2017-12-11 16:41:00

Papa:Majilio ni kipindi cha kutafiti dhamiri binafsi ili Bwana apate njia!


Majilio di kipindi cha kutambua utupu wa mioyo yetu ili kuweza kujazwa katika maisha,pia  kusawazisha na kuondoa kiburi ili kuandaa nafasi kwa ajili ya Yesu anayekuja. Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko wakati wa tafakari ya Sala ya Malaika wa Bwana, Mama Manisa akiwa anaadhimisha Domenika ya pili ya Majilio tarehe10 Dsemba 2017.

Baba Mtakatifu anatafakari kuhusiana na liturujia ya siku akisimamia maneo ya Nabii Isaya anaye tangazia watu mwisho wa uahamisho wao na kurudi Yerusalem. Nabii anasisitiza na kutoa wito wa kuandaa njia ya Bwana hasa kwa kujiweka utupu wetu na tabia zetu za dhambi  za kutotimiza wajibu mbele ya Mungu.  

Baba Mtakatifu anasema, utupu wa maisha yetu unaweza kujitokeza kutokana na kutosali au kusali kidogo. Kwa maana hiyo Majilio ni kipindi mwafaka cha kusali kwa kina ili kuimarisha na kutunza maisha ya kiroho, kuacha nafasi muhimu ambayo inamsubiri Yesu. Utupu mwingine unaweza kutokana na ukosefu wa upendo kwa kwa jirani, hasa kwa wale wenye kuhitaji msaada na siyo tu nyenzo, bali hata kiroho. Tunaalikwa kuwa makini kwa ajili ya mahitaji ya wengine, walio karibu zaidi, kama alivyokuwa Yohana Mbatizaji. Kwa namna hiyo tunaweza kufungua njia ya matumani katika jangwa ndani ya mioyo mikavu kwa ajili ya watu wengi.

Baba Mtakatifu anongeza kusema, Nabii anatoa msukumo ili kujishusha na kuondokana na kiburi majivuno na uonevu. Mahali ambapo kuna kiburi, majivuno,uonevu, siyo rahisi Bwana kuingia kwasababu moyo huo umejaa kiburi, uonevu na majivuno. Tunatakiwa kuwa na tabia ya upole na unyenyekevu, bila kupiga kelele, kusikiliza, kuongea kwa upole na hivyo kuandaa kufika kuja kwake mwokozi, Yeye ambaye ni mpole na mnyenyekevu wa moyo.

Na kwa maana hiyo tunaalikwa kuondoa vizingiti vingi tunavyoweka katika muungano na Bwana, kufanya furaha ya kweli ambayo ndiyo maandalizi ya kufika kwa Bwana. Baba Mtakatifu anatoa mfano mmoja kwamba, tunapokuwa tunasubiri rafiki mpendwa, tunakuwa na furaha na maandalizi mema. Kwa namna hiyo, ndiyo namna ya kujitayarish kwa ajili ya Bwana: kumsubiri kila siku kwa ili kuweza kutulizwa na neema yake atakapokuja.

Mwakozi tunayemsubiri, Baba Mtakatifu anongeza, anao uwezo wa kubadili maisha yetu kwa neema zake, kwa nguvu za Roho Mtakatifu, kwa nguvu ya upendo. Roho Mtakatifu anayetutia upendo katika mioyo yetu kisima kisichonyauka na kututakasa, maisha mapya na uhuru. Mama Maia aliandaa kuja kwake Kristo, kwa kujitoa kabisa maisha yake yote, akaacha abatizwe na Roho Mtakatifu ambaye alimjaza kwa nguvu zake.

Mara baada ya tafakari ya Sala ya Malaika wa Bwana, Baba Mtakatifu amekumbusha juu tuzo ya Nobel ya Amani kwa Kampeni ya Kimataifa kwa ajili ya kupiga marufuku silaha za kinyuklia , inayokwenda sambamba na Siku ya Kimataifa kwa ajili ya Haki za Binadamu. Baba Mtakatifu anasema, upo uhusiano wa nguvu kati ya haki za binadamu na kupiga marufuku wa silaha za kinyuklia. Na hivyo ametoa wito kwa viongozi wa dunia kupiga vita silaha za nyukilia kwa ajili ya kulinda haki za binadamu hususani kwa watu walio dhaifu na masikini. Anasisitiza kuwa, kuna haja ya kuwa na dunia isiyo na silaha za kinyukilia.

Kujikita katika utetezi wa haki ya kila mtu kwa namna ya pekee wale wadhaifu na wasio kuwa na fursa, ina maana ya kufanya kazi na maazimio ya kujenga dunia isiyo kuwa na silaha za kinyuklia. Mungu anatupatia uwezo wa kufanya kazi pamoja kwa ajili ya ujenzi wa nyumba yetu: kwa maana tunao uhuru, akili na uwezo wa kuongoza teknolojia, kuweka vipangamizi vya nguvu, ili kuweza kutoa huduma kwa ajili ya amani na maendeleo ya kweli.
Mawazo ya Baba Mtakatifu yanakuja ikiwa ni siku ambayo kundi lililoshinda tuzo ya mwaka huu ya amani ya Nobel likitoa wito kwa mataifa yenye nguvu za nyukilia kutekeleza mkataba wa Umoja wa Mataifa unaopiga marufuku silaha za nyuklia.

Hata hivyo Baba Mtakatifu ameonya mara nyingi, juu ya madhara ya silaha za nyukilia kwa binadamu pamoja na mazingira katika kipindi hiki ambacho pia mivutano inazidi kuongezeka kati ya Marekani na Korea Kaskazini. Na kwa njia hiyo, Baba Mtakatifu akiwa msitari wa mbele juu ya utetezi na ulinzi wa mazingira, anatumaini kuwa mkutano ulio anza mjini Paris utatoa uamuzi madhubuti wa kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.
Ikumbukwe kila tarehe 10 ya mwezi Desemba ya kila mwaka ni kawada ya kutoa tuzo ya Nobel ambayo ni kwa ajili ya Amani huko Aslo, pia kwa ajili ya Tiba, Fisikia, Kemia, Fasihi na Uchumi huko Stocolm.

Kwa mwaka huu 2017, waliopokea tuzo kwa ajili ya amani ni Shirika la ICAN ambalo ni Kampeni ya Kimataifa katika juhudi za kupiga marufuku silaha za nyuklia. Kwa njia hiyo tuzo ya amani imemwendea Mkurugenzi mtendaji wa shirika la ICAN, Beatrice Fihn mwenye umri wa miaka 35 kutoka Sweden na Setsuko Thurlow leo hii akiwa na umri wa miaka 85, manusura wa shambulio la bomu la atomiki la Marekani dhidi ya mji wa Japan-Hiroshima.
Wakati huo huo mfalme Gustav Carl wa XVI (16) wa Sweeden amewakabidhi washindi wa tuzo za Nobel za Tiba, Fizikia,Kemia,uchumi na fasihi mjini Stockholm. Tuzo ya fasihi amenukiwa mwaka huu mwandishi vitabu wa Uingereza Kazuo Ishiguro.

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.