2017-11-24 09:53:00

Papa:Ujumbe kwa washiriki wa Tamasha la 7 la Mafundisho Jamii ya Kanisa,Verona


Baba Mtakatifu ametuma ujumbe kwa njia ya Video kwa washiriki wa Tamasha la saba  la Mafundisho Jamii ya Kanisa huko Verona nchini Italia yanayo anza tarehe 23 -26 Novemba 2017 lenye kauli mbiu “uaminifu ni mabadiliko”. Katika ujumbe huo anasema, mada yao msingi waliyochagua kuhusu uaminifu ni mabadiliko, kilelezo msingi kinachotoa mshangao wa mantiki ambayo inatupelekea kufikiria hali halisi ya kuwa mwaminifu na uwezo wa kubadilika na hasa wa kufikiria uzoefu wa Ibrahimu katika Biblia anayeoneshwa kama mfano wa Imani. Alipokuwa mzee Mungu alimwambia: “Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha;”(Mw 12,1-2). Baba Mtakatifu anathibitisha, ili aweze kuwa mwamifu Ibrahimu alipaswa kubadili na kuondoka kama alivyo amriwa.

Neno la Mungu linasaidia kutofautisha sura mbili ya mabadiliko: kwanza ni ile ya imani, matumani na kujifungulia yaliyo mapya; ya pili ni ile ya matatizo ambayo yanafanya uache ule usalama uliozoea na kwenda kukutana na yale usiyo jua. Mabadiko hayo ni kutokana na mazoea ya kukaa mahali pamoja na kubakia katika utulivu, mahali ambapo umezungukwa na ukuta wa kukulinda na pia kuhifadhi,  au kurudia maneno yale yale, ishara zile zile daima zinazotufanya tujisikie na usalama zaidi, badala ya kuondoka na kujikita katika michakato iliyo mipya. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu anasema: ni wakati sasa wa kujiuliza ni kitu gani kinatokea, iwapo tunabaki na imani kwa Mungu na binadamu. 

Katika historia ya Ibrahimu matokeo ya kuitwa na Bwana yameonekana, kwa maana alibadili moja kwa moja maisha na kuingia katika historia mpya na ikafungulia upeo asiyo utegemea wa mbingu mpya na nchi mpya. Hiyo ni kuthibiths kwamba unapo mwitikia Mungu, daima kuna michakato mipya mingine inayojiokeza; Ni mambo mengi yanatukia  ambayo yanatupeleka mahali ambapo hatukutarajia. Kwa maana hiyo ni muhimu kufungulia daima michakato mipya na kwenda mbele,ni michato isiyo chukua nafasi bali inaendeleza michakato  halisi na ya dhati.

Imani kwa binadamu maana yake ni kutoka nje ya ndani mwako binafsi ili kukutana na utu kamili , sura yake, mahitaji ya ukarimu na uruma  ili kumfanya naye aondoke ndani ya kile kisichojulikana, na hata katika maisha ya pembezoni. Imani kwa binadamu maana yake ni kufungua macho na moyo kwa maskini, wagonjwa, wale wasiokuwa na kazi, waliojeruhiwa kutokana na sintofahamu, uchumi unaobagua na kuua, kuwafungulia wakimbzi wanaokimbia vurugu na vita. Uaminifu kwa binadamu maana yake ni kushinda nguvu za kujiweka kimbelembele na kujibinafsisha kwa nguvu na ubinafsi wa hali ya juu. Uaminifu kwa binadamu ni kutoa nafasi ya upendo mkuu kwa wengine, kupinga vishawishi kwa wale wasumbukao, ili kuwasha cheche za matumaini kwao.
Kwa namna hiyo uaminifu kwa Mungu na binadamu ndiyo mchakato unaoendelea na kuunda mabadiliko ndani mwetu na mabadiliko ya hali halisi katika kushinda hali ya kugandamana, badala yake kujikita kwa kina zaidi katika kuunda nafasi za ajira kwa vijana na kwa ajili ya kizazi endelevu. Mabadiliko ni ustawi na siyo tu wakati mambo yanakwenda vibaya, hata kama yanakwenda vizuri na kushawishika kupata matokeo.

Baba Mtakatifu pia anawewaomba watende huduma zao ili kuwafanya hata wengine washiriki mipango  hiyo, pia kutoa fursa ya nafasi ya kushirikishana kwa maana ya kupokea changamoto ya mabadiliko binafsi na kubaki waaminifu kwa Mungu na binadamu. Baba Mtakatitifu anasema kuwa lakini hiyo kwa maana nyingine inaweza kuonekana inapingana, lakini ki ukweli ndiyo safari ya kueleka katika mchakato ambao hausimamii katika nafasi tu inayotulinda, ya kubaki katika ubinafsi, nafasi ambazo tumezoea kwa jinsi yak ile kiitwacho “tumezoea kufanya hivyo”.

Mwisho anampa salama Askofu Zenti wa Verona anayekaribisha tamasha la 7 la Mafunzo kijamii ya Kanisa Katoliki na watu wote walioshirikia kuandaa. Akiwatakia matashi mema wa kutoa  mchango wa kusaidia misioni za Uinjilishaji katika Kanisa na Dunia ya kazi, uchumi na kisiasa.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya kiswahili ya Radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.