2017-11-26 11:22:00

Papa:Kazi iwe ni kwa ajili ya binadamu kwa maana mtu ni kitovu cha maisha!


Kazi lazima ielekezwe kwa njia ya mfano wa maendeleo endelevu ambayo inajikitia katika mshikamano wa binadamu wote wa dunia hii. Hayo ndiyo maneno Baba Mtakatifu Francisko katika barua yake aliyomtumia Kardinali Peter Turkson Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la huduma endelevu ya Binadamu katika tukio la Mkutano wa Kimataifa ulio andaliwa na Baraza hilo.

Mkutano ulionza 23 na kumalizika 24 Novemba jioni mjini Vatican wenye mada: kutoka Populorum Progressio kwenda  Laudato si’ “maana yake  kutoka katika Waraka wa Kitume wa Mwenye heri Paulo VI, juu ya “maendeleo ya watu” kwenda katika  Waraka wa Kitume wa Papa Francisko kuhusu ulinzi wa Mazingira nyumba yetu”. Mzunguko wa kazi ya wafanyakazi katika msingi wa maendeleo kamili ya binadamu, uendelevu na mshikamano. Lengo likiwa kwamba ulimwengu wa kazi uweze kuendelea kuwa ufunguo wa maendele katika sayari.

Baba Mtakatifu anasema, utume huo ni  kufuata nyayo za Yesu kwa njia ya kazi, kwa maana kazi ni ufunguo wa masuala ya kijamii na urahisi kwa ajili ya maendeleo kitasufi. Yesu ambaye alitumia muda wake wote katika maisha yake hapa dunia akifanya kazi kwa mikono akiwa seremala, anatualikwa kufuata nyanyo zake. Kwa maana hiyo, kila mfanyakazi ni mkono wa Kristo anaye endelea kutengeneza na kutenda yaliyo mema.
Kazi muhimu inayomfanya mtu achanue, ni ufunguo wa maendeleo ya kijamii, na kwa njia hiyo binadamu siyo biashara nasiyo zana katika mnyororo wa utengenezaji. Ni lazima maadili yatumuika katika kutea nafasi ya ajiri na kuunda hata nafasi mpya za kazi. Na zaidi ya hayo yupo binadamu kwanza  kama kitovu na siyo tu kazi.

Mahitaji mengine Baba Mtaktifu anasisitiza kuwa ni familia, rafiki na mapumziko. Kazi ni lazima iwe kwa ajili ya huduma ya binadamu. lakini iwapo inasimamia juu ya mantiki ya zana za mtu, na pia iwapo kazi hiyo inaharibu mazingira au kupelekea faida kwa badhi ya watu binafsi, mfano wa maendeleo ya uchumi hujitokeza kilio, hasa maskini wanaoishi chini ya Ardhi hii. Kwa maana hiyo lazima mambo haya yaende sambamba kati ya kazi, nyumba na ardhi . Pamoja na hayo bado kuna mambo matatu uhimu ya kuzingatia ambayo ni ya kuleta maendeleo ya kiuchumi kwamba  ni kati ya  kazi, muda na teknolojia.

Lakini pamoja na hizo teknolojia bado kuna hasa zinatojitokeza katika mawazo bila kujali kuwa  kuna uharibifu wa kijamii na mazingira. Na kwamba haijalishi kinachokitumika na nini kinakosa. Wanachozingatia ni kuingiza faida ya papo kwa papo na kila kitu wanaona ni haki kwa kile wakiitacho Mungu wa fedha. Leo hii anasema upo  mchezo wa kuchezea  heshima ya kazi ya kila mtu. Wafanyakazi katika mapambano ya kutetea haki zao, wamejifunza kukabiliana na mantiki ya kinachofaa, au kwa maana nyingine tunaweza ya kutumia kile kilichobaguliwa.  

Pia anasisitizia suala la  mazungumzo juu ya maendeleo, kwani anasema, sauti zote na utekelezaji wa upeo ni muhimu kwa wale ambao hawana  sauti na wale waishio pembezoni. Inahitajika watu wafanye kazi bila kuchoka ili waweze kutoa maisha katika mchakato wa ngazi zote. Ili mchakato uweze kuleta ufanisi, lazima kuanzia na kile tulicho nacho na kinatuunganisha kwa dunia nzima hasa kukazia mshikamano kwa watu wote duniani wa leo,hata wa kesho.
Ametoa wito wa kutafuta njia ya kuondokana na uchumi wa masoko na uwekezaji, ili kuwaongoza katika mitindo ya kazi ya kibinadamu ambayo ni kitovu Na kwa njia hiyo watetezi wote na vyama vya wafanyakazi kama utume ni lazima wawe watalaam wa mshikamano. Inahitaji miongozo thabiti ya matendo kuanzia upeo wa wafanyakazi ambao utawapeleka katika maendeleo kamili ya binadamu na endelevu.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya kiswahili ya radio Vatican
 
 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.