2017-12-05 15:50:00

Nia ya Maombi ya sala kwa mwezi wa 12 ni kwa ajili ya wazee wasisahuliwe!


Utunzaji wa wazee ni muhimu kwa kuendeleza elimu kwa kizazi endelevu. Ndiyo ujumbe mkuu wa Baba Mtakatifu Francisko kwa njia ya video akiwakilisha nia ya sala kwa mwezi wa kumi na mbli, ambapo anasisitizia juu ya kutazama na kujidunza kutoka katika hekima ya mababu na nafasi muhimu waliyo nayo katika jumuiya.

Kwa ujumbe wa Baba Mtakatifu katika Siku ya 55 ya Kuombea Miito dunianiani siku ambayo itaadishimwa tarehe 22 Aprili 2018, Baba Mtakatifu ameonesha hali halisi ya wito wa mkristo wa kuwa karibu na wengine na anasema ni vizuri na ni neema kubwa ya kujikabidhi moja kwa moja katika wakfu kwa Mungu na katika huduma ya ndugu.

Na kwa njia hiyo  historia ya familia katika Jumuiya ya watu! Ndiyo  mada ya video ya Baba Mtakatifu Francisko katika nia yake  ya sala kwa mwezi wa Desemba 2017. Huo ni wito mkubwa anao utoa ili watu wawe na dhamniri safi hasa ile ya kuwasaidia, bila kuwasahau wazee kwani hiyo pia ni hekima ya kuwatunza.

Wito huo pia unatokana na maneno ya mahubiri yake aliyofanya katika Misa ya tarehe 28 Septemba 2014  wakati Baba Mtakatifu anaadhimisha Sikukuu ya wazee katika uwanja wa Mtakatifu Petro, mahali ambapo alitafakari juu ya makutano kati ya kijana Maria na mzee mwenye hekima Elizabeth, Baba Mtakatifu anarudia kusisitiza katika video kuwa watu ambao hawatunzi wazee na kuwajali vema ni watu wasio kuwa na wakati endelevu.

Kutojali na sintofahamu mbele ya wazee wa jamii yetu ambao Baba Mtakatifu anazungumza, wanawakilishwa katika video kwa kuonesha  picha ya maisha ya wazalendo: wazee watatu wakitembea katika barabara, mojawapo ya msongamo wa watu wengi, lakini watu hao hawajali wazee hao. Safari wazee hao inawapeleka kuungana katika sehemu mmoja ambapo wote watapiga vyombo vya muziki.

Baba Mtakatifu anasema, wazee wanayo hekima ambayo wamekabidhiwa ili kuonesha uzoefu wa maisha katika historia ya familia, jumuiya na katika watu.
Katika picha  pia inaonesha wazee watatu wakiendelea  kupiga muziki, ni kijana mmoja tu anaye waona na kuwasikiliza kutokana na kwamba amefurahia mapigo ya muziki wao na hiyo naye anaingia ndani ya jengo hilo akiwa na kifaa cha muziki na kuungana na wazee hao,ambapo wote wanne wanapiga vizuri vyombo vyao katika mlio mzuri wa kuvutia

Kutokana na hili, ndilo fundisho la ujumbe kwamba,  kwa njia mchakato wa hatua za utamaduni kuelekea katika elimu, ndiyo nia  ya sala kwa ajili ya mwezi wa kuzaliwa kwa Bwana:Na hivyo mwisho Baba Mtakatifu anasititiza , wasisahau wazee , kwasababu katika kusaidiwa na familia na taasisi , wanaweze kutoa mchango wao wa hekima na uzoefu wa elimu katika vizazi endelevu.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.