2017-12-04 16:16:00

Papa:Nitazidi kuwakumbuka katika moyo wangu watu wa Myanmar na Bangladesh!


Majilio ni kipindi ambacho tumepewa na kupokea kutoka kwa Bwana anayekuja kwetu ili kusaidia kutazama utashi wetu juu ya Mungu, kutazama mbele na kuandaa siku ya kurudi kwake Kristo. Ni katika maneno ya mahubiri yake Baba Mtakatifu Francisko  Jumapili ya kwanza ya Majilio, tarehe 3 Desemba 2017 ambapo ametafakari juu ya maana ya kipindi hiki muhimu kwa mahujaji wote waliofikia katika viwanja vya mtakatifu  Petro kusali naye sala ya Malaika wa Bwana.

Baba Mtakatifu anasema,m Yesu katika Injili inatualika kuwa tayari na kukesha. “Je ni ni mtu gani anayalikwa kuwa  tayari? Ni yule ambaye katika kelele za ulimwengu hasumbuliwi  au kujidai kwa maana  yeye anaishi kikamilifu, anao utambuzi wa mahangaiko kwa kuwatazama zaidi wengine.  Aidha akifafanua zaidi ya yule aliye tayari anakesha anasema;  anaweza kutambua machozi na mahitaji ya jirani na kupokea hata ule uwezo na thamani ya kibindamu na kiroho, kwa kutafuta kupinga sintofahamu na ukatili wa sasa katika ulimwengu .Yeye  anao uwezo wa kufurahia  tunu za uzuri uliopo ambao unapaswa kulindwa. Lakini hiyo baba Mtakatifu anasisitiza kuwa inahitaji kuwa na mtazamo wa huruma kwa kutambua matatizo na umaskini wa kila mtu katika jamii, hata kutambua utajiri uliojificha katika mambo madogo madogo ya kila siku, mahlai ambapo Mungu ametuweka.

 Je ni nani akeshaye? Akifafanua  anasema: Ni yule anayepokea wito wa kukesha bila kukata tamaa na kukosa matumaini, wakati huohuo anapinga tabia mbaya za ubatili mwingi ambao upo nyuma ya dunia hii na wakati mwingine  kufikia kutoa hata   sadaka ya muda wake na utulivu binafsi na familia. Kuwa tayari na kukesha ni mambo ambayo ni muhimu kwasababu ya kuruhusu Mungu avunje vunje ugumu wetu ndani ya moyo na kutoa maana  authamani ya uwepo wake wa wema na huruma. Mwisho Baba Mtakatifu ameomba Mama Maria ili aweze kutuongoza kukutana na Mwanae Yesu Kristo na kutuongezea upendo mwingi kwa ajili yake.

Mara baaada ya mahubiri,mawazo ya Baba Mtakatifu katika tafakari ya  Malaika wa Bwana,katika viwanja vya Mtakatifu Petro Jumapili 3 Desemba 2017, yamerudi katika Ziara ya 21 ya Kimataifa ya kitume nchini Myanmar na Bangladesh, aliyotimizia  Jumamosi 2 Desemba 2017 , kwa njia hiyo maneno yake ya kwanza yalikuwa ni asante Bwana kwa ajili ya kumwezesha kukutana watu hao, hasa jumuiya katoliki na kuimarisha ushuhuda wao.

Ni mshangao mkubwa kukumbuka sura za watu wengi waliojaribiwa na maisha lakini wakitabasamu. Kwa maana hiyo ataendelea kuwaweka ndani ya moyo wake na kuwakumbuka katika sala. Amewashukuru watu wa Myanmar na Bangladesh. Aidha  Katika moyo wa Papa pia  ameshutushwa na ghasia za nchi nyingine  kwa kufikiria   maisha ya kijamii hasa baada ya uchaguzi wa rais Jumapili iliyopita: Katika sala anakumbuka kwa namna ya pekee watu wa nchi ya  Hunduras, nchi hiyo iweze kutulia ghasia zilizopo  na  amani iweze kutawala.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

 

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.