2017-11-29 16:05:00

Hotuba ya Papa kwa Baraza Kuu la Sangha:Wabudha na Wakatoliki watembee pamoja


Katika mkutano wetu ni fursa ya kurudia kwa upya na kuongeza juhudi za uhusiano wa  kirafiki na heshima kati ya wabudha na wakatoliki. Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko tarehe 29 Novemba 2017, wakati wa kutoa hotuba yake katika Baraza Kuu la Sangha la Wamonaki wa Kibudha katika Kituo cha Kaba Aye huko Yangon. Ni moja ya hekalu kubwa la kibudhaa linalojulikana sana katika Bara la Asia ya Kaskazini Mashariki.

Katika hotuba yake anasema ni fursa pia kuhakiki kwa dhati upamoja wa jitihada kwa ajili amani, heshima ya hadhi ya binadamu na haki ya kila mme na mke. Na si katika nchi ya Myanmar bali katika dunia mahali ambapo watu wanahitaji ushuhuda wa amani  hii kutoka kwa viongozi wa kidini. Baba Mtakatifu anaongeza kusema: hiyo ni kutokana na kwamba, tunapoongea kwa sauti moja kuhusu thamani msingi za haki, amani na hadhi msingi kwa kila binadamu, tunatoa neno la matumaini kwa wote. Pia ni kusaidia Wabudha,Wakatoliki na watu wote kupambana katika kutafuta  wema na mshikamano katika jumuiya nzima.
Aidha katika hotuba yake anaonesha kuwa, kila kipindi cha kibinadamu kimefanya uzoefu kuhusu kutafuta haki msingi za kuishi, katika kipindi cha migogoro na ukosefu wa usawa kati ya watu. Na katika kipindi chetu anasema, utafikiri matatizo yamekuwa ni makubwa zaidi. Hata hivyo anaongeza kusema kuwa, hata kama inaonesha kuwa  jamii imepiga  hatua kubwa ya maendeleo ya kiteknolojia, na watu wa dunia hii wanazidi kuwa na utambuzi zaidi juu ya kibinadamu, yaani kuwa na utambuzi hata wa hatima yake, ambayo inaweza kuwa na majeraha ya migogoro, umaskini na kusongwa, ambavyo ni matokeo yanayosababishwa na  migawanyiko mipya.

Mbele ya changamoto hizi, ni lazima kutojiachia, kwa njia hiyo Baba Mtakatifu anatoa wito kwa wabudha kwamba wawe mstari wa mbele katika  misingi inayoongoza kila utamaduni wa tasaufi, kwa maana ndani yake  upo utambuzi wa kwamba, kuna njia za kwenda mbele, njia ambazo zinapelekea uponyaji, uelewa wa kina na katika kuheshimu. Na njia ya utambuzi huo ni upendo wa dhati.

Ni upendo wa dhati  ambao unapelekea hatua za kuwa na  amani, usalama na matarajio mema ya  wote . Katika juhudi hizi zinaweza kuleta matunda ya kudumu, lakini yanayohitaji ushirikiano wa pamoja na ujasiri kati ya viongozi wa kidini. Kutokana na hilo, Baba Mtakatifu anawaakikishia wamonaki wa kibudha , kwamba Kanisa Katoliki litatembea bega kwa bega kama mshiriki wa dhati kwa mtazamo huo wa kuongozwa na haki ya kweli na  amani ya kudumu ambayo inamsaidia kutazama upeo wa kila mmoja katika dunia hii.

Baba Mtakatifu akitazama na kutafakari  tasaufi ya Budha,  amesema, kwa njia ya mafundisho ya Budha shuhuda yakinifu kwa wamoki wengi wa kike na kiume na watu wa nchi hiyo wamejikita kikamilifu kuunda thamani ya uvumilivu, kupokea, heshima ya maisha na kama vile tasaufi makini ya kuheshimu kwa kina mazingira asili. Thamani hizi msingi kwa ajili ya maendeleo ya jamii kuanzia kwa aliye mdogo ni muhimu katika umoja wa jumuiya, ndani ya  familia, na katika kupanuka hadi kufikia kutengeneza  mtandao wa mahusiano ambayo yanasukuma kuunganika kabisa  na mahusiano msingi, ili utande katika utamaduni, makabila, mila na desturi za taifa, lakini hawali ya yote ni misingi hiyo ijikite katika umoja wa kibinadamu.

Na katika utamaduni wa kweli wa makutano, thamani hizi zinaweza kusaidia kuongeza nguvu katika jumuia zote na kusaidia kupeleka mwanga ambao ni muhimu katika ujenzi wa jamii nzima. Wabudha na wakatoliki kwa pamoja lazima kutembea  njia moja kwa ajili ya wema wa wote katika ardhi hiyo. Na ndiyo matashi mema ya Baba Mtakatifu aliyowatakiwa katika kutembe kwa pamoja na kupanda mbegu ya amani na kuponyesha, uwelewa na matumaini katika nchi hiyo.

Sr Angela Rwezaula 
idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.