Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa Barani Afrika \ Maendeleo

SECAM NA COMECE kwa Pamoja waomba Viongozi kutengeneza ajira endelevu!

Mabaraza ya Maaskofu ya Afrika Mashariki (Secam) na Comece (Ulaya) wametoa wito kwa viongzo wakuu wa nchi kuhusu ajira endelevu kwa jamii katika mkutano wao 29-30 Novemba 2017 Abidjan Ivory Coast - REUTERS

30/11/2017 09:58

Maaskofu Katoliki wa Afrika ya  Afrika(SECAM) na wanachama wa Mabaraza ya Maaskofu Ulaya (COMECE), kwa pamoja wametoa wito kwa viongozi wa kisiasa Ulaya na Afrika, kutengeneza ajira endelevu kwa ajili ya kuwanusuru vijana wa Afrika wanaoteswa na umaskini, kutokana na kukosekana kwa ajira. Wto wa Maaskofu umo katika hati yao iliyotolewa na Tume ya SECAM NA Comece kwa ajili ya Mkutano wa Tano wa wanasiasa na wanadilomasia ambao hufanyika kwa lengo la kutazama kwa pamoja matatizo ya Afrika.

Maaskofu wameomba wanashiasa kushirikiana katika kutengeneza fursa za ajira na mipango mizuri ya maendeleo endelevu yenye kuheshimu pia mazingira. Aidha wameomba uwepo wa  haki na usawa katika biashara ya bidhaa na huduma,  hasa rasilimali  ambazo huchukuliwa kwa wingi kila mwaka toka Afrika. Kwa muda wa siku mbili,  29 / 30 Novemba 2017 Mji Mkuu Abidjan nchini Ivory Coast , kunafanyika Mkutano wa Tano wa Wakuu wa nchi na serikali na wawakilishi wa Kidiplomasia , kutoka Bara mbili: Afrika na Ulaya. Mkutano huu unaongozwa na Madambiu : Uwekezaji kwa Vijana kwa ajili ya Maendeleo Endelevu. Hata hivyo kuna wasiwasi wa Mada hiyo, kumezwa na hoja nyingine muhimu hasa wimbi la uhamiaji linaloendelea sasa. Wajumbe zaidi ya 5,000, toka mataifa 55 ya Ulaya na Afrika, wanahudhuria mkutano huu.

Mikutano ya awali, ilifanyika Cairo Misri 2000, Lisbon Ureno 2007, Tripoli  Libya 2010 na  Bruxelles Ubeligiji 2014..   
Maaskofu katika waraka wao wa kichungaji , wanasisitiza mkutano kuona jinsi vijana wa Afrika wanavyoathirika na mfumo mbovu wa kichinichini wa biashara ya binadamu. Hivyo wanatoa wito kwa washiriki wa mkutano,  kujikiti kwa udani zaidi  juu ya mada hii, hasa mapambanao dhidi ya biashara ya binadamu. Na wanategemea kwamba, Umoja wa Ulaya, utaweza fikia muafaka wa kutengeneza ajira na mipango endelevu kwa vijana wanaotoka nchi za Afrika. 

Uwepo wa mipango kama hiyo, inaweza kukatisha tamaa uwepo wa biashara ya binadamu. Kwa uwepo wa mipango mizuri hasa ya kufungua vivanda vidogovidogo mahalia na kilimo endelevu , kunaweza punguza  hamu ya vijana kutoka katika maeneo yao na kwenda sehemu mpya ambako wanatumaini maisha yao yanaweza badilika . Juhudi kama hizo , zinaweza pia kupunguza matukio ya maafa yanayosikika kila wa leo ktiak bahariya Mediterania, Maaskofu wameasa.  

Rais wa Bunge la Ulaya, Antonio Tajani , tarehe 22 Novemba akifungua Mkutano wa ndani wa Ulaya  mjini Bruxelles , kwa ajili ya kuweka mkakati wa Ulaya kwa Afrika, alitaja yale yanayosonga nia njema za ushirikiano kati ya Afrika na Ulaya kwamba ni pamoja na ukosefu wa nia za kweli, kisiasa na kuchumi katika kuliendeleza bara la Afrika. Ambapo Federica Mogherini ,mwenyekiti wa Tume ya Ulaya katika Masuala ya Siasa ya nje na uhusiano kati ya Afrika na Ulaya aliutaja Mkutano wa Abidjani kuw ani wito wa kuanzisha upya uhusiano kati ya Afrika na Ulaya.

Thabita J. Mhella
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

30/11/2017 09:58