Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Hotuba

Kard.Rozario Askofu Mkuu wa Dhaka ametoa shukrani kwa upendo wa Papa!

Kardinali Patrick D'Roazario amemshukuru Baba Mtakatifu kwa upendo mkuu wa ka nchi ya Bangladesh - AFP

01/12/2017 12:43

Baada ya misa Takatifu ya kutoa daraja Takatifu la Upadre kwa mapadre wapya 16, naye Kardinali Patrick D’Rozario, Askofu Mkuu wa Dhaka, ametoa hotuba yake fupi ya kumshukuru Baba Mtakatifu Francisko  ya kuwa,anapenda nchi ya Bangladesh, kwa maana ameonesha hivyo kwa njia nyingi. Na upendo wake mwingi uliojaa furaha ya kichungaji katika zizi dogo umeoneshwa katika kuwakilishwa na wakristo walio kusanyika kutoka pembe za nchi nzima na kwa njia hiyo wanatoa shukrani kubwa!

Akisimulia juu ya eneo hilo, Askofu Mkuu amesema kuwa, uwanja uliotumika kuadhimisha misa Takatifu umejaa hostoria, kwani ni mahali ambapo Baba wa Taifa, Bangabandhu Sheikh Mujibur Rahman, alitoa hotuba yake tarehe 7 Machi 1971, wakati nchi ya Bangladesh inajitangazia uhuru wake. Kwa njia hiyo,  hata leo hii kwa mara ya kwanza wakristo wote wamepata kuadhimisha Ekaristi Takatifu, ili kuenzi mchango wa kumbukumbu ya eneo hilo la kihistoria na  kwa namna ya pekee ni ishara kubwa na heshima ya nafasi maalumu iliyo nayo Kanisa iliyo  katika nchi hiyo.

Halikadhalia Askofu Mkuu Rozario amesema, Papa wa kwanza kufika katika ardhi hiyo, alikuwa ni Mwenye heri Papa Paulo VI, Novemba 1970 ili kuonesha upendo wake na huruma kwa waathirika waliokumbwa na  mafuriko,  yalisababishwa vifo karibia milioni moja ya watu. Na kwa njia hiyo  hiyo Kardinali anamkubusha Papa kuwa, kama ilivyotokea kwa mtanguliz wake kufika katika tukio hilo, hata yeye amependelea kufika katika nchi hiyo ili kuonesha mshikamano wa upendo, ukaribu na ukarimu  kwa wale wahitaji.

Sr angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

 

 

01/12/2017 12:43