2017-11-24 16:22:00

Papa:Tuendelee na mchakato wa kuomba umoja hadi siku utakapotimia!


Tarehe 24 Novemba 2017, Baba Mtakatifu amekutana na wanachama wa Tume Mchanganyiko kwa ajili ya mazungumzo taalimungu kati ya Kanisa Katoliki na Kanisa la Assira la Mashariki mjini Vatican.Akitoa hotuba yake , ameanza kwa kuwakaribisha na kumshukuru Askofu Mkuu Meelis Zaia wa Kanisa la Mashariki kwa hotuba yake na kwamba amfikishie Salam za kindugu katika Bwana Patriaki Katolikos Mar Gewargis III, wa Kanisa la Assira akimkubuka kwa namna ya pekee alipokutana naye mwaka mmoja uliopita, ambapo anasema  ni katika  hatua za mchakato wa kukua kwa ukaribu na umoja kati yao.

Kukutana nao leo  Vatican, imetoa fursa ya kutazama kwa shukrani juu ya  safari iliyotimia ya Tume mchanganyiko kutokana na uthabiti uliofanywa wa kihistoria wa kutiwa sahini mjini Roma mwaka 1994 katika mchakato wa  imani moja ya fumbo la Bwana kufanyika mwili.Na katika hatua hiyo, Papa anasema, Tume mchanyiko ilikuwa na azimio la mpango wa hatua mbili: Kuhusu taalimungu ya sakramenti na juu ya katiba wa Kanisa. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu anamshukuru Mungu kutiwa  sahini ya hati ya pamoja inayotazama kwa ujumla maisha ya sakramenti. 

Anaongeza, kwa maana leo hii  wanaweza kutazama kwa matumaini ya kesho na kuomba Bwana aendeleze kazi hiyo kwa  mchango mkubwa kukaribia siku ile iliyobarikiwa na kutarajiwa kwa furaha katika kuadhimisha moja kwa moja muungano wa Kanisa la Kristo. Aidha Papa amependela kusisitiza juu ya Hati hiyo ya pamoja kuwa, kwayo ni ishara ya msalaba na kama ishara. inayoonesha katika maadhimisho yote ya sakramenti.

Akitoa mfano:  Baadhi ya wandishi wa Magharibi wameweka ishara ya msalaba kati ya mafumbo matakatifu, kwa kuamini kwamba kila adhimisho la sakramenti linategemea  Pasaka ya kifo na ufufuko wa Bwana. Ni jambo zuri la kuigwa kwasababu msulibiwa amefufuka, ni ukombozi wa maisha yetu:  Kwa  msalaba Mtakatifu wote tunategemea amani na kutoka kwa  umoja kati ya mafumbo matakatifu ambayo tunaadhimisha, hata kati yetu wote tulio batizwa na kushiriki kifo na ufufuko wa Bwana.(Rm 6,4).

Kwa njia ya msalaba tunaweza kukumbuka kuwa Bwana ni mwenye huruma na hamwachi hata mmoja ndugu, bali anawapokea wote, hata majeraha yao. Kwa njia ya kufanya ishara ya msalaba ni kutaka kukumbusha majeraha ya Kristo , majeraha ambayo hayakufutika kwa njia ya ufufuko ,lakini yakajazwa na mwanga. Kwa maana hiyo haya majeraha ya wakristo, hata yaliyofunguliwa, yakipitiwa na uwepo hai wa Yesu na upendo wake yanageuka kuwa mwanga na kuwa ishara ya mwanga wa pasaka katika ulimwengu uliokumbwa na giza.

Katika utamaduni wa Kisiria Baba Mtakatifu anasema, Kristo msalabani anawakilisha kuwa ni tabibu mwema na dawa ya maisha. Kwa njia hiyo, anaomba Bwana aweze kuponesha majeraha yote yaliyopita, hata kuponesha majeraha mengi katika dunia. Hiyo ni kutokana na kwamba, leo hii majanga ni mengi yalifunguka ya vurugua na vita. Amemaliza akiwaomba wafuate kwa pamoja hija hiyo ya mapatano na amani ambayo Bwana amefundisha.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.