Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Hotuba

Papa:Walimu wa Kilatino waoneshe hekima na busara za mababa kwa kizazi endelevu

Walimu wa Kilatino waoneshe hekima na busara za mababa kwa kizazi endelevu - RV

06/12/2017 16:26

Tarehe 5 Desemba mjini Vatican , yameungana mabaraza 7 ya Kipapa katika maadhimisho XXII ya pamoja, ya yaliyoongozwa na Kardinali Gianfranco Ravasi, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Utamaduni:Na katika muungano huo Baba Mtakatifu Francisko hakukosa kuwatumia ujumbe kama, ambapo anawaeleza kuwa, kipindi cha kushirikishana kwa pamoja  ni fursa ya kutafakari mikakati msingi kwa ajili ya kutazama upeo wa binadamu kiakili.

Maadhimisho ya kukutana kwa pamoja yalianza tangu mwaka 1995 ambako kila mwaka wanafanyia sherhe hizo taasisi moja baada ya nyingine  ambayo baadaye utunukiwa hata zawadi. Kwa njia hiyo kiongozi wa mwaka huu ni Taasisi ya Kipapa ya Elimu ya Kilatini (Latinitatis)  wakiongozwa na mada ya (In interiore homine) Maana yake, mchakato wa utafiti katika utamaduni wa kilatino.

Baba Mtakatifu akiwapongeza kwa mada iliyochaguliwa,  ujumbe wake unasisitizia juu ya kiini cha uzoefu kwamba, si tu wa kikristo pekee bali hata wa kibinadamu, maana ya undani, ya moyo, dhamiri na utambuzi binafsi. Mambo haya yanaunganisha mila na desturi tofauti za kidini na utamaduni katika kutoa mapendekezo kwa mantiki kubwa ya dharura katika  nyakati zetu, kipindi  ambacho daima kinaonesha  tabia ya kijuu juu na purukushani katika ndani ya kitengo kati ya moyo na akili, undani na nje, dhamiri na mwenendo.

Baba Mtakatifu anabaisnisha kuwa  kuna mahitaji makubwa katika kipindi cha mgogoro, marekebisho na mabadiliko ambapo  si tu katika mahusiano ya kijamii lakini pia hasa  juu ya mtu na utambulisho wake wa kina na kwa njia hiyo ni wito wa kutafakari juu ya mambo ya ndani kwa kina na  juu ya kiini cha nini maana ya kuwa binadamu.  Ili kuweza kutafakari suala hili kwa kina  Baba Mtakatifu anatumia Neno la Injili inayoelezea Baba Mwenye huruma, kwa namna ya pekee, ya mtoto mpotevu kwamba baada ya kujirudi kwa kina alifikiri ni vema kurudi nyumba na ndipo akasema, “ nitaamka na kwenda kwa Baba yangu…(Lc 15,17-18).

Hiyo ni nguvu ambayo  kwa ufupi  ni maisha ya Mkristo na mwanadamu katika nguvu ya kwanza ya kujikita katika maisha ya ndani na baadaye ya nje, ambayo hutoa msukumo wa kuelekea  katika mwendo wa uongofu na  katika mabadiliko ya kina, ya dhati na sio ya unafiki, na  kwa maana hiyo ndiyo ya  maendeleo kamili na halisi ya binadamu. Aidha Baba Mtakatifu anaendelea kufafanua kuwa, wasomi na wataalam wengi wa kizamani, na katika ulimwengu wa sasa wa kikristo walitafakari, na wanatafakari  kuhusiana na mwenendo huo wa undani wa binadamu: Kwa mfano anamtumia, Mtakatifu Agostino  anaye andika katika kitbu chake cha “maungamo” (Confessioni) na katika “dini ya kweli” (De vera religione),

Yeye  anauliza juu ya maelewano ya kweli na akifafanua hekima ya kale na maneno ya Injili, anathibitisha na kusema kuwa,"Usiende nje yako mwenyewe, jirudi mwenyewe; ukweli unakaa ndani ya mtu wa ndani na, ikiwa utapata asili yako imebadilika, jishughulishe hata wewe pia” (39,72).
Baba Mtakatifu anasema, tafakari ya Mtakatifu Agostino, inatoa mwangwi kutoka katika tafakari ya Injili ya Mtakatifu Yohane 18,10) kwa ufafanuzi  kwamba rudini ndani ya mioyo yenu! Je ninyi mnataka kwenda mbali? Mkienda mbali mtapotea. Je ni kwanini mnajikita katika barabara ya jangwa? Baba Mtakatifu anasisitiza, kwa maana hiyo Mtakatifu Agostino, anatoa wito wa kutazama mwelekeo, mahali ambapo ndiyo mwisho wa safari ya binadamu. Ni kazi ya kujirudi ndani ya moyo na kuchunguza dhamiri ili kujua Mungu ni nani, kwa maana hapo ndipo  unapata sura ya Mungu na Yesu Kristo anaishi ndani ya moyo wa binadamu.
 
Akitafakari, juu ya huo  uthibitisho wa kupendeza  matokeo yake ni ya ajabu sana, anasema, hasa kwa kijana, ambaye anaanza kugundua dunia  kubwa ya maisha ambapo mara nyingi hubakia kushiriki katika mzunguko usio isha wenye kujaa udhaifu wa kijujuu, utupu au kulenga juu mafanikio ya nje tu  ambayo huficha udhaifu wa ndani, au unafiki ambao uweka kizingiti na huzuia uwazi wa kuonekana nje  na moyo.

Wito wa Baba Mtakatiu kwa Taasisi na washiriki wa  maadhimisho na Mkutano huo wa umma na kwa   namna ya pekee wenye shughuli ya kufundishia, na kuonesha hekima ya mababa, ambao wanapatikana katika vitabu vya utamaduni wa Kilatino: watambue kuongea katika mioyo wa vijana, watambue kutoa tunu inayotajirisha urithi wa tamaduni la kilatini,  kuwaelimisha juu ya safari ya maisha, kuwasindikiza katika njia ndefu ya utajiri wa hekima na imani,  kuchota kutoka katika kisima cha uzoefu  na hekima ya walio onja furaha na ujasiri wa kuingia kwa kina ndani ya moyo binafsi  ili kuweza kufuata na kuwa na utambulisho na wito wa binadamu. 

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahil ya Radio Vatican

 

06/12/2017 16:26