Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Hotuba

Papa:Mazungumzo yanawezekana kwa ngazi zote:binafsi,sala,familia na jamii

Papa amekutana na wawakilishi wa Baraza la Kipapa la Mazumguzo ya kidini na Kamati ya Palestina kwa ajili ya Mazungumzo ya kidini.

06/12/2017 16:38

Tarehe 6 Desemba 2017, Baba Mtakatifu amekutana na wajumbe wa Mkutano wa Kamati ya Kudumu ya mazungumzo ya kidini  na wahusika wa kidini kutoka nchi ya Palestina mjini Vatican, ambapo amefurahi kukutana nao wakiwa katika utafiti na ugunduzi,  ili waweze kuunda Makundi ya kazi ya kudumu kwa ajili ya mazungumzo kati ya Baraza la Kipapa la Mazumguzo ya kidini na Kamati ya Palestina kwa ajili ya Mazungumzo ya kidini.

Baba Mtakatifu akifafanua zaidi juu ya mazungumzo anasema: Kwa upande wa Kanisa Katoliki, daima imekuwa ni furaha ya ujenzi wa madaraja ya mazungumzo na jumuiya , watu na taasisi ambazo kwa hakika ni furaha ya pekee kukutana na watu wa dini na wataalam wa Palestina. Nchi Takatifu kwa upande wa wakristo inajulikana kuwa ndiyo ya mstari wa mbele ya mazungumzo kati ya Mungu na binadamu. Mazungumzo yaliyofanyika  huko Nazareth kati ya Malaika Gabrieli na Maria,  na vile vile ni matukio yanayoonekana hata katika maandiko ya Kuran. Mazungumzo pia yanaendelea kwa namna ya pekee kati ya Yesu na watu wake wanao wakilisha binadamu wote. Kuonesha hiyo kwa dhati, Yesu ni Neno  la  Mungu anaye zungumza na watu wake.

Mazungumzo yanaanzishwa katika ngazi zote:  binafsi, kwa njia ya kutafakari na  maombi, ndani ya familia , katika jumuiya nzima ya dini, kati ya jumuiya tofauti za dini, hata  jamii ya raia.  Jambo la kwanza msingi katika mazungumzo ni heshima ya pamoja, wakati huo huo kujikita zaidi katika kudumisha heshima ili mwishowe, kutambuana watu wote, kila mahali wanapokuwa  haki zao. Mazungumzo yanatoa fursa kubwa ya utambuzi wa pamoja, hata kuelewana  na kushirikiana kwa lengo la kutaka kujenga wema wa pamoja na kufanya harambee ya kukabiliana na watu wenye kuhitaji na  kuwahakikisha msaada wao wa lazima.

Baba Mtakatifu anawatakia matashi mema ili waweze kufikia hatua halisi ya kuunda nafasi ya  mazungumzo ya kweli ambayo inawezesha kutoa nafasi kwa jamii nzima ya Palestina, kwa namna ya pekee ya wakristo kwa kufikiria mahitaji mengi na changamoto ambazo wote tunaalikwa kuwajibika na kutoa kujibu kwa namna ya pekee kuhusiana na wahamiaji.

Aidha anao utambuzi wa  Serikali ya Palestina kuwa makini na kwa njia ya pekee Rais Mohmoud Abbas, akisaidia jumuiya ya Kikristo  kutambua nafasi yao na shughuli zao katika jamii ya Kipalestina. Kwa wote amewapa baraka za Mungu na kuwatakia amani na matarajio mema ya nchi ya Palestna, nchi Takatifu na nchi zote za Mashariki.

Sr Amgela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

06/12/2017 16:38