2017-11-22 16:31:00

Papa amenzisha kitengo cha Tatu cha ofisi ya Ukatibu wa Vatican


Papa Francis ameanzisha kitengo cha Tatu cha Ofisi  ya Katibu wa Vatican ikiwa ni Sehemu ya Wafanyakazi wa Ofisi katika nafasi ya Kidiplomasia ya Vatican, ili  kuimarisha ofisi ya sasa ya Wajumbe katika Uwakilishi wa Papa. Habari hiyo imetangazwa rasmi tarehe 21 Novemba 2017 katika taarifa ya Katibu wa Vatican.

Kitengo hicho kitakuwa chini ya Katibu wa Nchi,ambaacho kitakuwa na mwakilishi kwa ajili ya kuwakilisha Vatican ambaye kwa sasa ni mons. Jan Romeo Pawlowsk.  Kitengo hiki kitakuwa na lengo la kuonyesha na kuwa karibu na Baba Mtakatifu na Wakuu wa Sekretarieti ya Serikali, na  Wafanyakazi  wenye wajibu wa Kidiplomasia. Ili kufikia  lengo lake, Mwakilishi wa Kipapa anaweza kupanga na kutembelea ofisi za Uwakilishi wa Papa  mara kwa mara..
Katika kitengo hiki  kwa namna hiyo,  kitajikita moja kwa moja katika masuala yanayohusu watu wanaofanya kazi au kuandaa huduma ya kidiplomasia ya Vatican  na kuandaa  kama vile uteuzi, mafunzo ya awali na ya kudumu, hali ya maisha na huduma, maendeleo, vibali vya ruhusa , nk.

Wakati wa kutekeleza kazi hizi, kitengo hiki kitafurahia haki ya  uhuru wake,  wakati huo huo kujitahidi kuanzisha ushirikiano wa karibu na Kitengo cha masuala Makuu ya uhusiano  (ambayo itaendelea kukabiliana na masuala ya jumla ya Uwakilishi wa Kipapa) na kitengo cha  Mahusiano na Nchi za nje (ambayo itaendelea kukabiliana na masuala ya kisiasa ya kazi ya Uwakilishi wa Vatican).

Kwa maana hii, Wajumbe  Wawakilishi wa Kipapa watashiriki, pamoja na Msaidizi wa Masuala ya Makuu na Katibu wa Mahusiano na Mataifa, katika mikutano ya kila wiki inayoandaliwa na kuongozwa na Katibu wa Vatican. Aidha mwakilishi wa kitengo hicho ataitisha na kuongoza mikutano maalum  ili kuandaa uteuzi wa Wawakilishi wa Kipapa. Na mwisho  atakuwa na jukumu, pamoja na Mkuu wa Chuo cha Kipapa cha Mafunzo ya Kanisa, kuhusu uteuzi na mafunzo ya wagombea.

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.