Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Vatican \ Hotuba

Siku ya Amani duniani:Utekelezaji wa Mikataba kwa wahamiaji ni muhimu!

Wema wa wakimbizi na wahamiaji ni sawasawa na wema wa jumuiya inayowapokea pia ni haki na wajibu wa mahitaji kwa maisha endelevu. - ANSA

28/11/2017 15:29

Katika ujumbe wa Siku ya Amani duniani wa tarehe MosiJanuari  2018 , Papa anawaalika wote kutokuwa na hofu dhidi ya wahamiaji kwasababu za kisiasa, pia si kuwasukumiza wakimbizi na wahamiaji kwenda katika maeneo ambayo yanawasubiri kuteswa na migogoro. Hayo ni maneno ya Askofu Mkuu Silivan Maria Tomasi wa Baraza la kipapa la Huduma endelevu ya Binadamu akitoa ufafanuzi wa Ujumbe wa Baba Mtakatifu kwa Siku ya Amani duniani 2018. 

Askofu Mkuu anasema ni lazima kuwa na busara kwasasababu ya mikataba ambayo imetiwa sahini kuhusu nchi za  Afrika ya Kaskazini, nchi za Mashariki na nyingine ambazo zinahusishwa katika kuotoa au kuombwa makazi ya wakimbizi na wahamiaji kwa  kuzuia wimbi kuelekea Ulaya. Wakati huohuo ni nchi mbazo ziko hatari ya kusahau haki msingi za kibanadamu. 

Hiyo inajithibitisha wazi katika ukiukwaji wa haki hizo kwenye makambi mahali ambapo wakimbizi na wahamiaji wamepakiwa kama mizigo. Askofu Mkuu Silvan Maria Tomasi, akisisitiza zaidi anasema, ni lazima kuwa makini hasa katika kuleta uwiano sawa kati ya wahamiaji na wema wa jumuiya zinazowapokea, lakini pia si kufunga macho na mioyo mbele ya hali halisi ya wakati wa sasa.  Katika ujumbe wa Baba Mtakatifu Kuna suala linalo pinga tabia zilizosambaa za Sera za kisiasa na kwamba  sera hizo zinapanda mbegu za vurugu, ubaguzi wa rangi na mambo yatokanayo na hiyo, kwa maana hiyo  anawaalika viongozi wa nchi kuthibiti kwa njia suala hilo kwa njia  ya matendo mema ya kuwapokea na kuwasaidia waweze kushirikishwa haki msingi za kibinadamu. 

Hiyo inatokana na kwamba   miaka ya hivi karibuni kati ya 5 na 6 kumekuwapo na wimbi kubwa kwa wanaoingia au kutoka, wakati huohuo wanaoomba makazi na wahamiaji wengine wanaoingia kwa sababu nyingine nyingi zikiwemo za kiuchumi na kisiasa,umaskini,majanga ya kiasili hivyo kusababisha  ongezeko la hofu kubwa kwa nchi zinazowapokea. Pamoja na hiyo Askofu anaongeza kusema, haiwezekani kudharau hofu ya watu, la muhimu ni lazima kujikita kwa makini kuwapatia jibu la ukweli na la kiakili.  Ni lazima kuongozwa na mantiki ya wema katika matukio hayo na imani kuu.

Na zaidi kuunda tabia ya uwelewa halisi wa kile kinachotokea hasa kwa upande wa mchakato wa wahamiaji. Hiyo ni kuelimisha umma kutambua sababu msingi zinaziwafanya wakimbie nchi zao,kwani pamoja na hali za majanga ya asili yasiyozuilika  bado hata ukosefu wa hadhi ya kuishi kama binadamu, au kutafuta maisha bora yanayostahili, ambayo yanajali uhuru wa mtu kujieleza badala ya kukandamizwa, halikadhalika ulazima wa kuwahusisha nchi zote na familia ya kibinadamu .

Katika sababu hizo ni wazi tukiongozwa na Imani na hali ya kibadamu tunaweza kuonesha mshikamano kwa watu hawa ambao ni ndugu zetu, wanaohitaji kuthaminiwa na kutambua haki zao. Wema wa wakimbizi na wahamiaji ni sawasawa na wema wa jumuiya inayowapokea, pia ni haki na wajibu wa mahitaji kwa maisha endelevu.  Iwapo Papa anawaalika viongozi wa nchi kutafuta njia wazi na mikakati madhubuti ya matendo,ni hakika  kwamba viongozi hawa wajihusishe zaidi juu ya mikataba waliyoweka kwa mfano nchi ya Italia na Libia pamoja na zile za siasa ya Ulaya juu ya wahamiaji.

Aidha katika ujumbe  wa amani, Baba Mtakatifu anawaalika wawe na mtazamo wa kutafakari kwa kina juu ya wahamiaji na wakimbizi. Kwa kufafanua hilo anasema kuwa, ina maana ya kuwa na huruma na uwelewa wa kina, kwa maana haiwezekani kabisa kutazama matukio ya wahamiaji kwa mtazamo mmoja tu hasa  kuhusu ulinzi na usalama, bila kufikiria  usalama kwa wale wahitaji na kuwasaidia ili waweze kuishi kwa amani na hadhi ya kibinadamu.  Ni muhimu kuwajibika katika suala hili, hasa maelekezo na  kuelezwa zaidi hali halisi ya wahamiaji kwani inaweza   kutoa mchango wa dhati , na wakati huo huo kutambua vizingiti katika uwezo wa kuwapokea.

Baba Mtakatifu katika ujumbe wake wa amani pia anayo matumani kuwa mikataba miwili  iliyokubaliwa na Umoja wa mataifa juu ya wahamiaji na wakimbzi pia inayowahusisha hata Kanisa lote katika mchakato mzima inaweza kuwa chombo madhubuti kufikia utekelezaji kamili. Vatican kwa njia ya mitandao ya kidiplomasia daima wanajihusisha kwa dhati katika mazungumzo na majadiliano ya mikataba hiyo. Siyo mikataba ya kulazimisha, bali ni kama kitovu cha ujenzi wa sera kisiasa za kimataifa kwa pande zote za nchi washiriki walioandaa  mikataba hii.

Ni muhimu  kwamba sauti ya Papa ya moja kwa moja katika hali halisi ipate mwangwi na kusikilizwana mabaraza yote ya maaskofu duniani, Taasisi za kujitolea Katoliki wanaojihusiasha katika makambi ya wakimbizi na sekta mbalimbali mikataba hii kwa namna ya heshima ya haki msingi ya watu, kwa namna ya pekee wanaoomba makazi na wahamiaji, ili waweze kushiriki maisha ya umana kwa mujibu wa uwezo wao  na wao na kutoa  mchango  unaopaswa kutambuliwa na kuwa kweli sehemu ya jamii wanapoishi.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

28/11/2017 15:29