Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Katekesi siku ya Jumatano

Papa amesema,Misa ni kumbu kumbu ya Fumbo la Pasaka ya Kristo!

Baba Mtakatifu ameendeleza Katekesi yake sehemu ya 3 kuhusu mada ya maadhimisho ya Misa Takatifu.

22/11/2017 16:09

Ili kuweza kuendelea na Katekesi juu ya Misa, tunaweza kujiuliza: msingi wa misa ni nini?: Misa ni kumbukumbu ya Fumbo la Pasaka ya Kristo. Hiyo inatufanya tushiriki ushindi dhidi ya dhambi na kwa kuleta maana kamili ya maisha yetu. Ni maneno katika utangulizi wa Katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko tarehe 22 Novemba 2017 katika viwanja vya Mtakatifu Petro mjini Vatican katika mwendelezo wa sehemu ya tatu, kuhusu mada ya maadhimisho ya Misa Takatifu.

Ili kutambua thamani ya Misa, hawali ya yote ni lazima kutambua maana ya “kukumkumbu” kibiblia. Hiyo siyo tu kukumbuka matukio yaliyopita, bali uhakika kwa namna ya wakati uliopo na kufanya kukumbukumbu kwa kile kilichotendeka karne ishirini ziliyopita. Ni kwa namna hii Israeli anatambua ukombozi wake toka misri: Kila mara Pasaka inapoadhimishwa, matukio ya kutoka hufanywa yawepo katika ukumbuko wa waamini ili yalingana na maisha yao. (Katekisimu ya Kanisa Katoliki 1363).

Kwa njia ya mateso, kifo ufufuko na kupaa mbingu kwa Yesu Kristo umetuletea ukamilifu wa Pasaka. Misa ni kumbukumbu ya Pasaka yake, ya kutoka kwake ili kuleta ukamilisho wetu sisi na kufanya tuondokane na utumwa wa dhambi ,tupate kuingia katika  ahadi ya ufalme wa Mungu. 
Ekaristi daima itatupeleka katika upeo wa juu zaidi kutokana na matendo ya ukombozi wa Mungu: Bwana Yesu ambaye aliumega mkate kwa ajili yetu na kumimina juu yetu huruma yake na upendo wake alioonesha akiwa msalabani hivyo kuupyaisha moyo wetu, kuishi kwetu na namna yetu ya kuhusiana na Yeye na ndugu. Baba Mtakatifu anasema, Mtaguso wa Pili wa Vatican unasema: Kila mara inapofanyika sadaka ya msalabani ambayo ni Yesu Kristo kondoo wa Pasaka yetu aliyechinjwa, na kuadhimishwa juu ya altare, ni kufanya tendo la ukombozi  (Cost. dogm. Lumen gentium, 3).

Kila adhimisho la Ekaristi ni  mwonzi wa jua bila usio kuwa na  mawio yake ambaye ni Yesu Kristo. Kuudhuria Misa kwa namna ya pekee siku ya Jumapili, Baba Mtakatifu nathibitisha, maana yake ni kuingia katika ushindi wa Mfufuka, kuangazwa na mwanga wake pia na kupashwa joto kale. Kwa kuadhimisha Ekaristi na Roho Mtakatifu, inatufanya kushiriki maisha matakatifu ya Mungu ambaye ana uwezo wa kubadilisha kila mtu na utu wetu wa kufa.
Hatua za mchakato  wa kutoka kifo kufikia maisha mapya, na kipindi cha umilele Bwana Yesu anatusukuma hata sisi katika hatua zake ili kufanya naye Pasaka. Katika Misa tunaungana naye. Kwa maana, hakika Yeye anaishi nasi na sisi tunaishi naye kama anavyothibitisha Mtakatifu Paulo kuwa:“Maana mimi kwa njia ya sheria naliifia sheria ili nimwishie Mungu. Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu”.( » (Gal 2,19-20).

Damu yake inatupa uhuru ikiwa na maana ya  uhuru wa kifo  na hofu.Tunapata uhuru na si wa kimwili tu lakini pia kifo cha kiroho ambacho ni ubaya, dhambi ambazo mara nyingi tu waathirika, hata kuwasababishaia wengine. Kwa njia ya dhambi maisha yetu yanachafuka na kupoteza uzuri na maana yake ya kuchanua.  Badala yake Kristo ni ukamilifu wa maisha, tangu ashinde kifo na daima. Kanisa linathibitisa wakati wa maadhimisho ya Misa kuwa,  kwa ufuko wake alivunja vunja kifo na kukuunda maisha mapya. Pasaka ya Kristo ni ushindi wa maisha dhidi ya kifo, maana yeye alibadili kifo kwa kwa njia ya upendo upeo. Katika  Ekaristi, Yeye anataka kueleza upendo huo wa Pasaka yaani ushindi. Iwapo tunapokea kwa imani, nasi pia tunaweza kupenda kweli Mungu na jirani na kupenda kama yeye alivyo penda sisi kwa kutoa maisha yake.

Iwapo upendo wa Kristo huko ndani mwetu, tunaweza kutoa upendo mkamilifu kwa mwingine, aidha  kuwa na uhakika wa kina ya kwamba hata kama jiarani yangu atanikwaza siwezi kukwazika naye kabisa. Baba Mtakatifu ametoa mfano kuwa, wafiadini walitoa maisha yao  wakiwa na uhakika wa ushindi wa Kristo dhini ya kifo. Ni kwa njia ya uzoefu wa nguvu ya Kristo na  nguvu ya upendo, Nasi kweli pia tunao uhuru na kujitoa bila kuwa na hofu. Akitoa mifano kadhaa , amesema,tunapoingia katika misa ni kama vile tunakwenda njia ya msalaba, ndiyo fursa ya kutafakari Kalvario, na kutambua Yesu ni nani. Pamoja na hayo ametoa swali, je ni mara ngapi inatokea kujiuliza kipindi hicho, badala ya kuzungumza  na kupiga picha, au kama vile kidogo kufanya tamasha na maonesho? 

Hilo silo jambo zuri Baba Mtakatifu amesisitiza kwa mara nyingine kuwa, ndani ya misa yupo Yesu, lazima kubaki kimya,hata kulia, hata furaha za kukombolewa. Ni lazima kufikiria hayo tunapoingia katika misa: ninaingia katika njia ya Kalvario mahali ambapo Yesu alitoa maisha kwa ajili yangu. Na kwa namna hiyo mambo ya kufanya tamasha yanapotea, hata mazungumzo yanayo tuondolea umakini katika kuadhimisha jambo jema ambalo ni Misa na Yesu Kristo mshindi. Amemalizia na mawazo kwamba sasa imekuwa wazi jinsi gani Pasaka ipo hata leo hii inafanya kazi kila wakati tunapoadhimisha Misa, kwa maana ya kufanya kumbukumbu. Kushiriki Ekaristi tunaingia katika fumbo la Pasaka ya Kristo na kutupatia  uwezo wa kupitia kifo na Yeye ili  kuingia katika maisha.


Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

22/11/2017 16:09