2017-12-12 15:14:00

Mkutano kwa ajili ya maadhimisho ya Miaka 25 ya Chama cha Populorum Progressio


Katika tukio la Jubilei ya Miaka 25 tangu kuanzishwa kwa Chama cha Populorum Progressio (Maendeleo ya Watu), kwa ajili ya Amerika ya Kusini, mjini Roma, wamendaa Mkutano wenye kauli ya mbiu “Wimbo ulio mzuri kwa miaka 25 ya huduma kwa ajili ya maendeleo ya binadamu kwa  kutazama wakati endelevu”. Kuanzia tarehe 12 -14 Desemba 2017.

Tangu mwanzo wake kwa  utashi wa Mtakatifu Yohane Paulo II, tarehe 13 Februari 1992  chama hicho kilikabidhiwa chini ya Baraza la Kipapa la Cor Unum, ambacho kwa sasa chama hiki kunafanya sehemu ya utume wa kichungaji wa Baraza Jipya la Kipa kwa ajili ya Maendeleo Endelevu ya Binadamu.
Katika sehemu ya kwanza ya uzinduzi wa mkutano huo, baada ya utangulizi wa Kardinali Peter K.A Turkson, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Maendeleo endelevu na pia akiwa Mwenyekiti wa chama hicho, Kardinali Lorenzo Baldisseri, Katibu Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu, atatoa maelezo zaidi juu ya vipengele vya Sinodi  inayohusu Amazon  na watu wa kiasili inayotazamiwa kufanyika mwaka 2019;  pia kutkuwapo kipindi cha kuwasikiliza baadhi ya tafakari kwa upande wa maaskofu wa Amerika ya Kisini wanaoshiriki katika Mkutano huo.

Kati ya watoa mada wengine, pia  atakuwapo Profesa Guzmán Carriquiry ambaye atawakilisha masuala ya hali halisi ya sasa ya Amerika ya Kusini. Tarehe 13 Desemba 2017, wataendelea na mkutano wa mwaka kwa kujikita haza katika usimamizi wa fedha za chama hicho, mahali ambapo wanachama wataweza kuangalia kwa kina matumizi na hutoaji wa mhcango ya fedha kwa ajili ya kuwasaidia kusaidia jumuiya asili na  waafrro na wazalendo wa Amerika ya Kusini hata katika Visiwa vya Caribien kwa mwaka 2018.

Mkutano huo utakuwa ni fursa ya kutafakari namna ya kuboresha mtindo wa utume kwa njia ya  kufanikisha chama hicho. Siku itakayofuata ambayo ni tarehe 14 Desemba, washriki wote wa Mkutano wanatarajiwa kukutana na kuzungumza na Baba Mtakatifu Francisko ikiwa ni sehemu ya  sehemu ya maadhimisho ya Miaka 25 kuanzishwa kwa chama hiki cha “Populorum progressio” yaani “Maendeleo ya watu”, chini ya  Mtakatifu Yohane Paulo II mwaka 1992.
Kwa kipindi cha miaka 25 ni mipango mimgi iliyofanyika ya chama hiki ambayo ni zaidi ya 4,300  yenye thamani zaidi ya milioni 41 dola za kimarekani. Mipango hiyo inajihusisha katika jumuiya mahalia ambayo inatazama sekta mbali mbali, kama vile kilimo, ufugaji , ufundi, ujasiliamali , ukarabati kwa ajili ya maji safi ya kunywa , mafunzo na vifaa vya shule, afya na usafi. Kati ya wafadhili wakuu ni Chama cha Pupulorum Progressio, na zaidi washiriki wanarudia kwa upya wa Baraza la Maaskofu wa Italia.

Ikumbukwe Baraza la Kipapa la huduma ya maendeleo endelevu ya binadamu mnamo  tarehe 3 na 4 Aprili, 2017 liliadhimisha Mkutano wa Kimataifa kuhusu Miaka 50 tangu Waraka wa Kitume wa Mwenyeheri Paulo VI “Populorum progressio” yaani “Maendeleo ya watu” ulipochapishwa rasmi.  Lengo la mkutano huo ulikuwa ni kufanya upembuzi yakinifu kuhusu misingi ya kitaalimungu, kiutu na kichungaji inayofumbatwa katika Waraka huu mintarafu uhusiano wake na wale wanaotekeleza dhamana na wajibu wao katika ustawi na maendeleo ya binadamu.Kwa njia hiyo chini na mwangozo huo, chama hiki kinapata kuongozwa na  waraka huo Maendeleo ya watu katika nchi ya Amerika ya Kusini.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.