2017-11-25 09:15:00

Papa:Ujumbe wa Siku ya Amani Duniani 2018:Tutazame wahamiaji kwa imani


Kuwatazama wahamiaji  katika sayari hii kwa mtazamo uliojaa imani na  kuwafikiria kuwa si tishio bali ni fursa ya kujenga wakati ujao wa amani na kwasababu ya kuendeleza wakati wetu endelevu. Hayo ni maneno yaliyomo katika Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko kwa Siku ya Amani  Duniani kwa Mwaka 2018 ulitolewa Ijumaa 24 Novemba 2017. Ujumbe wa Amani wenye kauli mbiu Wahamiaji na Wakimbizi : waume kwa wake katika kutafuta amani” ni ujumbe unaokwenda sambamba na ule wa Siku ya wahamiaji na wakimbizi mwaka 2018. Katika ujumbe wa amani 2018 ni mkakati unajikita katika vipengele vya maneno manne ya mafundisho jamii ya Kanisa yaani kukaribisha , kulinda, kuhamasisha na kushirikisha wahamiaji na wakimbizi.

Baba Mtakatifu Francisko anaandika; kila mgeni anaye bisha hodi katika milango yetu, ni fursa ya kukutana na Yesu Kristo, ambaye anajifananisha na mgeni wa  kukaribishwa au kukataliwa kila nyakati (Mt 25,35.43). Bwana anawakabidhi upendo wa umama wa Kanisa kila binadamu yoyote anayelazimika kuacha nchi yake akitafuta maisha bora ya baadaye. Wito huo unapaswa kujieleza kwa dhati kila hatua ya uzoefu wa wahamiaji kwa maana ya kuanzia safari  hadi kufika na kurudi tena. Ni uwajibu mkubwa ambao Kanisa linataka kushirikisha wote, kwa waamini  yaani  wake kwa waume wenye mapenzi mema ambao wameitwa kujibu kwa upendo, hekima, mtazamo mwema na kila mmoja kadiri ya uwezo wa kila mmoja.

Katika ujumbe huo Baba Mtakatifu anakumbuka zaidi ya milioni 250 ya wahamiaji katika dunia na kati yao  milioni 22 na nusu ni wakimbizi. Hawa anasema, wanatafuta mahali pa kuishi kwa amani na kati yao anaongeza, wako radhi kuhatarisha maisha yao katika safari ndefu ya hatari yenye kukumbana na matatizo makubwa kupoteza maisha yao, hata kukumbana na kuta za kuwazuia waisiingie mahali wanapotarajia. 
Ujumbe unatoa wito wa kuwa na mtazamo wa huruma , kwa maana nasema ili kuweza kumkaribisha mwingine inahitaji kazi ya dhati, mshikamo na umakini, wakati huo huo kuwa na utambuzi na utelelezaji wa dhati kwa hali ngumu wanayokabiliwa nayo. Na kwa njia hiyo anawaalika viongozi wa nchi kuwa na karama ya hekima  ili kuweza kuingilia kati suala hili hasa katika njia za uendeshaji ambao unahitajika kuwaunganisha watu hawa katika jumuiya zao kwa kuhakikishia haki zao na maendeleo ya pamoja. 

Katika ujumbe pia anamtaja Matakatifu Yohane Paulo II na hata Baba Mtakatifu Mstaafu, ambao wamekuwa wakisitiza juu ya jilo kwa maana anasemama maa baada ya  majanga yaliyotokea ya karne  ya XXI  hata sasa kumekuwa na ongezeko la migogoro zaidi ya silaha na aina mbalimbali za vurugu, zikisababisha matatizo mengi ya kuhamahama kwa watu ndani ya nchi au zaidi. Lakini pia wengine wanahama kutokana na kuwajongelea ndugu na jamaa zao kwa ajili ya kufatufa maisha bora maana ni matoke ya ukosefu wa ajira na majanga ya asili.

Katika  ujumbe Baba Mtakatifu bado anaonesha jinsi gani nchi ambazo wahamiaji na wakimbizi wanaelekea, kuendelea kuzuka hatari ukosefu wa usalama wa nchi au ukosefu wa kupokea wageni  kwa kudharau hadhi ya binadamu; Anasema ipo hofu nyingi dhidi ya wahamiaji na hata kwa wanasiasa, badala ya kujenga amani, wao wanakuwa wakwanza kuchochea vurugu na ubaguzi wa rangi ambacho ni kisima kikubwa cha wasiwasi kwa wale wanaojikita kwa moyo wa dhati kutetea na kulinda kila aitwaye binadamu. 

Hekima na  imani vinatufanya tutambue kuwa wote tunashiriki katika familia moja ya kibinadamu, ikiongozwa hata kujikita ndani ya miji na  mahali ambapo kuna migawanyiko na  migogoro inayosababishwa na uwepo wa hali halisi ya wahamiaji na wakimbizi, ili kuweza kugeuka kuwa mantiki ya amani. Kwa njia hiyo ni wazi kwamba inawezekana kugundua kuwa wahamiaji  hawafiki wakiwa mikono mitupu: wao wanafika wakiwa wameja ujasiri, uwezo, nguvu na ari; na  zaidi wamejaa tunu na thamani za utamaduni wao.

Kutokana na thamani walizo nazo utajirisha maisha ya nchi inayowapokea. Na tunaweza kugundua wakati huo huo,ubunifu, wema na roho ya sadaka ya watu, familia na jumuia ambazo zinafungua milango na moyo kwa wahamiaji na wakimbizi ambao wamekimbia kutokana na uhaba wa mali  muhimu za kuwaendeleza. Mtazamo wa kutafakari  kwa kina unasaidia kuongoza mang'amuzi ya wahusika katika mambo ya umma, ili kutoa msukumo kwa wote katika familia moja ya binadamu na wema wa kila mmoja anayeishi ndani yake. Ni uhakika kwamba kwa yeyote anayejikita katika mtazamo huo atakuwa na uwezo wa kutambua vichupukizi vya amani ambayo tayari umeanza kuota, ili iweze kukua.

Mapendekezo ya mchakato mrefu wa amani  2018 utaweza kufikia hata Umoja wa Mataifa katika kielelezo cha kukubaliwa kwa mikataba miwili, mmoja ukiwa wa usalama wa wakimbizi, wenye sheria na mamlaka , mwingine unaotazama wakimbizi katika ujenzi na mapendekezo ya kisiasa na michakato yake. Kwa njia hiyo Papa anakumbusha mchango wa kipengele cha wahamiaji na wakimbizi unaotolewa na  Baraza la Kipapa kwa ajili ya Huduma endelevu ya  binadamu  ambao unapendekeza matendo 20 ya kutekeleza kama ishara na matendo kamili ya Kanisa Katoliki.
”Ni mategemeo kuwa, mikataba hiyo inaweza kupokelelewa ikadumu kwa muda mrefu na ujasiri kwa namna ya kupokea na kutekeleza kila aina ya fursa ili kuweza kujenga amani. Kwa namna hiyo ulazima wa ukweli wa kimataifa hautakuwa tu kutojali na katika kubaki kwenye utandawazi wa sintofahamu badala yake kujikita kwa dhati katika utekelezaji wa suala hili msingi kwa wajili ya binadamu katika mateso.

Mazungumzo ni muhimu na wajibu wa jumuiya zote za dunia hata nchi zile ambazo siyomaskini zinaweza kupokea idadi ya wakimbzi katika hali ya wema , iwapo ushirikiano wa kimataifa unahakikishia wao uwezekano wa mtaji wa lazima. Ujumbe wa Papa unaonesha kuwa uliandikwa tarehe 13 Novemba 2017 mahali ambapo Jumuia nyingi za Kanisa Katoliki linaadhimisha kumbukumbu ya Mtakatifu Francesca Cabrini ambaye ni msimamizi wa wahamiaji ambaye mwaka huu ni miaka 100 tangu kifo chake.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.