2017-11-21 15:56:00

Papa amewatia moyo maaskofu wa Hungaria waliokutana naye mjini Vatican!


Baba Mtakatifu Francisko amekutana na kuzungumza na maaskofu wa Hungary Jumatatu 20 Novemba 2017 ambao wako katika ziara yao ya kitume mjini vatican. Katika mazungumzo yao na Baba Mtakatifu wamegusia mada nyingi hasa za utajiri na uzalendo wa nchi ya kale ya Bara la Ulaya, kama vile hata mada msingi zinazohusiana na  ushirikishwaji, wahamiaji , wakimbizi na zaidi wakristo wanaoendelea kuteswa.  Kabla ya kukutana nao, Baba Mtakatifu Francisko amebariki Msalaba ambao utaweza kusimamishwa wakati wa Kongamano la Kimataifa la Ekaristi nchini Hungary, linalotarajiwa kuanza tarehe 13 hadi 20 Septemba 2020. 

Hata hivyo Kardinali Peter Erdo Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la  Esztergom-Budapest ameelezea kwa namna ya pekee juu ya mkutano wao kwa njia ya simu na vyombo vya habari vya radio Vatican kwamba, mkutano wao ulikuwa mzuri kwani  mara ya mwisho ya mkutano ulikuwa ni ule wa mwaka 2008 na sasa imepita miaka 9 ambapo changamoto za sasa zinazidi kuongezeka kwa upande wa Kanisa na jamii ya Hungary. 

Kardinali Erdo anasema, wamaeweza kushirikishana na Baba Mtakatifu  juu ya changamoto zinazokumba Kanisa la Hungary na kwamba leo hii wanaishi kipindi cha ulimwengu wa utandawazi mahali ambapo siyo rahisi kutazama na kubaki tofauti kama Kanisa  mbele ya watu wahitaji na maskini kwa njia hiyo Kanisa la Hangury linajitahidi kujikita kadiri ya uwezo wao kusaidia wahitaji.

Anafafanua kuwa  zaidi kuwa baada ya kuanguka kwa utawala wa kikomunisti Kanisa la Hungary limejaa wenye heri mashahid pia hata wengine wanasubiri kutangazwa mwenye heri kama vile mtumishi wa Mungu János Brenner shahidi wa Ekaristi lakini pamoja na hayo  wapo wengine watatu ambao wako kwenye mchakato. Anasema  kuwa hiyo imeleta mwamko  mkuu na mmoja wa nguvu katika  Kanisa la Hungary ambako asilimia 60% ni wakatoliki na asilimia 20% kutoka katika makanisa mengine, pamoja na hayo  wanajitahidi katika mazungumzo ya kiekumene na ile ya kujikita kwa kina katika elimu, hasa mafunzo ya kichungaji kwa watu wanao baguliwa pia kuwashirikisha  watu wa kabila la Warom.

Sr Angela rwezaula
Idhaa ya kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.