Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa \ Kanisa Ulimwenguni

Uturuki:Hakuna ruksa kusitisha mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi!

Mwendelezo wa Mkutano wa mwaka jana ambao walisisitiza Mataifa kuona wajibu wake katika kutunza mazingira kama hatua muhimu katika katika kupambana na umaskini duniani, wimbi la uhamiaji na ukosefu wa usalama. - REUTERS

20/11/2017 09:28

Barua ya kichungaji ya mwaka huu kwa waumini Waotodosi duniani kote, iliyotolewa na Upatriaki wa Kiekumeni wa Costantinople, kwa ajili ya utetezi wa kutunza mazingira ya Dunia, kwa mara nyingine inatoa wito kwa dunia kutafakari hali ya dunia na kama kijiji kimoja kwa kuzingatia mwelekeo unaotajwa katika hati ya makubaliano ya Paris juu ya utunzaji wa mazingira. Aidha barua hiyo inakumbusha juu Kanisa kwa Mkutano wa COP 22, ambamo walisisitiza Mataifa kuona wajibu wake katika kutunza mazingira kama hatua muhimu katika katika kupambana na umaskini duniani, wimbi la uhamiaji na ukosefu wa usalama.

Barua hiyo ya kichungaji kwa Waorthodosi wote,  imerejea pia wito wa Patriaki Batholomew I ambamo aliomba tarehe Moja Septemba iwe ni  siku ya sala ya kuombea viumbe wa Mungu dhidi ya uhalifu wa kibinadamu, na pia Azimio la pamoja na Papa Francisko linaloeleza kwamba, hapawezi kuwa na jibu la kweli katika kupambana na kipeo cha ekolojia na mabadiliko ya tabia nchi bila ya kuwa na jawabu thabiti la pamoja.

Hivyo barua ya kichungaji ya Waotodosi , imeendelea kuonyesha kujali kwamba,  kipeo cha ekolojia na mabadiliko ya tabia nchi kineendelea kukuzwa siku hadi siku na watu wanaonekana kuziba masikio dhdi ya rufaa zinazotolewa kwa ajili ya utunzaji wa ekolojia na mazingira.
Katika ujumbe wake wa mwisho, Patriaki wa Kiekumeni wa Constatinople, amegeukia kishawishi cha wanadini, wanasayansi na wanasiasa , kwamba kwa juhudi zao, wanaweza kuhimiza jumuiya za waumini na viongozi, kufanya mabadiliko ya kuonekana, na katika kizishawishi serikali na taasisi, kutoacha kutimiza wajibu wao wa kimaadili katika kutunza dunia yetu. Na hviyo ni jambo lisilokubalika kurudisha nyuma juhudi zilizokwisha anzishwa, badala yake ni kusonga mbele kwa kasi yote.

Janeth Mhella
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

20/11/2017 09:28