2017-11-24 15:57:00

Papa:Makanisa yetu yawe ni kwa ajili ya kutoa huduma,yasigeuke masoko!


Kukesha, huduma na kujitoa: ni kati ya maneno yaliyo ongoza mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko katika Misa ya asubuhi ya tarehe 24 Novemba 2017 katika Kanisa la Mtakatifu  Marta mjini Vatican. Amesisitiza hayo akitafakari masomo mawili ya liturujia ya siku ikiwa somo la kwanza la Makabayo na Injili kutoka kwa Mtakatifu Luka zenye kuwa na mada ya pamoja  ambayo inahusu utakaso wa hekalu. Kama vile Yuda na ndugu zake walirudia kulitakasa na kulitabaruku hekalu kutokana na wapagani kuliharibu, ndivyo hata  Yesu anawafukuza wafanyabiashara katika nyumba ya Bwana na kuwambia wameigeuza kuwa pango la wanyang’anyi.

Wakati huo huo Baba Mtakatifu ameuliza swali ni kwa jinsi gani ya takasa hekalu la Mungu? Jibu lake ni kwa njia ya kukesha, kutoa huduma na kujitoa bure. La muhimu ni hekalu la Mungu ambalo ni moyo wetu,mahali ambapo Roho Mtakatifu anaisishi, lakini Baba Mtakatifu anaongeza kuuliza maswali mengi: je ni kitu gani kinatokea ndni ya moyo wangu? Nimejifunza kukesha ndani mwangu ili Roho Mtakatifu Peke yake aweze kukaa ndani ya hekalu hili?
Ni lazima kulitakasa hekalu , hekalu  ndani ya moyo wangu  na kukekesha, anathibitisha lakini pia na kuonya kwamba lazima ya kuwa makini kwa maana ni kujiuliza daima je ni kitu gani kinatokea ndani ya moyo? Maana  kuna anayekuja na anayeondoka, je ni mawazo gani, je unazungumza na roho Mtakatifu? Je unasikiliza roho Mtakatifu? Kwa njia hiyo  Kesheni! Ni muhimu kuwa makini kwa kile kinachotukia ndani ya mioyo yetu. Yesu yu hai kwa namna ya pekee katika wagonjwa, wanaoteseka, wenye njaa na wafungwa kwa maana alisema mwenyewe.

Katokana na uhakika wa maneno ya Yesu, Baba Mtaktifu anajiuliza: je ninatambua kutunza hekalu, je ninatambua kutoa huduma kwa hekalu? Je ninawasogelea kuwasaidia, kuwavalisha, kuwatuliza wenye kuwa na mahitaji,? Akitoa mfano zaidi anasema, mara nyingi  Mtakatifu Crisostom alikuwa akiwakaripia wale waliokuwa wanatoa sadaka nyingi ili  kupendezesha kwa mapambo mengi hekalu, wakati huo huo hawakuwa  wanasaidia wale wenye kuhitaji. Alikuwa akiwakalipia vikali na kusema hilo siyo jambo jema: Kwanza ni huduma na baadaye kutakasa hekaliuambalo ni watu wenyewe. Kwa kusisitiza zaidi amesema tunapowakaribia wengine na kuwahudumia na kuwasaidia ni kufanana na Yesu, kwa maana yeye yumo ndani mwao! 

Akiendelea na sehemu ya tatu kuhusiana na kujitoa bure, Baba Mtakatifu anafafanua na kuanza na mfano wa masikitiko: ni mara ngapi tunapoingia katika hekalu:  akifikiria kama vile parokia au uaskofuni na mahali pengine, wakati mwingine hatujuhi kama tuko katika nyumba ya Mungu au sokoni. Kwa maana  anasema yapo masoko mengi,  na hata kudiriki kuweka orodha ya gharama za sakramenti. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu anasema, upo ukosefu wa kujitoa bure. Lakini  Mungu aliyetukomboa bure, hakutufanya tulipe chochote.

Hata hivyo Baba Mtakatifu anasema, kwa mambo kama hayo wengi watasema, fedha ni lazima kwa ajili ya uendeshaji wa majengo ya Kanisa, kuwatunza mapadre nk, lakini pamoja na hayo anasisitiza, ni lazima kutambua kujitoa bure, kwa maana wewe unajitoa bure na Mungu atafanya zaidi. Mungu atafanya zaidi kile kinachokosekana. Makanisa yetu lazima yawe makanisa ya huduma na ya kujitoa bure.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.