2017-11-20 16:03:00

Papa ametuma salam za rambi rambi kufuatia kifo cha Kard.Andrea Cordero!


Baba Mtakatifu anaonesha masikitiko makubwa kufuatia kifo cha Kardinali Andrea Cordero Lanza di Montezemolo, Askofu Mkuu wa  mstaafu wa Kanisa Kuu la Kipapa la Mtakatifu Paulo nje ya Ukuta mjini Roma. Barua yake aliyo mtumia  dada yake, Adriana Cordero Lanza di Montezemolo, Baba Mtakatifu anasema  Kardinali Andrea alikuwa mtu wa Kanisa, aliyeishi kwa imani na matumaini  katika kipindi chake cha maisha ya kikuhani, akitumikia Injili na Vatican. Aidha anakumbuka kazi yake ya kutume kuwakilisha ubalozi wa Vatican katika nchi nyingi kwa namna ya pekee Papua Guinea, Nikaragua, Hunduras, Uruguay , Israeli , Italia, mahali ambapo alijikita kwa upendo mkuu na hekima kwa wema wa watu, kama vile katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo.

Kardinali Andrea Cordero Lanza di Montezemolo alizaliwa huko Torino Italia tarehe 27 Agosti 1925. Tarehe 15 Oktoba 2016 Baba Mtakatifu alikwenda kumtembelea katika nyumba ya matunzo ya Villa Betania aRoma mahali ambapo alikuwa amelazwa.
Mazishi yatafanyika tarehe 21 Novemba 2017 saa tano na nusu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, ambapo misa itaadhimishwa na Kardinali Giovanni Battista  dekano msadizi wa Baraza la Makardinali na Baba Mtakatifu anataongoza sehemu ya mwisho  ya ibada ya mazishi. Kufuatia kifo cha Kardinali Andrea Cordero Lanza,Baraza la makardinali wanabaki 217, ambao kati yao wenye haki ya kuchagua 120 na wasio na haki ya kuchagua ni 97.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.