Kuna kazi nyingi ambazo kama wakristo tunaalikwa kutenda pamoja na kuhamasisha hadhi ya kila binadamu.Ni wito wa Baba Mtakatifu Francisko katika hotuba yake kwa wajumbe wa Baraza la Ushauri la Taifa la Makanisa ya Taiwan , aliowapokea tarehe 7 Desemba 2017 katika Ukumbi wa Mkutano mjini Vatican.
Akitaja Injili ya Mtakatifu Yohane ,mahali ambapo anasema, “ kama mimi nilivyo
wapenda ninyi, nanyi pendaneni, kwa maana mkipendana, watu wote watajua kwamba nyinyi
ni wanafunzi awangu” (Yoh 13,34-35),anakumbusha kuwa,ili upendo wa Mungu uweze kujikita
kwa dhati ndani ya maisha, kila mkristo anaalikwa kuwajibika kwa kushuhudia mbele
ya ulimwengu, matumaini ambayo yamo ndani mwetu .
Na ndiyo maana ya ulazima na muhimu wa kutia jitihada hasa katika mahusiano kati ya
imani za kikristo na kutangaza Kristo, hata kwa njia ya matendo ya upendo, hasa zaidi
juu ya mipango ya mafunzo kwa vijana endelevu, kwa namna ya pekee kwa njia ya kuwafundisha
mazungumzo ili kuweza kuunda jamii yenye haki.
Baba Mtakatifu anasema, Kanisa, tangu kuundwa kwa Baraza la Ushauri la Taifa kwa
ajili ya Makanisa ya Taiwan mwaka 1991, limejikita katika kuhamasisha kwa namna ya
pekee umoja kati ya waamini, katika Bwana na kuongeza jitihada za mashusiano kati
ya imani za kikristo.
Na mwisho wa mkutano, kabla ya kuwaalika kusali kwa pamoja sala ya Baba Yetu, ameeleza
matumaini yake na shahuku ya kutaka kutembea kwa pamoja katika upendo mkuu ili kuelekea
siku ile ambayo Bwana Yesu anapenda kuwaona wote wanakuwa wamoja na ili dunia ipate
kuamini!
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |