2017-11-30 11:49:00

Papa:Vijana wa Myanmar wako tayari kupeleka habari njema ya Kristo!


Nikiwa nakaribia kumaliza ziara yangu katika nchi yenu nzuri ninaungana nanyi kumshukuru Mungu kwa neema nyingi tulizo pokea kwa siku hizi. Nikiwatazama ninyi vijana wa Myanmar na wote ambao wanafuatilia misa hii nje ya Kanisa Kuu ninatamani kushikirishana nanyi tafakari la Somo la kwanza linalojikita ndani ya Moyo wangu. Ni somo kutoka katika kitabu cha Mtakatiu Paulo lakini kitokanacho na maeno ya  nabii Isaya, Mtakatifu Paulo akiwalenga jumuiya changa ya wakristo wa Roma. Maneno haya yanasikika kwa mara nyingine leo hii yasemayo: Jinsi ilivyo mizuri juu ya milima Miguu yake aletaye habari njema, Yeye aitangazaye amani, Aletaye habari njema ya mambo mema, Yeye autangazaye wokovu, Auambiaye Sayuni, Mungu wako anamiliki! (Rm 10,15; taz Is 52,7).

Ni utangulizi wa mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko tarehe 30 Novemba 2017 katika Kanisa Kuu la Yangon lilipambwa vizuri kwa rangi nzuri na vijana wengi walikuwa wamevaa nguo za utamaduni wa birmania na maelfu yenye sura za kuchangamka, ndani hata  nje kwa nyimbo na sauti nzuri !
Baba Mtakatifu akiendelea na mahubiri hayo anasema, baada ya kuwasikiliza sauti zao,na nyimbo zao wakiimba, anasema, anataka kuthibitisha  kuwa njia zao ni nzuri, za kutia moyo kuwaona, kwasababu wanaelekea katika njia njema na utume  mwema wa ujana wao katika imani na katika ari zao. Hakika wao ni ni habari njema kwasababu wao ni uthabiti wa imani ya Kanisa la Yesu Kristo anayeleta habari njema,ya fura na matumaini yasiyo kuwa na mwisho. 

Wengi wanauliza swali ni jinsi gani unaweza kuzungumza juu ya habari njema wakati wangi wetu wamezingirwa na mateso. Je habari njema iko wapi wakati upo ukosefu wa haki, umaskini wa kukithiri, matattizo yanayopelekea katika giza ndani mwao. Pamoja na hayo Baba Mtakatifu anasema, anataka watu watambue kuwa vijana wote wa kike na kiume wa Myanmar hawaogopi kutangaza  habari njema ya huruma ya Mungu kwasababu habari njema  ina jina na sura, yaani ni Yesu Kristo. Yeye Kama mjumbe na habari njema vijana wako tayari kujikta katika kupeleka neno la matumaini  kwa Kanisa katika nchi yao na duniani. Wao wako tayari kupelekea habari njema kwa ndugu na kaka wanaoteseka, wenye kuhitaji maombi ya sala na mshikamano, lakini pia hata upendo kwa ajili ya haki msingi  za kibinadamu na haki  kwa ajili ya kukua kwa upendo wa Yesu anaotupatia  yaani upendo na amani.

Hata hivyo  Baba Mtakatifu kwa vijana ametoa mapendekezo kama changamoto , kutokana na kwamba katika somo la kwanza  Mtakatifu Paulo alirudia mara tatu juu ya  neno “bila”. Hivyo anaongeza kusema, ni neno dogo lakini la kukufanya ufikirie kwa mantiki ya mpango wa Mungu. Swali linalomfikia kila mmoja: je itawezekanaje kuamini bila kusikia wanasema?, je utasikiaje wanaongea bila kutangza ujumbe? Je unaweza kuwa mjumbe bila kutumwa ?
(cfr Rm 10,14-15).

Baba Mtakatifu amewaomba vijana kutafakari kwa kina juu ya maswali hayo na bila kuogopa, kwa maana Mungu anawapenda sana, ni kama Baba asiye taka kuwaacha peke yao mbele ya masawali hayo. Pamoja na hayo amewasaidia kutafakari katika mawazo ambayo yanaweza kuwasaidia kujikita katika safari yao ya imani pia katika mang’amuzi ambayo Bwana anawaalika.
Dunia yetu imejaa sauti nyingi  za kufunika hata sauti ya Mungu, Baba Mtakatifu anathibitisha, lakini pamoja na kwamba wengine wamaweza kusikiliza na kuamini Yeye, bado wanahitaji watu wa kweli, wanaotambua kusikiliza kwa kwa makini na kuwasaidia. Kwa maana hiyo anaongeza kusema kuwa, hakika wao tayari wanataka kufanya hivyo. Hivyo Bwana anaweza kuwasaidia katika kusikiliza sauti yake, kuongea naye kwa utulivu na kwa kina katika mioyo yao.

Pia ni lazima kuongea na watakatifu, marafiki wa mbingu ambao wanaweza kuwa mfano wa kuigwa, Baba Mtakatifu anaongeza kusema, kwa mfano wa Mtakatifu Andrea, ambaye Kanisa linamkubuka sikukuu yake tarehe 30 Novemba. Yeye alikuwa mvuvi rahisi, lakini akageuka kuwa mfiadini na shuhuda wa Yesu. Hata hivyo kabla ya kuwa shahidi alifanya hata yeye makosa mengi lakini pamoja na hayo alikuwa mvumilivi na kujifunza taratibu ili aweze kuwa mtume wa kweli wa Kristo. Na kwa njia hiyo Baba Mtakatifu anasisitiza kwa vijana kuwa, wasiwe na hofu ya  kujifunza kutokana na makosa kwani, watakatifu wanaweza kuwaongoza kufika kwa Yesu na kujifunza kujikabidhi maisha yao katika mikono yake. Yesu ni mwingi wa huruma na hivyo wamshirikishe kila kitu ndani ya mioyo yao kama vile hofu zao, wasiwasi wao, ndoto zao  na matumaini. Wajikite kutafakari kwa undani katika maisha ya kiroho, kuyatunza na kulinda  kama wafanyavyo watunza misitu au bustani, wakivumilia kusubiri mavuno na  ndiyo hivyo, nao wawe na uvumilivu maana Bwana atawapatia matunda mengi kwa wakati wake na matunda hayo washirikishe hata kwa wengine.

Baba Mtakatifu Francisko amemamaliza mahubiri yake akasema; kutokana na kwamba lile ni Kanisa kuu lenye jina la Mama Maria Mkingiwa wa dhambi ya asili, anawatia moyo ili watazame Maria. Yeye alipoitikia ndiyo kwa Malaika alikuwa kijana kama wao. Alikuwa jasiri wa kujikabidhi katika habari njema aliyosikia na kuweka kujikabidhi maisha ya imani kutokana na wito wake na kujikabidhi moja kwa moja kwa upendo upeo wa Mungu. Kwa njia hiyo  hata wao kama Maria wawe wanyenyekevu lakini wajasiri wa kupeleka Yesu na upendo wake kwa wengine. Mungu abariki Myanmar! Na katika lugha yao : “Myanmar pyi ko Payarthakin Kaung gi pei pa sei”.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican



 








All the contents on this site are copyrighted ©.