2017-12-13 15:06:00

Ujumbe wa Papa kwa Maadhimisho ya miaka 25 ya chama cha Populorum Progressio!


Kuna miradi 4400 iliyofanyika katika nchi za  bara la Amerika ya Kusini na Caribbean ili  kuboresha hali ya watu wa kiasili, mchanganyiko na waafro, kutokana na  msaada wa Chama cha Populorum progressio. Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko aliyosisitiza katika  ujumbe wake  uliotuma kwa washiriki wa Mkutano ambao umefunguliwa  mjini Roma Jumatano  tarehe 12 Desemba 2017 katika tukio la Maadhimisho ya miaka 25 ya Chama hicho. MKutano huo unatarajiwa kufungwa 14 Desemba, ambapo wajumbe hao pia watakuwa na fursa ya kukutana  na Baba Mtakatifu Francisko.

Ujumbe ulioelekezwa kwa Kardinali Peter Turkson Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la huduma ya maendeleo ya watu na pia Mwenyikiti wa Taasisi ya Populorum Progressio, Baba Mtakatifu anasema: katika tukio la maadhimisho ya miaka 25 ya kuanzishwa kwa Taasisi hiyo, anapenda awafikishie  salamu kwa wanachama wote wa Bodi ya usimamizi wa chama hicho, kwa washirika wake na pia kwa wale wote ambao wamekusanyika kusherehekea tukio hilo mjini Roma.

Baba Mtakatifu Francisko ameelezea kuanzishwa kwake kuwa; tarehe 13 Novemba 1992  mtangulizi wake  Mtakatifu Yohane Paulo II alianzisha Taasisi ya Populorum Progressio ili kuchangia kuboresha hali ya watu wa asili, mchanyiko na Waafro wa Amerika ya Kusini, ambao ni kati ya makundi zaidi yaliyobaguliwa na jamii ya Amerika ya Kusini na Carribean. Na kwa maana hiyo Papa Yohane Paulo II alitamani, kuwa taasisi hiyo inonesha ukaribu wake kwa watu ambao wanakosa hata mahitaji ya lazima na ili wapate kuishi, ambao daima jamii au viongozi wa madaraka wamekuwa hawawajali katika hali zao.

Mipango iliyofanywa na kiungo hiki inataka kuwa udhihirisho wa upendo wa Mungu na uwepo karibu wa umama wa Kanisa katikati ya watu wote, hasa maskini  zaidi,(Lk 7,22). Kwa njia hiyo tangu kuanzishwa kwake, mipango 4,400 imeweza kufanyaika kutokana na mchango kuonesha ukarimu wa wakatoliki wengi na watu wenye mapenzi mema ambao walitoa kwa moyo wote sadaka zao, ili wengine waweze kuboresha hali ya maisha yao.

Ni muhimu kukumbuka kuwa, kama Kanisa mahalia la Amerika ya kusini wanashiriki na  kupanga mipango ya Baraza Usimamizi  huo ikundwa na  Kanda sita za kawaida mahali ambapo  wanajikita kupeleka mbele utafiti wa njia za kuanzisha na kuendeleza  mipango iliyowakilishwa na Maaskofu na wahusika wa kichungaji. Hali ya Amerika ya Kusini hata hivyo inahitaji uwajibikaji  kwa nguvu zaidi, Baba Mtakatifu anasisitiza,  ili hatimaye kuweza kuboresha hali ya maisha kwa wote, bila kubagua yoyote, kwa  kupambana dhidi ya ukosefu wa haki, rushwa, na ili hatimaye kuweza kupata hali bora ambayo ni matokeo ya jitihada zilizofanywa tangu hawali na sasa.

 Pamoja na kwamba, nguvu za nchi za Amerika ya kusini kuwa na watu wenye kuwa na  mshikamano na wengine, pia  ambao tayari wanao utajiri mkubwa kwa mtazamo wa kihistoria na utamaduni, kama pia rasilimali asili, lakini kwa sasa anaongeza Baba Mtakatifu kuwa,kuna kipeo kikubwa cha uchumi, na kijamii, uliosababishwa na janga la madeni ya nchi za nje, ambayo  yanazidi kugandamiza jamii,wakati huo huo kuchangia hata kiasi kikubwa cha unyonyaji, uharibifu wa mazingira ambayo ni nyumba yetu kwa ngazi ambayo mwanzo  hakuna aliyekuwa anatarajia hivyo!

Iwapo mfumo wa uchumi unaweka fedha kama kitovu na kwamba ndiyo Mungu wake, basi husababisha mivutano ya kisiasa na ubaguzi, ambapo pia hakuna tena nafasi  ya mtu, awe mke au mme. Kwa namna hiyo tendo la kuwa binadamu hugeuzwa kuwa kile kiitwacho utamaduni wa ubaguzi ambao upelekea  mateso na ukosefu wa haki nyingi za kuishi na kuwa na furaha, (taz.Barua ya Laudato SI n.44).

Taasisi iliundwa ili kuwa ishara ya uwepo wake karibu wa Papa na Kanisa kwa watu  wote, hasa kwa jumuiya zinazobaki zimebaguliwa na kuwekwa pembezoni, wasio kuwa na haki  msingi za kibinadamu ili wote wapate kushiriki katika meza moja, ambayo kwa bahati mbaya inatokea wengi wao kutoweza kushiriki kama vile jamii ya watu wa asili, mchanganyiko na waafro wa Amerika ya Kusini. Kanisa linaalikwa kuwa karibu na kugusa jirani ambaye ni mwili wa Kristo,pia ndiyo kipimo cha hukumu ya mwisho ya Kristo ( Mt 25).

Pamoja na kuwa na zana hafifu, Taasisi  hiyo inajikita zaidi katika mipango yake  hasa ya kuchangia kwa maskini zaidi, ili kuwaonesha hadhi yao (taz Laudato Si  158) kwa njia ya ushuhuda wa upendo wa Kristo anayejifanya msaada kupitia kwa ndugu na kaka ili apate kuinuliwa na kurudia kutumaini  na kuishi maisha yenye hadhi. 

Ni kwa njia hiyo Baba Mtakatifu anasisitiza, tunaweza kurudi kuwa mstari wa mbele katika maendeleo ya binadamu kamili, kumrudishia hadhi ya binadamu anayependwa na kutegemewa na Mungu, na ili apate kuchangia maendeleo ya kiuchumi na kisiasa katika nchi yenye kuwa na utajiri mwingi ambao  ni makao katika mioyo yao na katika utamaduni wao.

Mandeleo hayo yatakuwa ni juhudi ya kazi kwa  wote kwasababu ni tunda litokanalo na jitihada za pamoja ambapo kwa njia ya zana zilizotolewa kwa ukarimu na jumuiya ya Kanisa, ili kubadili anayebaguliwa kuwa rasilimali ya kweli na kwa manufaa, si ya nchi tu bali hata kwa binadamu wote. Na kwa njia hiyo Baba Mtakatifu anaongeza kusema, Taasisi ambayo inawekeza katika mipango mingi kwa ajili ya wazalendo hao, inaweza pia kupata kisima cha mawazo na ubunifu zaidi ya baadaye na kwa ajili ya uinjilishaji wa Bara hilo katika Sinodi maalum ya maaskofu wa Kanda ya Amazon, itakayofanyika mjini Roma mwezi Oktoba 2019.

Baba Mtakatifu anawashukuru sana wawakilishi wa Baraza la Maaskofu wa Italia ambao kwa ukarimu mkubwa na uaminifu wamezweza kusindikiza Taasisi hiyo , kama pia Mashirika mengine Katoliki na wafadhili wengi ambao wametoa michango yao  na sadaka zao  kwa ajili ya uendeshaji wa mipango hiyo. Mwishowe, anasawalimia washirika wa Sekretarieti ya Bogotá na ya Baraza la Kipapa kwa ajili ya huduma ya Maendeleo endelevuya kutokana na juhudi kubwa wanayofanya kwa ajili ya ndugu kaka na dada wanaohitaji.

Anawatia moyo waendelee katika shughuli hiyo ya huduma ya maendeleo ya watu na kwa ajili ya bara la Amerika ya Kusini, ili ushikishwaji kati ya wote uweze kuchangia na kuunda ulimwengu ulio bora, wenye haki na  ubinadamu,unaotazama sura ya Kristo kwa kila ndugu, katika watu wote walio baguliwa zaidi wa Amerika ya Kusini kwa kufuata pia mfano wa Mama Teresa wa Kalkuta.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.