2017-11-19 15:27:00

Papa:Tuwe na matumaini na kuondoa hofu juu ya zawadi za Mungu!


Katika Domenika ya mwisho  ya Mwaka wa kiliturujia, Injili inaelezea juu ya talanta (Mt 25,14-30). ya kwamba Bwana  mmoja kabla ya kwenda safari aliwakabidhi watumwa wake talanta, na kipindi cha wakati uli talanta hizo zilikuwa ni fedha zenye thamani kubwa:mmoja alipokea talanta tano, mwengine mbili na mmoja moja kwa mujibu wa uwezo wa kila mmoja. Aliye pokea tano alikwenda akazalisha nyinge tano. Na hata mtumwa wa  pili vile vile akaleta talanta nyingine mbili. Lakini aliyepokea moja alichimba shimo ardhini akaifukia talanta ya Bwana wake.

Ni mahubiri aliyo anza nayo Baba Mtakatifu Francisko wakati wa sala ya Malaika wa Bwana Jumapili ya tarehe 19 Novemba wakati Kanisa linadhimisha mwaka wa I wa Siku ya Maskini duniani. Baba Mtakatifu akiwahubiri mahujaji wote waliofika katika viwanja vya Mtakatifu Petro anasema:
Ni mtumwa mwenyewe katika Injili anayeeleza sababu ya ishara yake kuwa, Bwana analitambua kuwa wewe u mtu mgumu ,wavuna usipopanda wakusanya usipotawanya; bali nikaogopa nikaenda nikaificha talanta yako katika ardhi (taz Mt 25, 24-25).

Baba Mtakatifu anafafanua kuwa  mtumwa huyo anaonesha jinsi hasivyokuwa na matumaini kwa Bwana wake maana yake na hofu na ndiyo kizingiti. Hofu daima inagandamiza, daima inafanya ukosee uchaguzi. Hofu inakatisha tamaa ya kuanza mambo mapya, badala yake ni kukimbilia katika kutafuta suluhisho la haraka na uhakika, lakini ambayo itakufanya kushia kutenda jambo lisilo jema. Ili kwenda mbele na kukua katika safari ya maisha, ni lazima kuwa na imani, anathibitisha Baba Mtakatifu.

Somo la Injili hii linatutaka tutambue umuhimu wa kuwa na mawazo ya kweli juu ya Mungu. Tusifikirie kuwa yeye ni Bwana mbaya, mgumu na mkali anayetaka kuadhibu. Iwapo ndani ya mioyo yetu kuna mawazo potofu juu ya Mungu, basi maisha yetu kamwe hayatazaa matunda,  kwani tutaishi kila wakati na hofu ambayo haitatifanya kutenda lolote la msingi katika maisha. Tunaalikwa kutafakari na kugundua mtazamo wa kweli juu ya Mungu. Katika maandishi ya kale tayari Yeye alikuwa amejionesha kuwa ni Mungu mwenye  wingi wa huruma na mkarimu, si mwepesi wa hasira bali tajiri wa upendo na mwaminifu ( Kut 34,6).

Baba Mtakatifu ameongeza, daima Yesu alituonesha Mungu kuwa siyo Bwana mkali na asiye jali, Yeye ni baba aliyejaa upendo, upole na ukarimu, kwa njia hiyo lazima kuwa na imani kubwa kwake yeye.  Yesu ameweza kuonesha ukarimu na upendo wa Baba kwa njia nyingi: kwa mfano katika Neno lake, ishara zake, kuwakaribisha wote hasa wale wadhambi, wadogo na masikini, kama vile  Siku ya leo,  ikiwa ni ya kwanza ya Maskini Duniani. Lakini pia kwa njia ya kuonya kwa maana ya binadanu  kutojali maisha. Hiyo ni ishara ambayo Mungu napendelea tuwe nayo hasa ile ya utambuzi wa kujihusisha na kuwajibika kwa kila aina ya tendo na hasa kwa ajili ya ndugu zetu wahitaji.

Baba Mtakatifu anaendelea, Injili ya talanta inatualika tuwajibike binafsi na kuwa na matumaini ambayo yanajikita kuendelea katika njia mpya bila kuichimbia talanta chini ya ardhi,yaani zawadi za Mungu tulizo kabidhiwa maana tunatulizwa siku ya mwisho!
Bikira Maria atuombee ili tubaki waaminifu katika utashi wa Mungu na kuongeza zaidi talanta tulizokabidhiwa, kwa kufanya hivyo tuweza kuwa msaada kwa wengine na katika siku ya mwisho tutapokelewa na Bwana ambaye anatualika kushika nafasi katika furaha yake.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.