2017-12-07 16:57:00

Papa:Si Mungu anayetutia katika majaribu,bali ni Shetani,ndiyo ofisi yake!


Baba Mtakatifu ameendelea na mazungumzo na Padre Marko Pozza muhusika wa Kanisa dogo la Gereza huko Padua Italia,  katika program ya Televisheni 2000 ya Baraza la Maaskofu Italia  ambapo katika vipindi tisa kuhusu mada ya Baba Yetu, tarehe 6 Desemba 2017, usiku  wa saa 3.05 kimefikia kipindi cha 7. Na  katika kipindi hiki alikuwawapo mgeni, mtaalamu wa falsafa Bwana Umberto Galimberti.

Baba Mtakatifu anafafanua  na kusisitiza kuwa, katika sala ya Baba yetu, Mungu anayetutia katika majaribu siyo tafsiri nzuri nali tafsiri nzuri inaweza kuwa “usiniache nianguke  katika majaribu” , kwa maana, “ni mimi ninayeanguka, na si Mungu anayekuangusha katika majaribu ili akuone unavyo anguka, hiyo ni kwakuwa, baba hawezi kufanya jambo la namna hiyo, badala yake anamsaidia mwanae kuamka haraka!

Baba Mtakatifu akizungumza na Padre Pozza katika utangulizi wa vipindi hivyo juu ya Baba yetu, amethibitisha ukweli huo kwamba anayetutia katika majaribu ni shetani , na ndiyo ofisi ya shetani!

Program za vipindi hivi imeanzishwa kwa ushirikiano katika ya Sekretarieti ya Mawasiliano Vatican na Kituo cha Televisheni (TV2000 cha Baraza la Maaskofu wa Italia, Kipindi ambcho kimetengwa kwa vipindi 9, kila Jumatano usiku,Padre Marco Pozza anakutana pia na watu wengine walei katika ulimwengu wa taaluma ya utamaduni na usanii. Kwa njia hiyo katika kipindi cha 7, mgeni alikuwa ni mwanafalasafa Umberto Galimberti.

Ikumbukwe kwamba kattika makutano, maneno na majibu ya Baba Mtakatifu na Padre Marco Pozza, kimetolewa kitabu cha Baba yetu "Papa Francisko", kinachopatikana kwa sasa katika maduka ya vitabu Vatican.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.