2017-11-18 16:59:00

Papa Ratzinger akutana na washindi wa tuzo ya Ratzinger!


Jumamosi Baba Mtakatifu Francisko alikabidhi tuzo ya 17 kwa washindi watatu,wa  Tuzo ya Ratzinger,  akiwepo pia Kardinali Kurt Koch, mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya ukuzaji wa Umoja wa Wakristo. Washindi hao siku ya  Ijumaa, walikutana na  Papa Mstaafu Benedikto XVI,  mjini Vatican. Washindi ni  Wanateolojia  Theodor Dieter Mluteri, Padre Karl Heinz Mkatoliki naArvo Part Mtunzi wa muziki Mtakatifu.


Chanzo cha habari  kimeutaja mkutano wa Papa Mstaafu Benedikto XVI, na washindi hao kwamba, mazungumzo yao yalikuwa makini na tulivu, akiwepo pia Mkuu wa Shirika la Ratzinger  Padre Federico Lombardi. Wakati wa tukio hili, lilipambwa na wimbo wa Baba Yetu, uliotungwa na Arvo Part, mwaka 2011 kwa ajili ya adhimisho la miaka 60 ya Upadre kwa Papa Mstaafu Benedikto XVI. Kutolewa kwa tuzo hii kwa mara ya kwanza kwa msanii , inaoneysha jinsi Papa Mstaafu Benedikto XVI, alivyo na mapenzi kwa muziki na sanaa iliyowajongeza watu katika ukweli na katika kukutana na Mungu.

Janeth Mhella

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.