2017-11-27 16:18:00

Kard.Parolini:Ubatizo,kipaimara na komunio ni viunganishi katika ukombozi


Ninayo furaha kubwa ya kuadhimisha misa ya kuhitimisha Tamasha la Mafundisho Jamii ya Kanisa na ninawashukuru kwa mwaliko huu. Kwa wote ninawafikishia baraka kutoka kwa Papa Francisko ambapo  ni fursa pia ya kuwaomba kwa  namna ya  pekee kumsindikiza katika sala kwa ajili ya ziara yake ya kitume nchini Myanmar na Bangaladesh inayoanza usiku wa leo.

Ni maneno ya utangulizi wake Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican Jumapili tarehe 26 Novemba 2017 huko Verona katika kuadhimisha Misa Takatifu ya kuhitimisha Tamasha la Mafundisho Jamii ya Kanisa Katoliki. Akiendelea na tafakari la Maadhimisho ya siku ambapo ilikuwa ni  sikukuu ya Kristo Mfalme amesema, hii ni kuadhimisha ukombozi na kurudia kutazama mambo yote ya dunia, hata mbinguni kwa upande wa Bwana wetu Yesu Kristo aliyekufa na kufufuka kwa ajili yetu . (Ef 1,10).

Ubatizo, kipaimana na komunio ni mambo yanayo unganisha waamini wote katika kazi ya ukombozi duniani. Na kwa namna hiyo tunaalikwa kuishi kwa imani katika utume wa kubadilika kwa kila hali zote za maisha ya hapa duniani kuanzia familia, shuleni, kazini makampuni , uchumi, utamaduni na kisiasa. Zawadi ya Roho Mkatifu inawezesha kuwa mstari wa mbele katika ubinadamu mpya wa kushirikishana na kufunguliwa kizazi kipya, hata kwa kuishi  pamoja katika ulimwengu huu tukiwa na uwezo wa kukua kiukweli na wema. Kama isemavyo Waraka wa Mwanga wa Mataifa “ hakuna kilicho kizuri zaidi ndani ya moyo wa binadamu ambacho hakikosi kuwa na mwangwi katika moyo wa mitume wa Yesu Kristo.

Waamini wanaoishi na muungano wa Kristo aliyefanyika mwili na kiongozi wa watu anayetembea katika mbingu mpya na nchi mpya anaalikwa kutambua ukubwa wa dhamiri ya kijamii na ile ya imani kama anavyoelekeza Baba Mtakatifu Francisko katika waraka wale wa Evangelii Gaudium  Furaha ya Injili. Mwaamini wa kweli hawezi kamwe kuacha sababu za kina kujikita katika utume wa umisinaonari kwa kila hali ya dunia. Na hivyo anaalikwa kuishi nyuzi 360 katika kutimiza upendo wa ukweli, kwa kila iaina ya shughuli za uhusiano binafsi hadi katika masuala ya kifedha ,kiuchumi  na hata kijamii na kisiasa,ikiwa ni pamoja na familia ya kibidamu, katika mawasiliano na utamaduni.

Upendo wa Kristo unapaswa kushuhudiwa katika kulinda maisha mapya yanayozaliwa na katuka maisha yanazimika, waliobaguliwa na jamii na maskini wote ili kuunda kwa upa uchumi wa dhati kwa ngazi ya kidunia. Waamini wote na hata binafsi, kama vile vyama, ni lazima kuelimishwa juu ya kukaribisha, kuadhimisha na kushuhudia maisha ya Kristo katika ulimwengu ambao daima unazidi kuongezeka utandawazi. Kwao lazima kujikita kwa undani zaidi katika kupanda mbegu ya uhuru wa kindugu, mshikamano  na haki ya kijamii. Imani ni kama alivyosema Baba Mtakatifu kuwa, ni lazima kuishi kwa dhati, katika utambuzi wa ndugu wakati wate, yaani kama kufanyika mwili kwa kila mmoja,(Injili ya Furaha.

Akitafakari juu ya Injili ya Siku, anathibitisha yale maneno ya Yesu yasemayo kila mlipomfanyia mmojawapo wa wale walio wadogo, mlinifanyia mimi (Mt 25,40-45).Hiyo ni kuonesha kuwa kila tufanyacho kwa wale wenye kuhitaji, ukuu wa Mungu unajionesha kwetu nahata katuka matokeo mema ya kuwa na mahusiano kibinadamu, wakati huo huo ni kufungua njia kubwa ya mwisho yenye kuleta maana  hasa ile ya kufahamu ukweli wa hatima yetu.

Maadhimisho ya ekaristi yanasaidie kutambua na kuwa wawakilishi wa kweli na wakuu katika mawazo yetu na mipango yetu iweze kupata msingi katika elimu ya mtu na maadili kwa namna ya pekee ya ukamilisho wa upeo mpya wa uumbaji.
Tumshukuru Mungu anaye fanya mambo yote kuwa mapya katika safari na kusindikizwa na nguvu ya roho Mtakatifu ili kuweza kushikamana kama jumuiya moja ya kikristo katika ujenzi waUfalme, ambao ni Ufalme wa kweli ,haki , uhuru, upendo , utakatifu , neema, amani hadi Mungu atakupokuwa Mungu wa wote. ” (1kor. 15,28). Hata hivyo Ujumbe wa Baba Mtakatifu kwa njia ya Video uliotolewa wakati wa ufunguzi wa Tamasha hilo umewasaidia wajumbe wote katika mafundisho mema na msingi ya kijamii hasa kwa namna ya pekee kipengele cha IV cha waraka wa Furaha ya upendo.

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.