2017-11-28 12:45:00

Papa amekutana na Rais wa Myanmar na Aung San Suu Kyi


Tarehe 28 Novemba 2017 mchana, Baba Mtakatifu akiwa katika mji mkuu wa Nay Pyi Taw amepokelewa na Rais wa nchi, Bwana Htin Kyaw katika ukumbi  wa Rais. Wawakilishi wa Vatican na wa Birmania walikuwa wamemzunguka nyuma yao katika nyumba iliyopambwa vizuri.  Baba Mtakatifu na Rais wa nchi kabla ya kuongozana kuingia katika nyumba ya Rais, kwanza wamesimama jukwaani na kusikiliza nyimbo mbili  za kitaifa, zilizoongozwa na bendi ya kijeshi. Baada ya kusikiliza nyimbo hizo, walitembea kwenda katika nyumba kubwa yenye nafasi kubwa kwa kupitia katika ngazi iliyotandazwa na zulia nyekundu.

Katika nyumba ya kifahari iliyopambwa vizuri, Baba Mtakatifu kwanza amefikia katika ukumbi wa kwanza ambapo amekaa kwenye kiti kutia sahini katika kitabu cha wageni akiwa karibu na Rais wa nchi ya Myanmar. Baadaye wameongozana kwenda katika ukumbi mwingine uliopambwa na Bendera mbili za Taifa la Mynamar na Vatican kwa ajili ya kupigwa picha ya pamoja. Baadaye imefuata mazungumzo ya faragha katika ofisi ya Rais Htin Kyaw, pia na katika ofisi ya  Aung San Suu Kyi.

Taarifa zinasema kuwa kwa upande wa kiongozi wa Birmania, Aung San Suu Kyi, anathibitisha kuwa mkutano na Baba Mtakatifu ulikuwa ni kurudia kusisitiza juu ya imani katika uwezo na uwezekano wa amani katika nchi. Pia wamezungumza juu ya kipeo cha Rakhine (mahali ambapo wanaishi waislam wa Rohingya), pia kuhusiana  na marafiki  wema katika uwezo wao wa kujikita katika jitihada za  kusaidia kupata amani ambayo ina thamani isiyohesabika. Aidha kiongozi Aung San Suu Kyi anasema, lengo muhimu ni kupeleka mbele mchakato wa amani unaojikita juu makubaliano ya kusitisha moto wa vita kwa ngazi ya kitaifa iliyotokea katika serikali iliyopita.

Aidha anasema kuwa,mchakato wa amani siyo rahisi , lakini huo ndiyo mtindo mmoja ambao unaweza kupelekea watu wake ishara moja ya haki, ya kweli katika ardhi na kuwa matarajio ya kimbilio lao, shahuku yao na furaha yao. Jitihada za kutafuta amani ndiyo muhimu katika kuongeza juhudi zaidi ili kuweza kufikia maendeleo endelevu na ule uhakika wa kizazi endelevu.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.