2017-11-30 16:18:00

Papa: Ujumbe kwa Patriaki Bartholomew katika Sikukuu ya Mt. Andrea


Katika kuadhimisha Sikukuu ya Mtakatifu Andrea, ambayo inaadhimishwa kila ifikapo tarehe 30 Novemba yak ila mwaka, Baba Mtakatifu ametuma ujube kwa Patriaki wa Kiekumeni Bartolomew.  Katika ujumbe huo Baba mtakatifu anasema, pamoja na kuwa mbali katika Ziara ya Kitume huko Myanmar na Bangladeh, anayo shahuku ya kuwatakia Heri na Baraka za Sikukuu kwa wanachama wote wa Sinodi ya Kiekumene, mapadre, wamonaki, na waamini wote waliunganika katika Liturujia Takatifu Katika Kanisa la Kipatriaki la Mtakatifu Giorge kufanya kumbukumbu ya Mtakatifu Andrea Mtume na ndugu yake Mtakatifu Petro. Mitume wa kwanza , na ambaye ni msimamizi wa kanisa la Costantinople na la Kipatriaki la kiekemuene.

Pia anamwomba awea kusali kwa ajili ya wote wanaosafairi katika barabaram, akanini na angani na kwa namna hiyo wasali kwa ajili yake.
Baba Mtakatifu anasema,mwakilishi aliyemtuma  katika sikukuu yao ni kuonesha kwa ukaribu wa mshikamani kiroho katika sala, kushukuru na kusifu Mungu Mwenyezi kwa huruma anayoitoa kwa njia ya ushuhuda wa mtume Andrea. Na wakati huohuo mwakilishi wa kipatriaki aliyekaribishwa mjini Roma mwezi Juni,mwaka huu ameonesha ukaribu wa kiroho wakati wa kuadhimisha matendo ya  Mungu na kisima cha wema kilichowezekana kwa matendo ya  watakatifu Petro na Paulo wasimamizi wa Kanisa la Roma.

Mitume wa Yesu walitangaza habari njema hadi miisho ya dunia kwa njia ya maneno na sadaka ya maisha yao, maana wao waliona, walisikia na kushuhudia uzoefu wa Neno la maisha na kuona kweli Bwana wetu Yesu Kristo aliyekufa na kufufuka kwa ajili ya wokovu wetu.
Kwa maana hiyo kutangaza habari hiyo unawezesha kuingia moja kwa moja na ushirika wa Baba kwa njia ya Mwana na Roho Mtakatifu ambaye ni msingi wa umoja ulio unganishwa kwetu kwa njia ya ubatizo na katika jina la utatu Mtakatifu.

Baba Mtakatifu anaongeza; hii ni sababu ya furaha kubwa ya kukumbuka walipokutana naye wakati wa kuadhimsha miaka 50 tangu ziara ya Papa Paulo wa VI katika Kanisa lao huko huko Phana  iliyotokea tarehe 25 Julai 196. Katika sherehe hizo za Kihistoria za umoja kati ya Wachungaji wa Kanisa la Roma na Kanisa la Constanople ni vema kukumbuka ujumbe wa maneno ya Patriaki wa Athenagoras alipokuwa akimpokea Papa Paulo VI katika Kanisa la Mtakatifu Giorge, mahali ambapo leo hii wameuganika. Baba Mtakatifu anaamini kuwa, maneno hayo yanaweza kuwa ni chachu hata leo ya mazungumzo kati ya Makanisa yote.

Patriaki huyo alisema, tukuunganishe kile kichotenganishwa, mahali ambapo inawezakana katika matendo ya wote yaani Makanisa yete mawili husika, na kutoa nguvu zaidi kuimarisha masuala ya imani, uadilifu wa sheria tulizo nazo pamoja. Tudumishe mazungumzo ya kutaalimungu kwa mujibu wa misingi ya jumuiya kamili na msingi wa imani,uhuru wa mawazo ya kitaalimungu, mahali ambapo kuna ujenzi ulioanzishwa na mwili wa Mababa na katika aina nyingi za utamadunisho mahalia kama ilivyo kuwa tangu mwanzo wa Kanisa "(Tomos Agapis, Vatican-Phanar (1958-1970)

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili 

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.