2017-11-17 15:21:00

Papa:Ujumbe kwa njia ya Video kwa ajili ya Ziara ya kitume nchini Myanmar


Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe wake kwa njia ya Video katika maandalizi ya ziara yake ijayo nchini Myanmar na katika Ujumbe anasema, wakati akijandaa kutembelea Myanmar anapenda kuwasalimia kiurafiki watu wote wa nchi na kwamba ni shahuku ya kukutana nao mapema karibuni. Aidha anasema, anafika kule kutangza Injili ya Yesu Kristo, ujumbe wa mapatano, msamaha na amani. Ziara yake ni kutaka kuwaimarisha  na kuwatia moyo wanajumuiya Katoliki nchini Myanmar wawe na imani kwa Mungu na kutoa ushuhuda wa Injili ambayo inafundisha hadhi ya kila mtu mme na mke katika kufungua mioyo yao kwa wengine hasa kwa ajili ya maskini na wahitaji.

Pamoja na hayo Baba Mtakatifu anasema ni shahuku kubwa kutembelea nchi hiyo kwa moyo na heshima ili pia kuwatia moyo kwa kila jitihada katika sura ya kujenga umoja na mshikamano kwa huduma kwa ajili ya wema wa wote. Baba Mtakatifu anathbitisha kuwa, kwa sasa tunaishi kipindi ambacho binadamu wote wenye mapenzi mema wanahisi daima ulazima wa kukua na kuwa na uelewa, heshima na kusaidiana mmoja na mwingine ndani ya familia moja ya kibinadamu yaani ya watoto wote wa Mungu.  

Anatambua vilevile  ya kwamba, watu wa Myanmar wanafanya  kila  jitihada  kuandaa ziara yake;  hivyo anawashukuru!  Aidha kutokana na ziara hiyo anawaomba kila mmoja aweza kusali ili  ziara yake  iweze kuwa chem chemi ya matumaini  na kutiwa moyo watu wote. Wote amewabariki na baraka  za kitume zenye furaha na amani, akitarajia kuwaona mapema iwezekanavyo!


Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.