2017-11-23 16:18:00

Papa:Wanawake ni mfano wa kuigwa kwa ujasiri wa kutunza imani !


Kutoa uhuru kwa vijana, kufuta kumbukumbu na kufundisha vijana ni mambo matatu  ambayo Baba Mtakatifu ametafakari, yanayoonekana katika utamaduni wa ukoloni na iitikadi  kwa kila nyakati. Ameyasema hayo wakati wa mahubiri ya misa  katika Kanisa la Mtakatifu Marta Mjini Vatican tarehe 23 Novemba 2017. Ni katika mwendelezo wa barua ya Makabayo iliyo anza tangu wiki iliyopita  ambayo inaeleza  historia ya mfalme wa Antioko Epifane dhidi ya waamini wa Makabayo kushikiria sheria za Mababu zao.

Akifafanaua zaidi anasema , kile kilichotokea kwa watu wa Mungu wakati ule, hata sasa yanatokea,hasa inapozuka katika ardhi udikteta moja kwa moja  wa utamaduni au itikadi ambazo ni ukoloni. Bila kutaja jina Baba Mtakatifu anatoa mfano, wakufikiria udikteta uliofanyika karne iliyopita katika Bara la Ulaya,pia amesema ni  mashule mangapi yal jengwa ili kudundisha kuondoa uhuru na kuunda historia kwa upya, kumbukumbu za watu, au kulazimisha mifumo ya elimu kwa vijana. Na zaidi nchi ngapi zilihaidiwa kupewa fedha,mara baada ya kuomba mkopo, lakini wenye masharti kwamba nitakupatia laki muhimu ufundishe mashuleni nitkavyo amuru yaani kuonesha hata  vitabu watakavyo tumia, ambavyo vilikuwa vimefuta mambo ya Mungu aliyoumba na jinsi ya kazi ya uumbaji.

Baba Mtakatifu ametoa mfano zaidi, kwamba, ilikuwa kutaka kufuta utofauti  na kufuta historia,  ambapo ilikuwa ni kulazimisha kwamba,  tangu leo ni kuanza kufikiria, asiye fanya hivyo atawekwa pembezoni au kuteswa, na ndiyo maana ya udikteta.  Hayo yalijitokeza Ulaya mahali ambapo udikite ulionesha uhalifu mkubwa, wengi hawakuwa na uhuru wa kujibu kwa maana kulikuwapo na aina nyingi za kuteswa kwa yule ambaye alikataa. Hiyo ina maana ya kwamba ukoloni wa kiitikadi na utamaduni wake unafuta uhuru na kumbukumbu na kusasabisha uongo mkubwa.

 Hiyo ni kwasababu inaoekana hata katika soma la kwanza, katika kitabu cha makabayo kulikuwapo na ushawishi, lakini ni  mahali ambapo Mama anawashauri watoto wake wawe na uvumilivu mbele ya kifo, kwa njia hiyo  anasisitiza  Baba Mtakatifu, nafasi moja muhimu aliyo nayo mwanamke ya kuhifadhi kumbukumbu na mizizi ya kihistoria. Ni Kuhifadhi kumbukumbu ya ukombozi, ya watu wa Mungu ambao walikuwa na nguvu katika imani, pamoja na kwamba waliteswa kutokana na ukoloni wa itikadi za utamaduni. Kumbukumbu inasaidia kushinda kila aina ya mfumo wa mafundisho tofauti. Ni kukumbuka ya thamani, kukumbuka historia, na kumbuka ya kila kitu ulicho jifunza chema.

Akiendela na ufafanuzi juu ya mama anayezungumzwa  mara mbili katika lugha ya mababu yaani lugha ya asili , Baba Mtakatifu anaongeza kuthibitisha kuwa,hakuna  aina yoyote ya ukoloni wa utamaduni inayoweza  kushinda na kufuta  kilugha. 
Ukarimu wa mwanamke na ujasiri kama wa mama katika somo ya makabayo ambaye alikuwa mwenye nguvu kwenye mizizi ya lugha ya asili ya Babu na katika kutetea watoto wake na watu wa Mungu, Baba Mtakatifu anasema, hiyo ni njia ya kufikiria nguvu za wanawake walizo nazo, kwani wanao uwezo wa kuvumilia mbele ya utamaduni wa ukoloni. Ni mama na wanawake ambao wanahifadhi kumbukumbu na lugha , wenye uwezo wa kutetea historia ya watu na kuonesha  amani ambayo wataalimungu baadaye wanafafanua zaidi.

Watu wa Mungu walikwenda mbele kwa ajili ya nguvu za wanawake wengi, ambao walitambua kuwaonesha na kuwafundisha watoto wao juu ya imani. Na kwa njia hiyo, wanawake wengi wanatambua kuonesha imani katika lugha yao ya asili hivyo Bwana atupatie neema hiyo na kwa Kanisa ya kuwa na kumbumbuku bila kusahau lugha ya asili ya babu zetu na kuendelea kuwa wanawake jasiri

Sr Anela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.