upeo wa dunia, katika kitovu cha fadhili kuu tatu za kitaalimungu  yaani , imani, matumaini na mapendo. Noeli ni kipindi mwafaka cha kufanya takafakri hizo kwa kina. Ni kipindi ambacho kinakumbusha "Neno wa Mungu kutwaa mwili" na kujikita kwa dhati katika kazi ya uumbaji, katika historia, nyakati  na kwa kipindi.

 Ametenga vingele tofauti  katika Tafakari yake  kuhusu mwanzo wa nchi  kuwa ,tafakari ya kwanza ni kujikita katika mpango wa upashanaji wa habari, hasa juu ya uhusiano kati ya Kristo na ulimwengu. "Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.

Akimtumia mwandishi wa kizamani Abate wa Kingereza Alexander Neckam ( 1157- 1217), anasema akitafakri sehemu ya kwanza ya Biblia:nchi ilikuwa utupu kwasababu Neno lilikuwa bado kufanyika mwili. Na ardhi yetu ulikuwa tupu kwasababu hakuna aliyekuwa ameijaza kwa neema na ukweli. Ilikuwa utupu kwasababu hakuna aliyekuwa amesimama na kuishi na muungano wa kimungu . Makao yetu yalikuwa wazi kwasababu kulikuwa bado  hakuna  ujazo wa wakati. Na giza nene lilifunika kwasababu mwanga wa kweli ulikuwa bado haujaangazia kila mtu anayekuja katika ulimwengu huu.

Padre Cantalamessa anaongeza kusema kuwa, si rahisi kuelezea vya kutosha Injili kuhusu uhusiano ambao upo kati ya kazi ya uumbaji na neno kufanyika mwili ambayo inapatikana katika maandishi ya kwanza ya Kitabu cha Mwanzo na katika mwanzo wa Injili ya Mtakatifu Yohane .Anakumbusha kuwa hata Waraka wa Baba Mtakatifu wa Laudato Si“ unaelezea sehemu hiyo katika ( kipenge cha 99). Lakini ni  muhimu kuwa na utambuzi wa Yesu anachukua nafasi gani ndani maisha ya binadamu mbele ya ulimwengu mzima. Na kazi hiyo leo hii anabainisha kuwa ni ya dharura zaidi. Kama asemavyo mwandishi   Maurice Blondel kwa rafiki yake kwamba, kuna mabadiliko mengi yatokanayo na upeo wa sayansi ya asili na binadamu ambayo ni changomoto kubwa kwa ukristo katika kutazama vizingiti vingi vitokanavyo na matukio ya ulimwengu  wa sasa.

Maandiko ya Biblia ambayo ndiyo kiini cha imani yetu na nafasi ya ulimwangu wa Kristo yanapatikana katika maandiko ya Mtakatifu Paulo na Yohane yaliyotajwa katika Waraka wa Laudato Sii utajwao katika kitabu cha Wakolosai (1,15-17,)  kwamba  yeye ni mfano na sura ya Mungu, asiyeonekana, ni mzawa wa kwanza ... Na katika Injili ya Yohane (1,3 na 10)  anasema, kwa njia yake vitu vyote vimeumbwa naye ….

Padre Cantalamessa ameongeza kusema kuwa pamoja na kwamba maandiko hayo huonekana kufanana, lakini upo uwezekano wa kutenganisha kati yao na kuona utofauti wenye umuhimu wa maendeleo endelevu ya Kitaalimungu. Anafafanua zaidi kuhsu hili kwamba, kwa mujibu wa Mtakatifu Yohane, muungano wa kazi ya uumbaji ni pale ambapo Neno linafanyika mwili na kukaa kwetu.  Kwa upande wa Mtakatifu Paulo, kitovu ni katika Msalaba, kwa maana hiyo sehemu ya kwanza ni neno kufanyika mwili na sehemu ya pili ni fumbo la Pasaka.

Aidha amefafanua mitazamo tofauti ya ulimwengu kutoka kwa waandishi mbalimbali kwa mfano  Teilhard de Chardin, akichambua uhusiano na mtazamo wa ulimwengu, mawazo yake yanajikita katika haki ya mwisho wa historia ya dunia itakavyokuwa. Na katika biblia, inaonesha machafuko ya historia kwa upeo wa hukumu; kwa mfano uchambuzi wa magugu kati ya ngano. (Mt 13, 24). Na kwa upande wa Barua ya Mtakatifu Petro inasema, wakristo wanasubiri siku ya kuja kwa Mungu katika matukio ya kuwasha moto (2 Pt 3, 12). Na upeo huo ndiyo umekuwa kama mhuri wa Kanisa ambao unatazama maneno ya mwanzo, hasa kuonesha siku ile ya hasira, na dunia itakavyokuwa majivu. Yote hayo kwa mtazamo wa sasa unaweza kuona kwamba mwisho wa dunia ki ukweli ni wake ni mbaya.

Lakini pamoja na hayo yote, kuna kipengele cha kutazama dunia kwa upeo wa Roho ya Kristo katika ulimwengu: Padre Cantalamessa anaeleza kwamba, kosefu wa majibu yaliyo wazi kwa upande wa wataalamu wa taalimungu kuhusu masuala msingi kama hayo unategemea na ukosefu wa kuwa umakini kwa upande wa Roho Mtakatifu na uhusino wake na Kristo mfufuka. Mtakatifu Paulo anasema, Adamu wa mwisho alikuwa  Roho mtoa uzima (1 Cor 15, 45); Aidha anaongeza kusema, Bwana ni Roho  (2 Kor 3, 17). Hiyo ni kutaka kusisitiza kwamba, Bwana mfufuka anatenda tayari katika ulimwengu kwa kutumia mikono yake ambayo ni Roho Mtakatifu.

Mtume Paulo anathibitisha hayo kwamba:Kwa maana tunajua kwamba mpaka hivi sasa, viumbe vyote vinalia kwa maumivu kama ya kujifungua mtoto.Wala si hivyo viumbe peke yake,bali hata sisi tulio na huyo Roho, aliye wa kwanza wa zawadi za Mungu; sisi pia tunalalamika ndani yetu, tukingojea tufanywe watoto wa Mungu, nazo nafsi zenu zikombolewe. (WaromaR 8, 22-23).
Ni kuonesha kuwa, Roho Mtakatifu ni nguvu ya maajabu ambayo inatoa msukumo kufikia ukamilifu wake. Na ndiyo maana hata Mtaguso wa II wa Vatican unathibitisha hasa, katika matendo yote kwa ngazi zote za kijamiii zinazounganishwa na ulimwengu. Kila kitu cha maendeleo ya utunzaji wa mazingira ni kazi ya Roho Mtakatifu. Na Yeye ndiye wa kwanza katika uumbaji wa kila kitu .

Akifafanua katika kipengele kingine anasema; Je Yesu anajikitaje katika  kazi ya uumbaji? Padre Cantalemessa anafafanua, hapo ndipo kuna kazi kwani Kristo anatenda kazi yake katika uumbaji kwa upande wa kijamii kutokana na  amri yake ya upendo kwa jirani. Katika uhusiano wa nafasi na maana ya jirani ndiyo kuonesha ukaribu, katika uhusiano kwa wakati, ikiwa na maana ya ukaribu wa wale watakao kuja baada ya sisi, wakati huo huo ni kuanzia na watoto,vijana ambao wapo hatarini kutokana na uwezekano wa kuishi katika sayari bila ya kuwa na thamani. Au kuwa na hatari ya kutembea njiani wamejifunika kitambaa usoni ili wapate kupumua, au kuanzisha ukoloni katika sayari nyingine. Kwa njia hiyo ukaribu, katika nafasi na katika muda Yesu alisema Yote mlio fanya kwa mdogo mmefanya kwa ajili yangu. ” (Mt 25, 40.45).

Kama ilivyo katika mambo yote, hata utunzaji wa kazi ya muumbaji iko katika ngazi hiyo; kazi ya ulimwengu na katika sehemu mahalia. Padre Canatalamessa ametumia msema wa kisasa kuwa (Think globally, act locally) fikiria kiulimwengu lakini utendaji wake uwe mahalia. Anathibitisha kuwa hii ina maana ya uongofu ambao unapaswa kuanzia binafsi, hasa kwa kila mmoja wetu. Ametoa mfano kuwa Mtakatifu Francisko wa Asizi alikuwa mara nyingi anawaeleza ndugu zake wadogo kuwa, “sijawahi kuwa mwizi wa sadaka, hata kuomba au kutumia bila kuwa na mahitaji.Nachukua kile kidogo ninachokihitaji ili hata maskini wengine ambao hawana waweze kushiriki, kwasababu kufanya kinyume, ni kama kuiba”.

Anashauri kuwa, leo hii kanuni hiyo inaweza kufanyiwa kazi. Ni muhimu katika ardhi hii,na hata sisi sote tunapaswa kupendekeza ikawa kanunu yetu ya maisha kwamba, sisi siyo wezi wa rasilimali, tunatumia kile tunachokihitaji,  tukikumbuka kuhifadhi kwa wale watakao kuja baada ya sisi.
Na kwa kuanzia hapo, ametoa mfano kwamba, sisi tunaofanya kazi kwa kutumia karatasi, tunaweza kutumia karatasi chache kufikiria ardhi ambayo ni mama yetu, ili miti ikatwe kidogo. Na Noeli  ni wito wa nguvu katika kukumbusha hilo hasa kwa matumizi ya vitu, na mfano wake unaanzia kwake yeye Muumba, aliye muumba binadamu, lakini alifurahia kuzaliwa katika holi la ng'ombe.

Na kwa njia hiyo Padre Cantalamessa amemalizia akiwaomba wakumbuke daima wimbo wa Mtakatifu Alphonce Marie Dei Liguori: “A Wewe uliye duniani na muumba,mkate na moto vinakosa“. Waamini wote na wasio waamini tunaalikwa sote kujikita katika wazo la dhati na kuheshimu kazi ya uumbaji, lakini zaidi sisi wakristo tunapaswa kuwa na sababu, na nia tofuati.Iwapo Baba wa Mbingu alifanya yote kwa njia ya Kristo, pamoja na Kristo, hata sisi lazima kutafuta kila njia kufanya kila kitu kama hivyo: kwa njia ya Kristo, pamoja na Kristo, yaani kwa neema yake na kwa utukufu wake, hata kile tunachotenda leo hii.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.