Baba Mtakatifu Francisko kama alivyo fanya kwa nchi ya Myanmar katika tukio la ziara yake ya kitume ambayo inakaribia, vilevile ametuma ujumbe wake kwa njia ya Video kwa waamini na raia wa nchi ya Bangladesh mahali ambapo anatarajia kufanya ziara ya kitume tarehe 30 Novemba hadi 2 Decemba 2017.
Katika ujumbe huo, Baba Mtakatifu anasema, wakati akijiandaa kutembelea nchi ya
Bangladesh siku chache zijazo, anatamani kuwatumia ujumbe wa salam za upendo wa kwa
watu wote; ambapo ni matarajio yake kuwaona na kukaa pamoja nao.
Ainafika kama mtumishi wa Injili ya Yesu Kristo, kutangaza ujumbe wa mapatano, msamaha
na amani. Kufika kwake ni kutaka kuwaimarisha jumuiya katoliki ya Bangladeshi katika
imani na ushuhuda wa Injili ambayo inafundisha hadhi ya kila mme na mke na kuwaalika
wafungue mioyo yao kwa ajili ya wengine hasa kwa walio maskini na wahitaji.
Wakati huo huo aidha, anatamani kukutana na watu wote kwa namna ya pekee kukutana
na viongozi wa dini huko Ramna. Baba Mtakatifu anaongeza, kwa sasa tunaishi kipindi
ambacho waamini na wote wenye mapenzi mema kwa kila sehemu wanaitwa kuhamasisha kwa
pamoja uvumilivu, heshima na kusaidiana mmoja na mwingine kama vile watu walio ndani
ya familia moja ya kibinadamu.
Kadhalika Baba Mtakatifu anao utambuzi ya kwamba watu wa Bangladesh wako katika jitihada
kubwa za kufanya maandalizi makubwa ya kumpokea, kwa njia hiyo anawashukuru! Anawaomba
kila mmoja kusali ili siku ambazo atakuwa katika ziara hiyo ziweza kuwa kisima cha
matumaini na kutiwa moyo kwa wote. Na juu yao wote na familia anawabariki kwa baraka
ya Mungu yenye furaha na amani.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |