2017-11-26 14:26:00

Papa ameombwa kusindikizwa kwa sala katika ziara ya kitume barani Asia


Mara baada ya mahubiri  yake,Baba Mtakatifu amesema juu ya kupokea habari za kusikitisha kufuatia mashambulizi ya kigaidi huko kaskazini ya Sinai nchini Misri. Na kwa njia hiyo anaendelea kusali kwa ajili ya waathirika, majeruhi na kwa jumuiya nzima kutokana na janga hili. Mungu awaokoe na majanga haya  na kuwapa nuvu zaidi wale  wanaoendelea kujikita katika kutafuta amani, mapatano na kuishi kwa pamoja. Kutokana na kwamba watu hao walikuwa wakisali, Baba Mtakatifu ameomba kukaa kimya na kusali kwa ajili yao. …..

Aidha amekumbuka kuwa huko Córdoba nchiniArgentina,  alitangazwa mwenye heri Mama  Catalina de María Rodríguez, Mwanzilishi wa Shirika la Hermanas Esclavas del Corazón de Jesús, Shirika la kwanza la kike katika maisha ya kitume nchini Argentina kwenye Karne ya 19. Baba Mtakatifu anasema, Mama Catalina alikuwa ameolea lakini akabaki mjane na kujiweka wakfu kwa Mungu kwa kujitoa kiroho na mali zake zote kuwasaidia wanawake maskini na waathirika. Sifa kwa Bwana kutokana na mwanamke huyo mwenye moyo kama wa Yes na  ubinadamu amethibitisha Baba Mtakatifu.

Ziara ya Kitume nchini Myanmar na Bangladesh: Halikadhalika amewakumbusha  wahujaji wote waliofika viwanja vya Mtakatifu Petro kusali kwa ajili yake  kutokana na kuanza Jioni safari ya ziara ya Kitume katika nchi ya  Myanmar na Bangladesh. Wamsindikize katika sala ili uwepo wake kwa watu hao uwe ishara ya ukaribu na matumaini

Papa amesali katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria kwa ajili ya Ziara yake barani Asia

Hata hivyo kama kawaida ya utamaduni wake kabla ya kuanza ziara yake ya kitume, jioni ya tarehe 25 Novemba 2017, Baba Mtakatifu alikwenda katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria mjini Roma kusali kwa ajili ya ziara yake nchini Myanmar ana Bangladesh. Ni ziara Ziara yake katika nchi mbili ambayo inaongozwa na kauli mbiu “Upendo na Amani” na “Maelewano na amani”.

Sr Angela Rwezaula
 Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.