2017-11-23 09:29:00

Burke:Ni ziara ya kitume ya Papa katika nchi mbili za pembezoni!


Ni Ziara ya 21 ya kitume kimataifa ya Baba Mtakatifu Francisko ambayo ataelekea nchini Myanmar na Bangladesh kuanzia tarehe 26 Novemba hadi 2 Decemba. Ndiyo maelezo kamili yaliyotolewa na msemaji Mkuu wa Vatican,Bwana Greg Burke na kukumbusha juu ratiba ya safari yake, akisisitiza kuwa Baba Mtakatifu kwa nchi mbili barani Asia anapeleka ujumbe wa mapatano, msamaha na amani.

Mkutano uliofanyika tarehe 22 Novemba 2017 mjini Vatican Bwana Burke amesema kuwa, Baba Mtakatifu Francisko atakuwa na mkutano wa faragha tarehe 30 Novemba na kiongozi wa kijeshi wa Birmania Jenerali Min Aung Hlaing. Aidha  Bwana Burke  ameonesha kuwa, katika mkutano wa kidini na kiekumene kwa ajili ya amani ambao unatarajiwa kufanyaika tarehe 2 Desemba huko Dhaka nchini Bangladesh watakuwapo hata kikundi cha wakimbizi wa rohingya.

Kabla ya misa huko Dhaka, watoto wa mitaani wazawadia Baba Mtakatifu kandambili wanazotengeneza wao kwa mikono yao. Na kati ya watu watakao kuwa katika ziara ya Baba Mtakatifu, Bwana Grek Burke amesema hata mfanyakazi wa kilei katika kitengo cha uchapishaji Vatican. Akiwa katika nchi mbili atakazotembelea Baba Mtakatifu Francisko atasafiri kwa magari yaliyofungwa kawaida bila kuwa na ulinzi. Nchini Mynmara ,Baba Mtakatifu atapata malazi kwa Askofu Mkuu, wakati akiwa Bangaldesha atakwenda katika nyumba ya ubalozi wa Vatican nchini humo.

Kuhusiana na  ziara ya kitume ya Myanmar na Bagladesh Bwana Greg ameweza pia kuzungumza na waandishi wa habari wa Radio Vatican, akigusia juu ya hali halisi ya nchi hizi kwamba, katika nchi hizi mbili ni nchi za pembezoni, kwa maana mara nyingi Baba Mtakatifu anaongea sana juu ya maeneo ya pembezoni kwa maana hiyo ni kuonesha hali  halisi hata kwa jumuiya katoliki katika maeneo yote mawili ambayo ni wachache sana.

Akifafanua juu ya changamoto wanazokabilia katika  nchi hizi hasa ile ya umaskini,Bwana Burke anasisitiza kuwa , kwa mfano wa nchi ya Bangladesh imepita kipindi kigumu katika maendeleo, kwa njia hiyo ujumbe wa Baba Mtakatifu utakuwa ni wa kuleta matumaini na fursa katika nchi. Hata hivyo kuna jambo jingine muhimu hasa linalohusu mazungumzo ya kidini. Nchi ya myanmar inawakilisha  sehemu kubwa ya dhehebu la wabudha, na nchi ya Bangladesh rasmi ya serikali ya Kiislam. Bwana Burke anasema, Baba Mtakatifu hata hapa anataka kuoenesha kwa mara nyingine tena maana ya dini kwa ajili ya amani na kwa ajili ya mapatano.

Kama Baba Mtakatifu alivyokwisha watumia ujumbe kwa nchi hizi mbili kuwa anataka kuwaimarisha jumuia katoliki imani yao, anasema ni ziara ya kituma ambayo ina mantiki msingi kwa ngazi ya kichungaji. Na imeonekana mara nyingine Baba Mtakatifu anakwenda mbali sana kwa ajili ya kutazama jumuiya ndogo kwa maana hiyo ni msaada mkubwa na mtindo wake wa kuwaimarisha watu hao imani.

Akifafanua juu ya mikutano muhimu ambayo Baba Mtakatifu atakabiliana nayo, Bwana Burke anasema katika  nchi ya Myanmar, mkutano muhimu utakuwa ni ule wa kukutana na wabudha. Na katika nchi ya  Bangladesh utakuwa ni ule wa kidini,hasa ni fursa ya kurudi katika mada ya mahusiano kati ya dini. Kwa namna hiyo katika nchi zote mbili,ni vema kuona kwamba Baba Mtakatifu atamalizia ziara yake akikutana na vijana, na jumuiya ndogo katoliki ambazo zinaleta maana na  matumaini makubwa katika nchi hizo.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.