Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Katekesi siku ya Jumatano

Papa:Wito kwa ajili ya Yerusalem,mji Mtakatifu wa Wayahudi,Wakristo na Waislam

Papa ametoa wito kwa ajili ya Yerusalem, mji Mtakatifu wa Wayahudi,Wakristo na Waislam

06/12/2017 16:13

Mara baada ya Katekesi yake yake Jumatano 6 Desemba 2017, Baba Mtakatifu ameonesha  wasiwasi mkubwa  kuhusiana na nchi ya Yerusalemu na hasa mara baada ya Rais wa Marekani  kutaka kuhamisha ubalozi wake katoka Tel Aviv,  Israeli kwenda katika mji Mtakatifu wenye kuwa na dini tatu za kiyahudi, kikristo na kiislam.

Baba anasema Yerusalem ni mji mmoja mtakati kwa ajili ya wahahudi, wakristo na waislam wakiheshimu maeneo Matakatifu kulingana na dini zao.Vilevile na wito maalumu kwa ajili ya  amani, kwa njia hiyo, anaomba Bwana Mungu ili utambulisho huo uweze kutunzwa na kulindwa kwa ajili ya wema wa nchi Takatifu na nchi za Mashariki na katika dunia nzima, ili itawale hekima, busara ili kuziua kuongeza mivutano mipya ambayo  tayari imeandama dunia na ishara nyingi  za ukatili wa migogoro.

Mwisho amewasalimia wahujaji wote hasa zaidi wa kutoka Poland kwa namna ya pekee waliojikitika kutoa zawadi na kuleta katika uwanja wa Mtakatifu Petro mti wa Krismasi, pia amekumbusha kuwa Jumapili ijayo nchini Poland wataadhimisha Siku ya Sala kwa ajili ya Kanisa hitaji la Mashariki. Kwa namna hiyo anawawakabidhi kwa Mungu matendo hayo, ambayo ni ishara ya umoja kwa ajili ya kusaidia waamini na wachungaji wa nchi zinazopakana na nchi hiyo.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

06/12/2017 16:13