2017-12-11 16:27:00

Papa:Acha ufarijiwe na Bwana,usipende kulalamika na hasira hovyo


Acha ufarijiwe na Bwana na usipendelee kulalamika na kuwa na vinyongo na machungu ndani ya moyo wako. Hayo ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko akitoa wito katika mahubiri yake kwenye Kikanisa cha Mtakatifu Marta mjini Vatican  wakati wa kuadhimisha misa, asubuhi ya tarehe 11 Desemba 2017.

Baba Mtakatifu akitafakari kuhusu somo la kwanza kutoka kitabu cha Isaya 35,1-10  ni mahali ambapo Bwana anatoa ahadi ya faraja kwa watu wake.Bwana alikuja kutoa faraja, Baba Mtakatifu anasema, hata Mtakatifu Ignazio anafundisha kuwa, ni vema kutafakari sala ya faraja ya Kristo akifananisha kwa namna nyingine na baadhi ya marafiki wanao watuliza wengine. 

Pamoja na hayo anasema, inatosha kufikiria siku ya kwanza ya Juma ya ufufuko ambapo Mwinjili Luka anasema Yesu aliwatokea mitume wake , ambao walikuwa na furaha ya kutoweza kuamini. Mara nyingi faraja za Bwana zinatoa mshangao anathibitisha Baba Mtakatifu! Lakini siyo rahisi wakati mwingine kuacha ufarijike. Ni rahisi kuwafariji wengine na kuwatuliza kuliko kujifariji binafsi. Hiyo ni kwasababu mara nyingi tunashikilia mambo hasi ,na kushikilia zaidi na majereha ya dhambi ndani mwetu. Mara nyingi kuna uchaguzi hata wa kubaki pekee yako katika kitanda, kama ilivyo kuwa  katika Injili ya siku. Mi kulala pale bila kusimama. Lakini Neno la Yesu lilisikika na linaendelea kusikika hata leo kwamba simama!

Akifafanua ugumu wa kutosimama, Baba Mtakatifu anasema tatizo ni kuwa, sisi ni bwana wa mawazo hasi, kwasababu ndani ya mioyo yetu yapo majeraha ya dhambi. Na katika mawazo chanya ndiyo sisi tunahitaji kuomba, wakati huo huo hatupendelei kuombaomba faraja hiyo. Baba Mtakatifu anatoa mifano  miwili ya kwamba, unapoendeleza chuki na kupika mchuzi hasi wa mabaya, nikuonesha moyo mchungu na kwa maana hiyo unabaki na ubaya ndani ya maisha yako. Aidha akiwaza kiwete katika  kisima cha Silowe, aliyekuwapo tangu miaka 38, kwa maana maji yalipokuwa yakitingishika hakuna mtu aliweza kumsaidia. Wengi walimwona, lakini hakuna aliyekuwa akimsaidia. Hiyo ina maana ya kubaki na uchungu ambao kwa watu wengi wanatamani kubaki hivyo. Na kwa njia hiyo binadamu nahaitaji kufarijika.

Sehemu ya pili ya uchungu ni ile ambayo inatupelekea kulalamika. Wapo watu wengi wanao lalamika mbele ya Bwana badala ya kusifu.Kulalamika kama muziki unaosindikiza maisha. Kutokana na kulalamika Baba Mtakatifu anamkumbuka Matakatifu Teresa wa mtoto Yesu aliyekuwa anasema ; ole wake mtawa anaye sema hakutendewa haki au wamenifanyia jambo lisilokuwa na sababu”. Aidha amekumbuka Yona, kwamba ni mwenye tuzo ya Nobel ya kulalamika. Alimkimbia Mungu kwasababu ya kulalamika kuwa, angeweza kufanya jambo, lakini akaishia kumezwa na nyangumi, na baadaye akarudi katika utume. Yeye badala ya kufurahi kwa ajili ya uongofu wa watu wake,alimlalamikia Mungu kwasababu ya kuwakomboa!

Kwa njia hiyo Nabii Isaya anaalika watu wawe na ujasiri kwasababu Mungu anakuja kuwakomboa: Baba Mtakatifu anatoa mfano mwingine akirudi katika Injili ya Siku kuwa watu walipanda juu ya paa kwasababu, kulikuwa na watu wengi, na kushusha kitanda mbele ya Yesu . Watu hao hawakufikiria kwamba kulikuwapo  waandishi au watu wngine, walichojali ni  uponyeshwaji wa mtu yule. Kwa njia hiyo ujumbe wa siku hii ni kwamba tuache tufarijiwe na  Bwana, japokuwa siyo rahisi kuacha ufarijike na Bwana, maana ili kufanya hivyo lazima ujivue ubinafsi, yaani yale mambo ambayo unafikiri ni tunu binafsi za chuki, uchungu na kama vile kulalamika na mambo mengine mengi.

Leo hii inaweza ikawa mwafaka wa kujitafiti dhamiri binafsi ya moyo wako kuona kama unayo machungu, hasira, huzuni na lugha unayotumia. Je unamsifu Mungu au daima ni unalalamika? Basi ni kumuomba neema ya ujasiri ili aweze kuja na kukufariji!

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kisahili ya Radio Vatican

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.