2017-11-26 14:18:00

Papa:Tutahukumiwa siku ya mwisho kulingana na matendo yetu kwa jirani!


Katika Domenika ya mwisho ya Liturujia ya mwaka tunaadhimisha Sikukuu ya Kristo  Mfalme wa Ulimwengu. Ufalme wake  upo katika kuongoza na kutoa huduma, hivyo ufalme  wake utaoneshwa  nyakati za mwisho akihumu. Ni maneno yaliyomo katika mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko wakati wa sala ya malaika wa Bwana Jumapili 26 Novemba 2017 wakati Mama Kanisa akiadhimisha Sikukuu ya Kristo Mfalme wa Mataifa. Baba Mtaatifu anaendelea katika mahubiri yake: Sura ya Injili inafunguliwa na upeo mkubwa ikionesha kwamba,Yesu anaweleza mitume wake, “hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake" (Mt 25,31).

Na  huu ni utangulizi  wa hakika wa kusimulia historia ya  hukumu ya ulimwengu. Baada ya kuishi katika maisha ya dunia hii kwa unyenyekevu na umaskini, Yesu anaonesha sasa utukufu wa Mungu , mahali ambapo yeye mwenyewe anatokea, akizungukwa na kundi  kubwa la malaika. Binadamu wote wamealikwa mbele yake  ili yeye aweze kutimiza madaraka yake juu yao , kwa kuwabagua  wengine kati yao,kama vile mchungaji abaguavyo  kondoo na mbuzi.

Akifafanua zaidi juu ya kubagua anasema; wale wa mkono wa kuume atawambia njooni enyi mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu, kwa maana nalikuwa na njaa mkanipa chakula, nilikuwa na kiu mkaninywesha,  mgeni  mkanikaribisha, uchi mkanivisha,mgonjwa mkanitazama, mfungwa mkanitembelea.... Ndipo wenye haki watashangaa kwa maana hawakumbuki kama walikutana na Yesu na hata kama waliweza kutoa msaada wa namna hiyo. Lakini yeye atawambia, Amin nawambia kadiri mlivyowatendea mmojawapo wa hao ndugu zangi walio wadogo , mlinitendea mimi. 

Baba Mtakatifu anasema, neno hili haliachi kamwe kutoa mshangaona kuoenesha bayana upendo upeo wa Mungu ambaye anadiriki kujifananisha na sisi na siyo tu tunapokuwa vizuri, wenye afya na furaha, bali hata tunapokuwa wahitaji. Mtindo huo wa kujificha namna hiyo ndiyo unafanya kukutana na Yeye ,kwa maana yeye ni kama omba omba njiani. Yesu anakionesha kwa mantiki msingi juu ya hukumu yake ya mwisho ambayo itatazama kwa dhati kuhusu  matendo ya ukaribu na  ujirani katika matatizo. Na ndiyo anajionesha katika upendo na ufalmea wa Mungu. Ni lazima kuwa na mshikamano kwa anaye teseka  na kwa kila sehemu kwa njia ya matendo ya huruma, anathibitisha Baba Mtakatifu!

Katika hukumu, ya mwisho inaonesha alivyo wafukuza wale ambao katika maisha yao hawakujihangaisha na mahitaji ya ndugu. Hata hao pia Injili inaonesha jinsi gani walibaki na mshangao na kuuliza lini walimwona na njaa,  hana nguo, mgonjwa, au mfungua na hawakuweza kumhudumia. Baba Mtakatifu anongeza ,wao wanafikiri kama wangemuona kwa hakika wangefanya hivyo, lakini Yesu anawapa jibu kuwa, kile ambacho hakufanya kwa wale walio wadogo, hawakumsadia Yeye. Hivyo Baba Mtakatifu anathibitisha kuwa mwisho wa maisha yetu tutahukumwa juu ya upendo wa dhati na juu ya kupenda na kuhudumia Yesu katika  ndugu zake hasa wadogo na wenye shida.  Yesu atakuja siku za mwisho kuhukumu mataifa yote, lakini wakati huo huo anakuja kila siku na kwa njia nyingi, hivyo anaomba tumpokee! 

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.