Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Hotuba

Papa:Safari yangu inafanikiwa hasa ninapokutana na watu wa Mungu!

Papa Francisko akizungumza na waandishi wa habari katika ndege ya kurudi Roma amesema alilia na watu wa Rohingya - RV

04/12/2017 15:00

Safari inafanikiwa hasa ninapoweza kukutana na watu! Ni maneno ya uhakika wa Baba Mtakatifu alioutoa wakati anazungumza na kujibu maswali ya waandishi wa habari wakati wa kurudi  na ndege kutoka  Bangladesh kuja Roma. Mkutano wa waandishi wa habari ulianza nusu saa mara baada ya kutoka uwanja wa ndege wa Dhaka. Baba Mtakatifu Francisko, ameweza kuzungumza na wandishi wa habari kwa muda wa dk 58 na hasa mada juu ya masuala ya kibinadamu kwa namna ya peke ya Warohingya, kusitisaha silaha za kinyukilia na uwezekano wa ziara nyingine katika bara la Asia na hasa uwezekano wa nchi ya China.

Baba Mtakatifu akijibu swali, kuhusiana juu ya ziara yake amesema, anafurahia ziara yake  na hasa kufanikiwa anapokutana na watu wa nchi ambao ni watu wa Mungu,kukutana nao, kuwasikiliza au kuwasalimia . Ameweza kukutana na viongozi wa kisiasa lakini zaidi kwake ni ile hatua ya kukutana na watu ambao ndiyo msingi wa nchi na ndiyo furaha kamili ya Baba Mtakatifu. Amejibu masali hayo kutokana na ukawaida wa waandishi wahabari kutaka kujua zaidi ni kitu gani Mkuu wa Kanisa anafikiria hasa kuhusu juu ya watu wa Rohingya, mojawapo ya kabila linaloteswa katika dunia. Waandishi wa habari walitaka kusikia sauti ya Papa, nini ameweza  kuwakilisha katika  mkutano wa Ijumaa alipowakumbatia kikundi cha wakimbizi mbele ya macho ya sayari hii.    

Hata hivyo Baba Mtakatifu kuhusiana na suala hili,anasema la muhimu ujumbe umefika, pamoja na kwamba hasiwengeza kutamka neno la Royingya katika hotuba rasmi maana wangefunga milango mbele yake. Hata hivyo Baba Mtakatifu hafichi hasira yake aliyoipata kidogo kutokana na tabia moja aliyoiona hapo jukwaani. Pamoja na hayo yeyealiweze kuelezea hali halisi kuhusu haki za binadamu na kwamba kila mmoja anastahili, bila kutengwa. Na kwa njia hiyo ameridhika sana na mazungumzo aliyofanya na viongozi wa huko, kwasababu yalikuwa ya kweli pia hawakuweza kumfungia mtu yoyote mlango.

Aidha Baba Mtakatifu aneleza jinsi gani alivyoishi katika Mkutano wa madhehebu ya kidini huo Dhaka na kwamba alilia na Warohingya wakiwa wanatokwa  machozi machoni mwao, hata hivyo pia aliomba wawe na  heshima kwao kutokana na  wale  waliotaka kuwafukuza kuondoka  jukwaani, huo ulikuwa ni ushauri alioomba kwa viongozi wa madhehebu ya dini ili warohingya wawe karibu naye. Kuhusiana na wakimbizi, pia Baba Mtakatifu amesema kuwa alifikiri kwenda katika kambi ya warohingya japokuwa kulikuwa na matatizo ya maandalizi.

Swali jingine kuhusu sura ya Aung San Suu Kyi, mwenye tuzo ya Nobel ya amani kwa ajili ya utetezi wa demokrasia ya Birmania, leo hii yeye ni Mshauri wa Nchi na Waziri wa mambo ya nchi za nje Birmania. Baba Mtakatifu amesema,nchini Myanmar hali ni ngumu ya kuweza kutathimini bila kuuliza. Japokuwa hali ya kisiasa inaendelea kukua na sera zeke lakini ikumbukwe kuwa nchi bado iko katika kipindii cha mpito , yenye kuwa na thamani nyingi za kiutamaduni, historia, lakini pia katika kisiasa ni kipindi cha mpito, hivyo lazima uwepo uwezekano wa  kutathimini katika mtazamo huo.

Akijibu juu ya suala la Jenerali wa Birmania aliyekutana naye mapema  kabla ya ratiba rasmi iliyokuwa imepangwa, Baba Mtakatifu amethibitisha, jinsi alivyokutana naye kutokana na maombi, lakini bado kulikuwa na shida ile ile ya jina la Rohingya,lakini kipindi chote cha mazungumzo, alitumia maneno yote aliyotaka kusema, bila kutumia jina hilo. Hata hivyo siyo rahisi kuendeleza mbele  ya ujenzi , wakati huohuo huo hata kurudi nyuma, ni muhimu kwenda mbele , kwa sababu amesikia  kuwa katika Serikali ya Rakhine ni tajiri sana kutokana na kwamba wana utajiri wa almasi na inawezekana ndiyo sababu ya watu kufukuzwa wasiishi katika ardhi ile. Pamoja na hayo Baba Mtakatifu hana uhakika na hivyo anasema inafanya ufikirie kama ilivyo Afrika.

Swali jingine lilikuwa ni kitu gani kimebadilika kwa miaka hii tangu  hotuba ya Mtakatifu Yohane Paulo II mwaka 1982 kuhusiana na na salaha za kinyuklia ambapo Baba Mtakatifu Francisko anazidi kushutumu , kwa kutazama hata kipeo cha Korea ya Kaskazini na Marekani. Anasema nyakati zetu, kuna mabadiliko makubwa: Leo hii kuna ukomo,na inawezekana kusitisha silaha za kinyuklia kwa njia ya majadiliano.

Je ni kwanini tuko katika ukomo wa kupokea na kutumia silaha za kinyuklia? Baba Mtakatifu anasema, leoo hii viwanda vinaendelea kutengeneza nyuklia, kuleta hatari ya kuharibu ubinadamu. Ni  silaha za hatari na ukatili wenye uwezo wa kuharibi watu bila kuharibu majengo. Ni hatari!Akifafanua zaidi anasema silaha hizo ni za hatarari na kuna aina mbili za utamdunisho: kwanza utumadunisho ambao Mungu ametupatia kuutenda katika utamaduni, katika kazi, katika upelelezi(Utafiti) na mbele  utamaduni wenyewe. Kwa kufikiria sayansi ya madawa, ambayo imeendelea sana, tamaduni nyingi, katika ufundi na mambo mengine.

Binanadamu amepewa madaraka ya kutumia utamaduni kuanzia utamadunisho alio upokea. Lakini wakati huo anafikia hatua kuwa na utamaduni mikononi mwake wa kufanya utamaduni wake tena. binadamu anao utamaduni mikononi mwake: Firikiria huko Hiroshima na Nagasaki. Miaka 60 na 70 iliyopita ya uharibifu mkubwa. Hiyo inatokea wakati nguvu ya atomi ina uwezo wa kujichungaza yenyewe, aidha  fikirieni hajali nchini Ukraine. Kwa nia hiyo Baba Mtakatifu anathibitisha kuwa kuna haja ya kusitisha silaha za kinyuklia.

Akijibu swali kuhusu Uinjilishaji, Baba Mtakatifu ametaja Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kuwa alisema Kanisa halipo kwa ajili ya kufanya propaganda, bali linajieleza lenyewe na matendo yake. Kwa njia hiyo mazungumzo yameendelea juu ya safari ya kitume ambayo anatarajia, lakini pia ile ambayo haikufanyika ya India. Na hata suala la utashi wa kupendelea kwenda China. Masuala ya China yako katika ngazi kubwa ya utamaduni. Lakini pia kuna mazunguzmo kisaisa, zaidi kwa ajili ya Kanisa la China na  Kanisa la kujificha, vyote hivyo vinapaswa kwenda katika njia moja kwa makini na inahitaji uvumiluvu, pamoja na kwamba milango ya mioyo iko wazi.

Akijibu juu ya suala la kutoa daraja la upadre aliofanya katika ziara yake, Baba Mtakatifu amesema, mara nyingi yeyé ana tabia ya kutumia dakika chache kabla ya maadhimisho kuongea na wateule kwa faragha. Na vijana hao walionekana kuwa na utulivu na dhamiri safi ya uwelewa wa utume katika maskini na pia watu wa kawaida. Na pia aliwauliza kama wanacheza mpira wa miguu kwa maana ni muhimu.

Pia baada ya kuongea nao, aliweza pia kuongea na walimu wao, ambao walimsimulia kuwa kabla ya kuingia seminarini kwanza yapo maandalizi ya seminari ili weweze kujia na kujifunza namna ya kuishi katika seminari, vilevile hata kujifunza lugha ya kingereza ambayo inawaunganisha katika jumuiya, kutokana na kwamba wanatoka katika makabila tofauti. Ni vijana wanaotambua kukaa na watu karibu maana ndiyo wito wao. Amemalizia akiwashukuru sana waandishi wa habari  kwa maswali pia kwa yote waliyo fanya katika ziara hiyo na hivyo ni muda wa chakula na kupumzika amewatakia mlo mwema na usiku mwema!

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

04/12/2017 15:00